settings icon
share icon
Swali

Je, Mungu ni mwenye enzi ama tuna hiari huru?

Jibu


Tunapoongea kuhusu hiari huru, kawaida tinajali suala la wokovu. Tungependa kijua ni nani haswa anadhibiti mwelekeo wetu wa milele.

Majadiliano yoyote ya hiari huru ya binadamu lazima yaanze na ufahamu wa asili ya binadamu kwa sababu hiari ya binadamu imefungana na asili hiyo. Mfungwa ana uhuru wa kwenda juu na chini katika kijumba chake lakini ameshinikzwa na kuta za kijumba hicho na hawezi kwenda nje haijalishi jinsi anavyotamani kufanya hivyo. Ndivyo ilivyo kwa wanadamu wote. Kwa sababu ya dhambi, watu wamefungwa ndani ya seli za ufisadi na uovu ambao umeingia ndani yetu. Kila sehemu ya binadamu iko katika utumwa wa dhambi -miili yetu, akili zetu, na mapenzi yetu. Yeremia 17:9 inatuambia kuhusu hali ya moyo wa binadamu: "huwa ni mdanganyifu na hauwezi kuponywa." Katika hali yetu ya asili isiyo na uvumilivu, sisi ni wenye nia ya kimwili wala sio ya kiroho. "Kwa kuwa na nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii" (Warumi 8:6-7). Mistari hii inatuambia kwamba kabla ya kuokoka tunakuwa na uadui au vita na Mungu, hatujajisalimisha kwa Mungu na kwa amri yake, na pia hatuna uwezo wa kufanya hivyo. Biblia ni wazi kwamba, katika asili yetu, wanadamu hawezi kuchagua kilicho chema na takatifu. Kwa maneno mengine, hatuna "hiari huru" ili kumchagua Mungu kwa sababu hatuna hiari huru. Imeshinikizwa na asili yetu, jinsi vile mfungwa ameshinikizwa na kijumba chake.

Basi mtu anawezaje kuokolewa? Waefeso 2:1 inaelezea mchakato huo. Sisi ambao "tumekuwa wafu kwa makosa yetu na dhambi zetu" tumefanywa "kuwa hai" kupitia Kristo. Mtu aliyekufa hawezi kujifufua kwa sababu yeye hana uwezo wa kufanya hivyo. Lazaro alilala katika kaburi lake siku nne, hakuweza kufanya lolote kujifufua. Kristo akaja na akamwamuru afufuke (Yohana 11). Ndivyo ilivyo nasi pia. Tumekufa kiroho, na hatuwezi kufufuka. Lakini "Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi" (Warumi 5:8). Yeye anatuita kutoka kwa kaburi zetu za kiroho na kutupatia asili mpya, ambayo haaina uchafu wa dhambi kama vile asili ya zamani ilivyokuwa (2 Wakorintho 5:17). Mungu aliona hali ya kukata tamaa ya nafsi zetu, na kwa upendo wake mwingi na rehema, mwenye enzi alichagua kutuma mwanawe msalabani ili atukomboe. Kwa neema yake tumeokolewa kupitia karama ya imani ambayo anatupatia ili tuweze kumwamini Yesu. Neema yake ni karama ya bure, imani yetu ni karama ya bure, na wokovu wetu ni karama ya bure inayopewa wale ambao Mungu amechagua "kabla ya kuweka msingi wa ulimwengu" (Waefeso 1:4). Kwanini alichagua kufanya kwa njia hii? Kwa sababu ilikuwa "sawasawa na uradhi wa mapenzi yake, kwa utukufu wa neema yake" (Waefeso 1:5-6). Ni muhimi kuelewa ya kwamba mpango wa wokovu umeundwa ili kuleta utukufu kwa Mungu wala sio binadamu. Mwitikio wetu ni kumsifu kwa "utukufu wa neema yake". Ikiwa tungechagua wokovu wetu wenyewe, ni nani angepata utukufu? Ni sisi, na Mungu ameweka wazi kwamba hatatoa utukufu anaostahili Yeye kwa mtu mwingine (Isaya. 48:11).

Swali ibuka ni, tanapata kujua aje ni nani ameokoka "kutoka kwa msingi kwa ulimwengu"? Hatuwezi kujua. Ndio maana tunachukua habari njema ya wokovu kupitia Kristo hadi mwisho wa dunia, tukiwaambia wote watubu na kupokea karama ya Mungu ya neema. Wakorintho wa pili 5:20 inatuambia tunapaswa kuwaomba wengine wapatanishwe na Mungu kabla muda kuyoyoma. Hatuwezi kujua ni nani mungu atachagua kumwachilia kutoka vijumba vyao vya gereza ya dhambi. Tunamwachia chaguo hilo na kupeleka injili kwa wote. Wale wanaokuja kwake Yesu "hatatupa nje" (Yohana 6:37).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mungu ni mwenye enzi ama tuna hiari huru?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries