settings icon
share icon
Swali

Je! Mungu hukasirika?

Jibu


Itakuwa upumbavu kupuuza ujumbe katika Maandiko ambayo yanasungumzia kuhusu hasira ya Mungu. Naam, Mungu huwa na hamaki: kuna mifano mingi katika Biblia yah ii. Yeye, "aghadhibikaye kila siku" (Zaburi 11:7).

Ingawa hatuwezi linganisha hasira ya Mung una usoefu wetu wa kibinadamu wa hisia hiyo. Lazima tuangalie tena ndani ya maandiko. Waefeso 4:26-27 inatuambia kwamba unaweza kuhisi hasira bila kufanya dhambi. Vile Mungu hawezi tenda dhambi, tunajua kuwa hasira yake ni haki, mbali na hali yetu ya hasira ndani yetu. Vile Yakobo 1:20 inasema, "kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu."

Mktadha wa aya hii ya Mungu kuwa na hasira inaonyesha ni kwa nini yeye huwa na hasira. Mungu huwa na hasira wakati kuna uasi wa maadili yake. Mungu ni mwadilifu, mwenye haki, na mtakatifu na hakuna hata moja ya hizi sifa ziteweza kuridhiana (Kutoka 20:4-6; Isaya 42:8). Mungu alikasirishwa na taifa la Israeli na wafalme wake kila wakati walipogeuka na kutomtii yeye (mfano, 1 Wafalme 11:9-10; 2 Wafalme 17:18). Matendo maovu ya Wakanaani, kama vile dhabihu ya watoto na jinsia potovu, ziliamsha ghadhabu ya Mungu kiwango kwamba aliamrisha Waisraeli kuwaangamiza kabisa- kila mwanaume, mwanamke, mtoto, na wanyama-ili kuondoa uovu kutoka nchi (Kumbukumbu 7:1-6). Vile mzazi anaweza kasirishwa na kitu chochote kinaweza kukwaza watoto wake, na hivyo hasira ya Mungu inaelekezwa kwa kile ambacho kitawadhuru watu wake na uhusiano wao naye. "Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi'" (Ezekieli 33:11).

Katika Agano Jipya Yesu alishikwa na hamaki kwa walimu na viongozi wa dini wa siku hizo kwa kuitumia dini kwa manufaa yao wenyewe na kuwaweka watu utumwani (Yohana 2:13-16; Marko 3:4-5). Warumi 1:18 inatuambia kuwa hasira au ghadhabu ya Mungu huwajia wale ambao ni "uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu." Kwa hivyo Mungu hushikwa na hamaki kwa uovu ndani ya watu, na anapinga uovu huo kwa juhudi za kuwarejesha kutoka kwa dhambi, ili kwamba wapate maisha ya kweli na uhuru ndani yake. Hata katika hasira yake, motisha ya Mungu ni upendo kwa watu wake; kurejesha uhusiano ambao dhambi iliharibu.

Huku Mungu lazima alete haki na adhabu ya dhambi, wale ambao wamemkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi wao hawako tena chini ya ghadhabu ya Mungu kwa dhambi. Kwa nini? Kwa sababu Yesu alipitia kipimo kamili cha ghadhabu ya Mungu msalabani ndiposa tusiweze kuipitia. Hii ndio maana ya kuwa kifo cha Yesu kilikuwa "upatanisho," au uridhisho. "Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho" (Warumi 8:1-4).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mungu hukasirika?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries