settings icon
share icon
Swali

Inamaanisha nini 'kutwaa mwili'? Ni namna gani ambayo Yesu ambeye ni Mungu anatwaa mwili?

Jibu


Neno kitenzi la Kilatini kutwaa lilimaanisha "kuwa na mwili." wakati tunaposema kuwa Yesu Kristo ni Mungu "ana mwili," tunamaanisha kwamba Mwana wa Mungu aliutwaa nyama, umbo la mwili (Yohana 1:14). Ingawa, wakati hili lilitendeka ndani mwa tumbo ya Mariamu, mama wa dunia wa yesu, hakukoma kuwa Mungu. Ingawa Yesu alikuwa mwanadamu kamili (Waebrania 2:17), alibaki na hali yake kama Mungu (Yohana 1:1, 14). Yesu anawezaje kuwa mwanadamu pia Mungu kwa wakati mmoja ni mojawapo siri katika Ukristor walakini haijalishi hilo sio jaribio la Imani sahihi (1 Yohana 4:2; 2 Yohana 1:7). Yesu ana hali mbili kuu, Uungu na uanadamu. "Mnapaswa kuniamini ninaposema kwamba mimi niko ndani ya Baba naye Baba yuko ndani yangu. Ama sivyo, aminini kwa sababu ya mambo ninayofanya" (Yohana 14:11).

Biblia kwa wazi inafundisha uungu wa Kristo kwa kuwasilisha kama mtimizaji wa unabii Agano la Kale (Isaya 7:14; Zaburi 2:7), kuwepo kwake milele (Yohana 1:1-3; Yohana 8:58), kuzaliwa kwake kwa muujiza (Luka 1:26-31), Miujiza yake (Mathayo 9:24-25), uwezo Wake wa kusamehe dhambi (Mathayo 9:6), kukubali kwake sujudu zote (Mathayo 14:33), uwezo wake wa tabiri yatakoyo tokea (Mathayo 24:1-2), na kufufuka kwake kutoka wafu (Luka 24:36-39). Mwandishi wa Waebrania anatuambia kuwa Yesu ni malaika mkuu (Waebrania 1:4-5) na malaika wote wanapaswa kumsujudu (Waebrania 1:6).

Biblia pia inafunza juu ya kutwaa mwili-Yesu akawa mwanadamu kamili kwa kuutwaa mwili wa nyama. Yesu alitwaliwa mimba na akazaliwa (Luka 2:7), alikuwa na usoefu wa kukua (Luka 2:40), akawa na mahitaji ya kimwili (Yohana 19:28) na hysia za kibinadamu (Mathayo 26:38), alijifunza (Luka 2:52), alikufa kifo cha kawaida (Luka 23:46), na akafufuliwa na mwili wa kawaida (Luka 24:39), Yesu alikuwa mwanadamu kila njia ijapokuwa dhambi; aliishi maisha yasiyo na dhambi (Waebrania 4:15).

Wakati Kristo aliutwaa mwili wa binadamu, asili yake haikubadilika, lakini nafasi yake ilibidalika. Yesu katika hali yake asili ya Mungu kwa njia ya roho, alinyenyekea kwa kuweka kando utukufu wake na manufaa (Wafilipi 2:6-8). Mungu hatakoma kuwa Mungu kwa sababu yeye habadiliki (Waebrania 13:8) na asiye na miwsho (Ufunuo 1:8). Ikiwa Yesu alikoma kuwa Mungu kamili hata nukta moja, maisha yote yangeangamia (ona Matendo 17:28). fundisho la kutwaa mwili lasema kuwa Yesu, huku akibaki kuwa Mungu kamili, alikuwa mwanadamu kamili.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Inamaanisha nini 'kutwaa mwili'? Ni namna gani ambayo Yesu ambeye ni Mungu anatwaa mwili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries