settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Mungu anawaruhusu wat kumdhihaki?

Jibu


Kila siku, kila pande ya ulimwengu, kunao watu ambao humdhiaki Mungu. Wengi huvuka mipaka na kumkufuru, kejeli na kutingiza ngumi yao kwa Muumba. Kiwango cha dhihaka ni cha kuvunja moyo na ujaziri wao ni wa kuangaliwa. Mungu anayaona mambo yote, na hakika anaweza kufanya kitu kuyahusu. Ni kwa nini anayaruhusu kuendelea?

Mungu aliumba mwanadamu na nia huru. Ufunuo 4:11 yasoma, "Wastahili ee Bwana na Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na nguvu. Maana wewe uliumba vitu vyote, na kwa matakwa yako viliumbwa na vipo." Mwenyezi Mungu alituumba kwa utukufu wake na mapenzi, na ni furaha gani itakayokuwepo kuliko ile ya kupenda na mtu kwa hiari na furaha bila kulazimizwa kupenda? Mungu hakuumba viumbe bila akili ambavyo vitafuata amri zake. Alitaka watoto sawia na vile wazazi wanatamani watoto, sio kama watumwa bali watu wanaofikiria, na walio kamilika katika udhaifu wao na nafsi zao. Mungu alitaka kuwa na ushirika nasi, uhusiano nasi. Ulio wa kweli, upendo halisi ni wa hiari.

Na kwa sababu Mungu aliumba mwanadamu njia hii-ingawa hakulazimika kufanya hivyo, lakini alichagua kufanya-tuko na hiari huru kumuasi, mkufuru na naam ahata kumdhihaki. Lakini tumeonywa katika Wagalatia 6:7 kwamba Mungu hafanyiwi mzaha. Ukufuru na mzaha ni vya muda. Kunayo siku ya majuto, na mwishoye mtu atavuna alichopanda.

Tuko na uwezo wa kuchagua mema au mabaya, lili sahihi au asi. Mungu pia alitupa suluhisho, njia ya kuondokana na dhambi na kwa uzima wa milele. Yesu Kristo ametoa njia ya kurejesha uhusiano wa upendo na Mungu, kupitia dhabihu yake msalabani.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Mungu anawaruhusu wat kumdhihaki?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries