settings icon
share icon
Swali

Ikiwa Mungu yuko kila mahali, hiyo inamaanisha kuwa yuko kuzimuni?

Jibu


Kuwepo kila mhali kwa Mungu ni mojawapo ya sifa zake asili. Haki yake pia ni asili, na kwa hivyo, ni sharti yeye kuadhibu wenye dhambi ambao hamwamini Yesu kwa wokovu. Kwa hivyo tunaye Mungu anasunguziwa kuwa kila mahali na bado anadumisha mahli kuitwao kuzimu, ambao kunaelezewa kuwa mhali ambapo ni kwa watu ambao wemeondolewa mbele zake (ona Mathayo 25:41).

Vifungu vitatu hasa ni vya maana kwa mjadala huu. Cha kwanza ni Zaburi 139:7-12, ambapo Daudi anasema, " Nikimbilie wapi ambako roho yako haiko? Niende wapi ambako wewe huko? Nikipanda juu mbinguni, wewe upo; nikijilaza chini kuzimu, wewe upo. Nikiruka hadi mawio ya jua, au hata mipakani mwa bahari, hata huko upo kuniongoza; mkono wako wa kulia utanitegemeza. Kama ningeliomba giza linifunike, giza linizunguke badala ya mwanga, kwako giza si giza hata kidogo, na usiku wangaa kama mchana; kwako giza na mwanga ni mamoja." kuzumu ni neno pana na halifanani na jehanamu, neno linalotumika mara nyingi kwa kurejelea mahali pa hukumu ya milele.

Wathesalonike wa Pili 1:7-9 yasema kwamba wale wote ambao hawamjui Mungu "adhabu yao itakuwa kuangamizwa milele na kutengwa mbali na utukufu wake mkuu." Huku Ufunuo 14:10 yasema yeyote anayemwabudu mpinga Kristo "mtu huyo atateseka ndani ya moto wa madini ya kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele ya Mwanakondoo." Aya hizi mbili sinakanganya sana taka mada hii kwa sababu mkanganyo wao ulio wazi. Hata hivyo, kunalo elezo rahisi linalopatikana katika neno la asili la Kiyunani.

Katika Ufunuo 14:10, "mbele ya" limetafsiriwa kutoka kwa Kigiriki enopion, ambalo linamaanisha "mbele ya, kabla." Hili ni neno la umbali, linalo onyesha umbzli, umbali unaopimika. Kwa ulinganisho, neno lililotafsiriwa "mbele ya" katika 2 Wathesalonike ni prosopon (uso), ambalo mara nyingi linarejelea uso wa mtu, au mwonekano wa sura. Paulo anaonekana kuchukua moja kwa moja kutoka Isaya 2:10 vile lilivyo katika Biblia ya Kiebrania. Kunayo marejeleo mengine juu ya Mung una watu Wake wakiwa "wametengwa," hata huku duniani. Kilio cha Yesu cha uchungu msalabani ni mfano mmoja (Mathayo 27:46; Marko 15:34). Mwanatheologia Dkt. Louis Berkhof anafundisha kwamba Paulo anamaanisha "kutokuwepo kwa neema ya Mungu." Elezo hili la kuzimu linawakilisha kinyume halisi cha mbinguni. Mbingu hutoa baraka na utele sio kwa sababu ya karibu na Mungu kiroho, bali kwa kuwa katika ushirika kamili naye. Kuzimu inahuzishwa na kutokuwa na bahati ya baraka kwa sababu ya kuteleza kutoka kwa ushirika na Mungu.

Mwishowe, inaonekana kuwa Mungu kwa hakika "yuko" hata kuzimuni, au kuzimu imo mbele yake, inalingana ni namna gani mtu anatizam jambo hili, Mungu mile yote atabaki kuwa kila mahali. Mile atajua chenye kinaendela kuzimuni. Ingawa, hoja hii haimanishi kuwa roho ambazo zimefungwa huko zitakuwa na uhusiano na Mungu au mawasiliano yoyote Naye.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ikiwa Mungu yuko kila mahali, hiyo inamaanisha kuwa yuko kuzimuni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries