settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kwamba Mungu hupeana?

Jibu


Kuna mistari zaidi ya 169 katika Biblia ambayo inaelezea njia ambazo Mungu hutupa. Wafilipi 4:19 inasema kwa urahisi: "Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake,katika utukufu ,ndani ya Kristo Yesu." Ingawa watafutao mafanikio wanaeza kuwa wanatafuta pesa au mali kutokea kimaajabu, tunapaswa kuchunguza kenye Mungu anahitaji ili kutupea sisi.

Kama mzazi yeyote mzuri, Mungu hawezi kutupa kile anachojua kitatuthuru. Lengo lake ni kutusaidia kuendeleza Ukristo ili tuweze kuwa chumvi na mwanga ulimwenguni (Mathayo 5: 13-14). Mungu hatutaki kumwona kama mtoaji wa mbinguni wa mali tu. Kupata vitu sio lengo la msingi la maisha haya (Luka 12:15).

Mungu hutafautisha kati ya mahitaji yetu na upungufu wetu kwa sababu anajua kwamba mahali hazina yetu iko moyo wetu pia uko apo (Mathayo 6:21). Anataka tujue kwamba ulimwengu huu sio nyumba kwetu na kwamba sehemu ya kile tunachohitaji kinastahili kulenga mtazamo wetu katika uzima wa milele wakati bado tunaishi humu.

Mungu anahusika na kila sehemu ya utu wetu: nafsi, roho, na mwili. Kama sifa za tabia Yake hazipungui, hivyo njia ambazo Mungu hutupa sisi ni zaidi ya chochote tunaweza kuomba au kufikiria (Waefeso 3:20). Tunaweza amini wema wake, mwongozo, na huduma ya uchungaji hufanya zaidi kwa sisi kuliko tunavyoweza kufikia sisi wenyewe. Mungu hutoa njia kwa sisi kuendeleza uhusiano wa karibu, wa kuzungumza,uhusiano wa utiifu na Yeye ili tuweze kujiongoza na wengine katika "Zaburi 23" ubora wa maisha. Wale ambao mchungaji wao ni Bwana anaweza kusema, "Sikosi chochote" (Zaburi 23: 1).

Katika Sala ya Bwana, Yesu anawafundisha wanafunzi Wake kuomba, na utegemea wetu juu ya Mungu huthibitishwa kila wakati tunapoomba, "Tupe leo mkate wetu wa kila siku" (Mathayo 6:11). Katika Mathayo 6: 25-34, Yesu anawaambia wanafunzi wake wasikue na wasiwasi kuhusu chakula au mavazi. Baba anajua mahitaji yetu. Anahitaji uhusiano wa agano na sisi, na ambao unahusisha kumtumaini ili kukidhi mahitaji yetu ya kila siku na kutafuta kwanza ufalme wake na uadilifu (Mathayo 6:33).

Zaburi ya 84:11 inasema, "Hakuna kitu kizuri ambacho anazuia kutoka kwa wale wanaotembea kwa uangalifu." Mstari huu unakukumbusha kwamba kuna sehemu tunayocheza katika utoaji wa Mungu unaojaza mafanikio katika maisha yetu. Lazima tutembee kwa uangalifu.

Yakobo 4: 3 ni jibu kwa maswali yetu kuhusu kwa nini maombi wakati mwingine huenda bila majibu: "Unapoomba, hupokei, kwa sababu unaomba kwa nia mbaya, ili uweze kutumia kile unachopata kwenye raha zako." Mungu anaona moyo, na maombi yetu, nia zetu ni muhimu kwake.

Vifungu vingi kuhusu utoaji wa Mungu vinahusiana na haja yetu ya chakula na mavazi na mahitaji ya kila siku ya kimwili. Vingine hutaja mahitaji ya nafsi yetu na roho, mtu wetu wa ndani. Anatupa kwa amani (Yohana 14:27), faraja (2 Wakorintho 1: 4), na "nguvu, upendo na kujidhibiti" (2 Timotheo 1: 7). Kwa kweli, Yeye "... aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni,katika ulimwengu wa roho,ndani yake Kristo" (Waefeso 1: 3). Katika hali yoyote ya kimwili tunayojikuta, tunaweza kuwa na furaha katika Bwana (Wafilipi 4:12).

Vifungu kama Wagalatia 1:15 na Yeremia 1: 5 inatuhakikishia kwamba upendo na uongozi wa Mungu ulianza hata kabla ya kuzaliwa. Ni zawadi gani kujua kwamba Mungu amehusika katika maisha yetu tangu mwanzo! Upendo wake kwa ajili yetu umehusishwa na mahitaji yake kwa faida yetu nzuri zaidi. Kwa kweli Yeye ni Yehova-Jire, Bwana-Anayetoa.

Utoaji wa Mungu unaendelea na uhusiano wake unaoendelea na viumbe wake wote, ambao unamtegemea sana (Zaburi 104: 21). Mara nyingi, tunachukulia kwa msaha mvua inayonyesha, jua linalojitokeza kila asubuhi, upepo unaofariji unaopiga, na maji makuu yanayotakasa pwani zetu na kuimarisha maisha katika bahari yetu kubwa. Lakini mambo haya yote yanathibitiwa na Mungu wetu mwenye upendo katika utoaji wake kwa ajili yetu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kwamba Mungu hupeana?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries