settings icon
share icon
Swali

je! Mungu husahau hasa dhambi zetu? Ni namna gani Mungu anayejua mambo yote anaweza kusaau kitu chochote?

Jibu


Kuna vifungu vingi katika Biblia ambavyo vinaonyesha kuwa Mungu husamee na kusaau dhambi zetu. Isaya 43:25 inasema, "Walakini mimi ndimi niliyefuta makosa yenu kwa heshima yangu, ndimi niyafutaye makosa kwa ajili yangu mwenyewe, na wala sitazikumbuka dhambi zenu." Waebrania 10 inaelezea jinsi dhabihu ya Yesu msalabani kwa ajili ya dhambi zetu ilikuwa ya kwanza na ya mwisho. Kinyume na mifumo ya dhabihu ya Agano la Kale, ambapo dhabihu zilitolewa kila mara kwa ajili ya dhambi, Yesu alilipia dhambi mara moja. Dhamana yake ilikuwa kamilifu. Waebrania 10:14-18 inasema, "Basi, kwa tambiko yake moja, amewafanya kuwa wakamilifu milele wote wale wanaotakaswa dhambi zao. Naye Roho Mtakatifu anatupa ushahidi wake. Kwanza anasema: "Hili ndilo agano nitakalofanya nao, siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika akilini mwao." Kisha akaongeza kusema: "Sitakumbuka tena dhambi zao, wala vitendo vyao vya uhalifu." Basi, dhambi zikisha ondolewa, hakutakuwa na haja tena ya kutoa tambiko za kuondoa dhambi."

Andiko hili linaiweka wazi kwamba Mungu hakumbuki makosa yetu. Ijapokuwa, Mungu "kutokumbuka" sio kile tunachofikiria kuwa kusaau. Mungu anajua mambo yote. Anajua kila kitu na hakuna anaweza kusaau. Ingawa, anaweza amua kutokumbuka kitu. Katika mahusiano yetu ya kiwanadamu, tunaweza kuamua kukumbuka makosa ambayo mtu ametukosea, au tunaweza amua kusaau. Kumsamehe mtu, lazima tuweke kumbukumbu mbaya mbali na mawazo yetu. Hatuisaau dhambi haswa, ni sio kwamba hatuwezi kumbuka kosa, lakini tunaamua kulisaau. Msamaha unatusaidia tusidumu katika masaibu yetu ya kale.

Badala ya kutendea kadri ya dhambi zetu zinavyostahili, Mungu huziondoa dhambi zetu kutoka kwetu "Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi"- umbali wa kadri (Zaburi 103:12). Fikiria ukizulu ulimwenguni. Lini mtu anaacha kwenda mashariki na kwenda magharibi? Ni vigumu kusema. Wakati tumeokoka, dhambi zetu zinasamehewa kabisa. Hayo ndio mwandishi wa Waebrania nasungumzia- Yesu alitoa dhabihu ya mara moja na ambayo inaondoa dhambi zetu kabisa. Katika Kristo tumehesabiwa haki mbele za Mungu. Warumi 8:1 inatuambia kwamba hamna hukumu tena kwa wale walio ndani ya Kristo. Badala yake, anatuchukulia kuwa wenye haki. Wakorintho wa Pili 5:21 yasema, "Mungu alimfanya ahusike na dhambi kwa ajili yetu, ili sisi kwa kuungana naye, tupate kuushiriki uadilifu wake Mungu." Katika namna hii, Mungu "husahau" dhambi zetu.

Hata kama tu Wakristo, bado twatenda dhambi, lakini tunajua kwamba Mungu ni mwaminifu atatusamehe (1Yohana 1:9). Mungu hutakasa, na anasonga mbele. Hatuhesabii dhambi zetu. Badala yake anatuweka huru kutoka utumwani mwa dhambi na kutuweka huru ili tuwe na maisha mapya. Kujua msamaha kamili wa Mungu katika Kristo, tunaweza ungana na mfalme Hezekia kwa kumtukuza mkombozi wetu: "umezitupa dhambi zangu nyuma yako" (Isaya 38:17). Kama Paulo tunaweza kusahau yaliyopita na "kufanya bidii kuyazingatia yale yaliyo mbele" (Wafilipi 3:13).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

je! Mungu husahau hasa dhambi zetu? Ni namna gani Mungu anayejua mambo yote anaweza kusaau kitu chochote?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries