settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini kuna nyakati ambapo Mungu huonekana kuwa kimya/hayupo katika maisha ya muumini?

Jibu


Katika kujibu swali hili, mtu anakumbushwa kuhusu Eliya na kutoroka kwake kutoka kwa Yezebeli. Eliya alikuwa mtu wa Mungu ambaye Mungu alimtumia kufanya mambo makuu. Hata hivyo, aliposikia kwamba Yezebeli alikuwa ametishia maisha yake, alitoroka (1 Wafalme 19). Eliya alisali kwa BWANA na kwa kweli alilalamika kuhusu jinsi alivokuwa akitendewa: “Akajibu, nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote. Waisraeli wamelikataa Agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi, mimi peke yangu, niliyebaki, nao sasa wananitafuta ili waniangamize” (1 Wafalme 19:10). Jibu la BWANA kwa Eliya ni la kushangaza: “Bwana akasema, “Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele za Bwana, kwa kuwa Bwana yu karibu kupita hapo.” Kisha upepo mwingi na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele za Bwana, lakini Bwana hakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la nchi, lakini Bwana hakuwamo kwenye lile tetemeko. Baada ya tetemeko la nchi ukaja moto, lakini Bwana hakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunongʼona” (1 Wafalme 19:11-12).

Tunaona katika kifungu hiki cha Maandiko kwamba kile Eliya alichofikiri hakikuwa kweli. Eliya alifikiri Mungu alikuwa kimya na kwamba yeye peke yake ndiye aliyebaki. Mungu hakuwa “kimya” tu bali alikuwa na jeshi lililongoja katika mbawa ili Eliya hakuwa peke yake: “Hata sasa nimeweka akiba watu elfu saba katika Israeli, wote ambao hawajampigia Baali magoti, na wote ambao midomo yao haijambusu” (1 Wafalme 19:18).

Katika mwenendo wetu kama waumini waliozaliwa mara ya pili, inaweza kuonekana kuwa Mungu amekimya, lakini kamwe Mungu hawezi kimya. Chenye huonekana kama kimya na kutofanya kazi kwetu ni Mungu anaruhusu tupate fursa ya kuisikia “sauti ya utulivu ya kunongʼona” na kuona maandalizi ambayo ametuandalia kwa imani. Mungu anahusika katika kila eneo la maisha ya muumini-nywele kichwani mwetu zimehesabika (Marko 10:30; Luka 12:7). Hata hivyo, kuna nyakati ambazo tunapaswa kutembea kwa utiifu kwa nuru ambayo Mungu ametupa kabla hajatuangazia zaidi njia yetu, kwa sababu katika enzi hii ya neema Mungu anazungumza nasi kupitia kwa Neno Lake.

“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu,” asema Bwana. “Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia, ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Kama vile mvua na theluji ishukavyo kutoka mbinguni, nayo hairudi tena huko bila kunywesha dunia na kuichipusha na kuistawisha, hivyo hutoa mbegu kwa mpanzi na mkate kwa mlaji, ndivyo lilivyo neno langu lile litokalo kinywani mwangu: Halitanirudia tupu, bali litatimiliza lile nililokusudia na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma” (Isaya 55:8-11).

Kwa hivyo, Mungu anapoonekana kuwa kimya kwetu kama waumini waliozaliwa mara ya pili, inaweza maanisha kwamba tumeacha kusikiza sauti Yake, tumeruhusu mahangaiko ya ulimwengu kuziba masikio yetu ya kiroho au tumetekeleza Neno Lake. Mungu hasungumzi kwetu leo hii kwa ishara, miujiza, moto au upepo, Roho wake huzungumza kwetu kupitia Neno na katika Neno hilo tuko na “maneno ya uzima.”

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini kuna nyakati ambapo Mungu huonekana kuwa kimya/hayupo katika maisha ya muumini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries