settings icon
share icon
Swali

Ni namna gani Mungu ni kimbilio letu?

Jibu


Neno kimbilio linakufanya ufikirie nini? Pengine jengo ambalo limefungwa na kufuli halingiliki, pengine boma lililo na kuta pana, au pengine kitu rahisi kama mwavuli unakukinga tokana na mvua. Taswira yoyote ikujiayo akilini, inaweza kubalika kuwa kimbilio ni mahali salama. Wakati Biblia inaelezea Mungu kama kimbilio letu, inasema kuwa Mungu ni mahli petu salama wakati tunahitaji kinga kutokana na kitu.

Kumjua Mungu kuwa kimbilio letu hutwezesha kumwamini sana kwa hiari. Hatupaswi kuogopa hali au watu ambao hutishia maisha yetu, iwe ni ya kimwili au kiroho. Hakuna hali tutakayo kumbana nayo ambay haiwezi dhibitiwa na Mungu wetu, kwa hivyo mahali pazuri pa kuwa kila mar ani kuwa pamoja naye. "Jina la Mwenyezi-Mungu ni mnara imara; mwadilifu huukimbilia akawa salama" (Methali 18:10).

Swali ambalo hujibuka ni "nitamfanyaje Mungu kuwa kimbilio langu?" ni rahisi kuwa na taswira ya kimbilio halisi linalotukinga tokana na hatari fulani, lakini tunawezaje kumfanya Mungu-ambaye hatuwezi mwona-kuwa kimbilio letu?

Daudi ni mfano mkuu wa mtu ambaye alimjua Mungu kama kimbilio lake. Katika nyakati tofauti katika maisha yake, Daudi alikuwa mkimbizi kutoka kwa watu ambao walitaka kumua, lakini mara nyingi alipata usalama wake kwa Mungu. "Wokovu na fahari yangu vyatoka kwa Mungu; mwamba wangu mkuu na kimbilio langu ni Mungu. Enyi watu, mtumainieni Mungu daima; mfungulieni Bwana yaliyo moyoni mwenu. Mungu ndiye kimbilio la usalama wetu" (Zaburi 62:7-8). Njai rahisi ya kumfanya Mungu kimbilio na rahisi, kumuuliza Yeye awe kimbilio. Daudi alisema, "mfunguliw Mungu moyo wako"; Hilo ndilo Daudi alifanya wakati wote. Alimfungulia Mungu moyo wake wote kwa kile kilichoendelea katika maisha yake na akamsihi Mungu aingilie kati kwa niapa yake. Wakati tunamgeukia kwa msaada au ulinzi, tunaanza kumjua kama kimbilio letu.

Kwa ulinganisho kwa Imani ya Daudi, viongozi wa Israeli katika siku za Isaya walijaribu kupata usalama kwa vitu vingine mbali na Mungu. Katika Isaya 28:15 Bwana anawakemea kwa sababu "mmefanya uongo kuwa tegemeo lenu, na udanganyifu kuwa kinga yenu." Na Mungu bado anawapa kinga bora: "Basi, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu: "Tazama! Naweka mjini Siyoni jiwe la msingi, jiwe ambalo limethibitika. Jiwe la pembeni, la thamani, jiwe ambalo ni la msingi thabiti; jiwe lililo na maandishi haya: 'Anayeamini hatatishika.' Nitatumia haki kama kipimo changu, nitatumia uadilifu kupimia." Mvua ya mawe itaufagilia mbali uongo mnaoutegemea, na mafuriko yataharibu kinga yenu. Hapo mkataba wenu na kifo utabatilishwa, na mapatano yenu na Kuzimu yatafutwa. Janga lile kuu litakapokuja litawaangusheni chini (Isaya 28:16-18). tunaweza jaribiwa kutafuta usalama kwa vitu vingine mbali na Mungu, lakini vitu kama hivyo vitatoa usalama hisia potovu za kinga. Mungu ndiye kimbilio la kweli tutakalo pata.

Mungu ndiye kimbilio letu. Ingawa, hiyo haimaanishi kamwe hawezi kutuelekeza kwa hali ngumu au hali hatari. Yesu aliwaongoza wanafunzi wake kwa mashua, akijua kwamba mawimbi makali yangevuma; wanafunzi waliogopa, lakini Yesu, kimbilio lao alituliza mawimbi (Mathayo 8:23-27). Wakati tuko katika mapenzi ya Mungu, tunaweza kukumbana na hali ngumu kwa ujasiri, kwa sababu Mungu yuko pamoja nasi.

Nyakati sisizohesabika, Mungu aliwaongoza Waisraeli kwa vita dhidi ya kikozi kilichokuwa dhabiti kuwaliko, na wakati walimtumainia Mungu na kumtii, kila wakati walikuwa washindi (ona Yoshua mlango wa 6 na 8 kwa baadhi ya mifano). Yesu alituambia, "Nimewaambieni mambo haya ili mpate kuwa na amani katika kuungana nami. Ulimwenguni mtapata masumbuko; lakini jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu (Yohana 16:33).

Haijalishi hali yetu, mahali salama pa kuwa kila mara ni katika katikati mwa mapenzi ya Mungu. Meahidi kuwa kimbilio letu: "Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?'" (Waebrania 13:5-6).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni namna gani Mungu ni kimbilio letu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries