settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu aliruhusu majanga ya asili, mitetemeko ya ardhi, vimbunga, na sunami?

Jibu


Ni kwa nini Mungu aliruhusu mitetemeko ya ardhi, kiluwiluwi, vimbunga, sunami, miporomoko ya ardhi, na majanga mengine ya asili? mwishoni mwa mwaka 2004 janga la sunami liloikumba Asia, upepo mkali ulioikumba Marekani ya kusini mwaka wa 2005, na 2008 kimbunga huko Myanmar vilfanya watu wengi kuuhoji wema wa Mungu. Ni jambo la kusikitisha kwamba majanga ya asili mara nyingi yanakisiwa kuwa “matendo ya Mungu” huku hakuna utukufu wowote kwa Mungu kwa miaka mingi, miongo kadhaa, au hata karne ya hali ya hewa ya amani. Mungu aliyeumba ulimwengu wote na sheria za asili (Mwanzo 1:01). Wingi wa majanga ya asili ni matokeo ya sheria hizi zatimia. Vimbunga, tufani, na upepo mkali ni matokeo ya mifumo tofauti ya hali ya hewa mbumburisho. Mitetemeko ya ardhi ni matokeo ya muundo wa kisahani wa dunia ambao wabadilisha dira ya sunami ukisababishwa na tetemeko la ardhi chini ya maji.

Biblia inatangaza kwamba Yesu Kristo anaiunganisha asili ya dunia pamoja (Wakolosai 1:16-17). Mungu anaweza kuzuia majanga ya asili? Kabisa! Je, Mungu wakati mwingine ushawishi hali ya hewa? Naam, kama tunavyoona katika Kumbukumbu 11:17 na Yakobo 5:17. Hesabu 16:30-34 inaonyesha kwamba Mungu wakati mwingine husababisha majanga ya asili kama hukumu dhidi ya dhambi. Kitabu cha Ufunuo kinaelezea matukio mengi ambayo yanaweza dhahiri kuwa kama ilivyokwisha elezwa juu ya majanga ya asili (Ufunuo sura ya 6, 8, na 16). Je! ni kila maafa ya asili adhabu kutoka kwa Mungu? La.

Kwa njia ile ile ambayo Mungu anaruhusu watu wabaya kwa kufanya vitendo viovu, Mungu anaruhusu duniani kutafakari matokeo ya dhambi ambayo yamekuwa juu ya viumbe. Warumi 8:19-21 inatuambia, “Viumbe vyote vinatazamia katika hamu matarajio ya wana wa Mungu kufunuliwa. Kwa maana, viumbe viliwekwa katika hali ya kuchanganyikiwa, si kwa hiari yake mwenyewe, lakini kwa mapenzi yake aliyevitiisha katika tumaini kwa kuwa viumbe vyenyewe vitaokolewa kutoka utumwa wa kuoza na kuletwa katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.” kuanguka kwa wanadamu katika dhambi kulikua na madhara juu ya kila kitu, ikiwa ni pamoja na dunia tunamokaa. Kila kitu katika viumbe kiko chini ya “kuchanganyikiwa” na “kuoza.” Dhambi ndiyo sababu kuu ya majanga ya asili, vile ilivyo sababu ya kifo, ugonjwa, na mateso.

Tunaweza kuelewa ni kwa nini majanga ya asili hutokea. Chenye hatuelewi ni kwa nini Mungu anayaruhusu majanga hayo kutokea. Ni kwa nini Mungu aliruhusu sunami kuua juu ya watu 225,000 katika Asia? Kwa nini Mungu aliruhusu kimbunga kuharibu maelfu ya nyumba za watu? Kuna jambo moja, matukio kama hayo huitingisha imani yetu katika maisha haya na kutulazimisha kufikiri juu ya maisha ya milele. Makanisa kawaida hujaa watu baada ya maafa. Baada ya watu kutambua jinsi maisha yao ni ya mwembamba na kwa kweli vile jinsi maisha yanaweza kuchukuliwa papo hapo. Tunachojua ni hiki: Mungu ni mwema! Wingi wa miujiza ya ajabu ulitokea wakati wa majanga ya asili ambao ulizuia hasara hata zaidi ya maisha. Majanga ya asili kusababisha mamilioni ya watu kutazama upya vipaumbele vyao katika maisha. Mamia ya mamilioni ya madola katika misaada hutumwa kuwasaidia watu ambao wanateseka. Huduma za kikristo zina fursa ya kusaidia, kuhudumia, shauri, ombea, na kuongoza watu kwa imani inayookoa katika Kristo! Mungu anaweza, na huleta mema makubwa nje ya majanga ya kutisha (Warumi 8:28).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu aliruhusu majanga ya asili, mitetemeko ya ardhi, vimbunga, na sunami?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries