settings icon
share icon
Swali

Je Mungu ana mwili halisi?

Jibu


Biblia na falsafa mzuri zote zimenakili kuwa Mungu ni roho isiyoonekana. Katika Yohana 4:24 inasemkana kwamba Mungu ni roho (angalia pia Luka 24:39; Warumi 1:20; Wakolosai 1:15; 1Timotheo 1:17). Kwa sehemu hii ndio maana ni kwa nini hakuna kitu chochote kilitumika kumwakilisha Mungu (Kutoka 20:4). Lakini hii pia inaweza kuonyeshwa kwa kuangazia juu ya kile Mungu alicho. Kifalsafa kweli hiyo hutimia. Yote iliyoumbwa ina mwisho na ukadri. Lakini mwanzilishi wa kwanza ambaye ni (Mungu) hakuumbwa, na kwa hivyo hana mwisho. Kile kilicho zaidi ya mwisho, kwa ufafanusi, kiwe kisicho na mwisho, na biblia inasema kuwa Mungu yuu zaidi ya viumbe vyote (1 Wafalme 8:27; Ayubu 11:7-9; Isaya 66:1-2; Wakolosai 1:17). Kile kilicho cha na mwili hakiwezi kuwa cha milele-kwa sababu hauwezi ongeza sehemu iliyo na mwisho pamoja hadi iafikie kutokuwa na mipaka. Kwa hivyo Mungu ni roho kinyume na mwili halisi katika Uungu wake. Hii haimanishi hawezi kujidhihirisha kimwili. Mungu sio uchachu uliounganishwa au kitu chochote cha kinachofikiriwa. Pia hawezi kadirika, sio anga, na hana eneo mahalum (uwepo ni dhana tofauti).

Kujua ukweli huu unaweza tusaidia kuelewa hotuba ya kimajazi ambayo mara nyingi imetumika kuelezea juu ya Mungu au mara nyingi hatua ya Mungu katika maandiko. Kwa Mungu, pindi tu dhana iliyo na mwisho imetolewa kutoka kwa tangazo, chenye hubaki ndio hakika kweli. Ikiwa hakuna chochote kimebaki, basi itakuwa ni methali tupu. Baadhi ya methali huchukua sifa kutoka kwa kiumbe chenyewe (2Samueli 22:3). Wengine hutumia sifa za mwanadamu (kimajazi-Kumbukumbu 33:27). Katika njia hii tunaweza kuanzia toka kwa kile tonachokijua kupitia usoefu wetu hadi kwa kile tunachokijua kupitia methali. Kwa mfano, wakati maandiko yanamwelezea mkono wa Mungu ulio na nguvu, kwa kawaida tunajua katika fafanusi kuwa mikono ina mwisho-lakini pengine haiwezi kuwa. Kwa hivyo mkono wa Mungu hauna mipaka ya nguvu ya kutenda (chenye tunaita kuwa mwenye enzi). Wakati maandiko yanaelezea mawazo ya Mungu, tunajua kwamba mawzao yana mipaka, lakini fahamu haina mipaka. Mawazo ya Mungu hakika ni fahamu yake isiyo na mipaka (chenye tunaita kujua mambo yote).

Kulikuwa na nyakati katika biblia wakati Mungu alijidhihirisha kimwili ili aonekane na wanadamu katika mfano ambao wangeweza kuulewa bila hatari yoyote kwao. Kwa sababu Mungu alisema, "hakuna mwanadamu yeyote atakayeniona na kuishi" (Kutoka 33:20), alichagua wakati fulani kujidhihirisha katika mfano wa mwanadamu. Matukio hayo yanaitwa kuonekana kwa Mungu (Mwanzo 12:7-9; 18:1-33; 32:22-30). Kila mwenakano wa Mungu Mungu huchukua mfano wa mwanadamu ili kuonyesha mfano wa ubadilisho wake, mahali Mungu alichukua mfano wa mwanadamu kuishi kati kati yetu kama Imanueli, "Mungu pamoja nasi" (Mathayo 1:23).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je Mungu ana mwili halisi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries