settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu aliruhusu Shetani na mapepo kutenda dhambi?

Jibu


Na wote wawili malaika na wanadamu, Mungu alichagua kuwasilisha uchaguzi. Wakati Biblia haitoi maelezo mengi kuhusu uasi wa Shetani na malaika walioanguka, inaonekana kwamba Shetani pengine mkubwa wa malaika wote (Ezekieli 28:12-18 )-katika kiburi aliamua kuasi dhidi ya Mungu ili kutafuta kuwa mungu wake mwenyewe. Shetani (Ibilisi) hakutaka kuabudu au kumtii Mungu; alitaka kuwa Mungu (Isaya 14:12-14). Ufunuo 12:4 inaeleweka kuwa maelezo ya kimfano ya thuluthi moja ya malaika kuchagua kufuata shetani katika maasi yake, kuwa malaika walioanguka - mapepo.

Tofauti na binadamu, hata hivyo, uchaguzi malaika waliamuwa na kumfuata Shetani au kubaki waaminifu kwa Mungu ni uchaguzi wa milele. Biblia haitoi nafasi kwa malaika walioanguka ya kutubu na kusamehewa. Wala Biblia haionyeshi kwamba kuna uwezekana zaidi wa malaika kutenda dhambi. Malaika ambao hubaki waaminifu kwa Mungu wameelezwa kuwa "malaika wateule" (1 Timotheo 5:21). Shetani na malaika walioanguka walimjua Mungu katika utukufu wake wote. Wao kuasi, licha yao kujua kuhusu Mungu, ulikuwa uovu mkubwa. Matokeo yake, Mungu hawapi Shetani na malaika wengine walioanguka nafasi ya kutubu. Zaidi ya hayo, Biblia haitupi sababu kuwa wengeamini na kutubu hata kama Mungu angewapa nafasi (1 Petro 5:8). Mungu aliwapa Shetani na malaika uchaguzi huo aliowapa Adamu na Hawa, wa kumtii au kuasi. Malaika walikuwa na uhuru wa uchaguzi wa kufanya; Mungu hakuwalazimisha kwa nguvu au kuhimiza malaika yeyote kutenda dhambi. Shetani na malaika walioanguka walitenda dhambini kwa hiari yao wenyewe na kwa hiyo wanastahili hasira ya Mungu wa milele katika ziwa la moto.

Kwa nini Mungu alimpa malaika uchaguzi huu, wakati Yeye alijua matokeo yake itakuwa namna? Mungu alijua kwamba thuluthi moja ya Malaika wataasi na kwa hiyo kulaaniwa kwa moto wa milele. Pia Mungu alijua kwamba Shetani atazidisha uasi wake zaidi na kumjaribu binadamu katika dhambi. Kwa hivyo, ni kwa nini Mungu alirumhusu? Biblia haitupi jibu kamili kwa swali hili. Hilo linaweza kuulizwa kwa kila hatua yoyote ya maovu. Kwa nini Mungu aliruhusu? Hatimaye, inakuja kwa utawala wa Mungu juu ya uumbaji wake. Mwandishi wa Zaburi anatuambia, "Kama kwa Mungu, njia yake ni kamilifu" (Zaburi 18:30). Kama njia za Mungu ni "kamili," basi tunaweza kuamini kwamba lolote afanyalo - na chochote Yeye anaruhusu - ni kamilifu pia. Hivyo mpango kamili kutoka kwa Mungu wetu mkamilifu ulikuwa wa kuruhusu dhambi. Akili zetu si mawazo ya Mungu, wala ni njia zetu njia zake, kama Anavyotukumbusha katika Isaya 55:8-9.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu aliruhusu Shetani na mapepo kutenda dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries