settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kuwa Utatu ni Mungu katika nafsi tatu?

Jibu


Wakati tunasungumzia kuhusu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kuwa "nafsi," hatumaanishi kuwa wao ni binadamu au wanafanana na mwanadamu kwa njia yoyote. Katika lugha yetu ya kila siku, ijapokuwa hivyo ndivyo neno nafsi kila mara linatumika, hivyo inaeleweka kuwa baadhi utata waisunguka rejeleo la "nafsi" za Utatu.

Wakati tunasungumzia kuhusu Mungu, tunatumia neno nafsi ili kuonyesha Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kila mmoja wao ana utu au sifa. Hiyo inamaanisha kuwa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wote wana akili, hisia, na hiari. Kiumbe chochote kilicho na akili, hisia, na hiari kinaweza chukuliwa kuwa mtu, kwa hivyo wanadamu ni nafsi, lakini na malaika pia na viumbe vya kiungu. Tafsiri ya mtu haiwezi jumulisha kuwepo kwa sababu moja fupi, kwamba wanadamu hawakomi kuwa kuwa watu hata baada ya kufa. Maiti ya mtu aliyekufa yanabaki nyuma kuoza, lakini nafsi halisi-ule utu-unaendelea kuishi mbinguni au jahanamu.

Tunaposungumzia juu ya Mungu kuwa anaishi katika nafsi tatu, tunamaanisha kwamba kuwepo kwa Mungu kuna jumulisha sehemu tatu, akili, hisia, na hiari. Kila nafsi ya Utatu ina jukumu maalumu katika uumbaji na katika wokovu wa mwanadamu. Roho Mtakatifu ni wa ajabu na sio Baba wala Mwana (Yeye hutoka kwa Baba na Mwana, Yohana 15:26). Baba na Mwana pia wao ni wa kipekee (wakati Yesu aliomba kwa Baba, hakuwa anaomba kwa nafsi yake, Luka 15:34). Kila mmoja wao ni Mungu, walakini "nafsi" tofauti. Tukitumia neno mtu ni njia moja pekee lugha ya mwanadamu inaweza kuelezea dhana hii.

Hizi nafsi tatu zote za Utatu ni moja, ni Mungu aliyeunganika kikamilifu. Wanashiriki hali moja na kiini kimoja, na wote ni Mungu mmoja, lakini kila nafsi ya Utatu ni tofauti na ya kipekee. Dhana kwamba Mungu anaishi katika nafsi tatu ni ya muhimu kwa sababu nyingi. Kwa mfano, Mungu ni upendo (1Yohana 4:8). Lakini katika milele iliyopita kabla Mungu aumbe kitu chochote, je! Hangekuwa upendo? Hiyo ni kusema kwamba, upendo unaweza kuwepo mahali hamna mtu anaweza kupendwa? Kwa sababu Mungu anaishi katika hali tatu sawia, nafsi sawia milele, upendo upo pia. Upendo wa milele umedhihirishwa milele katika hizo nafsi tatu za Kiungu. Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kila mara wanapendana, na kwa hivyo upendo u milele.

Pindi tutaweka kando dhana kuwa "nafsi" inaweza kuwa "mwanadamu," tunaweza kuelewa kwa urahisi jinsi Mungu anaweza semeka kuwa anaishi katika "nafsi" tatu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kuwa Utatu ni Mungu katika nafsi tatu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries