settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Mungu Hujieleza kwa njia ya wingi katika Mwanzo 1:26 na 3:22?

Jibu


Mwanzo 1:26 yasema, "Kisha Mungu akasema, "Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.'" Mwanzo 3:22 yasema, "Kisha Mwenyezi-Mungu akasema, "Sasa, binadamu amekuwa kama mmoja wetu." Kunazo maandiko mengine katika Agano la Kale ambazo kwayo Mungu hujirejelea akitumia wingi. Pia ni muhimu kukumba kwamba Elohimu, mojawapo ya majina ya Mungu katika Agano la Kale (limetumika zaidi ya 2,500), liko katika wingi.

Watu wengine wametumia aya hizi kukisia kwamba kunayo zaidi ya Mungu mmoja. Ingawa, tunaweza kutupilia mbali Imani ya kuwepo kwa miungu wengi, kwa sababu hiyo itahitilafiana andiko sisohesabika zinazotuambia kuwa Mungu ni mmoja na kwamba kuna Mungu mmoja. Mara katika Isaya 45 pekee Mungu anasema, "Mimi ni Mwenyezi-Mungu, wala hakuna mwingine; hakuna Mungu mwingine ila mimi" (aya ya 5,6,18).

Uwezekano wa fafanuzi la pili ambalo Mungu Hujirejelea Yeye mwenyewe katika wingi ni kwamba Mungu alikuwa anajumulisha malaika katika maelezo yake. Kwa kusema "sisi" na "yetu" Mungu alikuwa anasungumzia kuhusu viumbe vyote vya mbinguni, Yeye akiwemo. Ingawa, hamna mahali Biblia inasema kuwa malaika wana "mfano" au "sura" wa Mungu "ona Mwanzo 1:26). Elezo limetolewa la wanadamu pekee

Jinzi Biblia na hasa Agano Jipya humwakilisha Mungu katika Utatu (nafsi tatu lakini Mungu mmoja), Mwanzo 1:26 na 3:22 zinaweza tu kuonyesha sungumzo katika Utatu. Mungu Baba ako na "mawaziliano" na Mungu Mwana na Roho Mtakatifu. Agano la Kale linatupa fununu juu ya wingi wa Mungu, na Agano Jipya linaweka wazi wingu huu katika somo la Utatu. Ni wazi, hamna njia tunaweza elewa kikamilifu jinsi hii inafanya kazi, lakini Mungu ametupa ujumbe wa kutosha wa kujua kwamba anaishi katika nafsi tatu-Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Mungu Hujieleza kwa njia ya wingi katika Mwanzo 1:26 na 3:22?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries