settings icon
share icon
Swali

Mungu hujali kuhusu mambo madomadogo ambayo hutoke maishani mwetu?

Jibu


Naam Mungu hujali kuhusu mambo madogo madogo ambayo hutokea katika maisha yetu kwa sababu kila kitu huwa kidogo sana ikilinganishwa na Mungu! Luka 12:7 inasema, "Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi, bora ninyi kuliko mashomoro wengi." Mungu huchukua muda wake ili kujua ni nywele ngapi ziko kwa kichwa chetu- sasa huyo ndie Mungu wa maelezo ya kina!

Ndani ya maandiko yote tunaona kwamba Mungu yuna haja na maisha yetu sana kama watoto wake. Yeye hujali kwa kila hali ya maisha yetu, kwa sababu sisi ni viumbe wake tulioumbwa kwa mfano wake (angalia Mwanzo 1:27). Yeye anajali viumbe vyake vyote, ikiwa ni pamoja na mimea, wanyama, na masingara. Matayo 6:26 yasema, "Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?" Ikiwa Mungu hukimu mahitaji ya ndege wa angani, ambao hawakuumbwa kwa mfano wake, ambao hawana ihari ya kumchagua au kumkataa, ni jinsi gani atakidhi mahitaji yetu? Kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, tunaweza kumwani: "Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba" (Matayo 6:8).

Katika huduma ya Yesu duniani, tunaona kwamba Yesu alikuwa na haja sana na hali ya maisha ya watu. Yesu amekuwa na haj asana katika ubora na utele. Yesu alitumwa kuokoa waliopotea na kusiba mwanya kati ya mwanadamu na Mungu tangu kuanguka, lakini bado alichukua muda wake kukidhi mahitaji ya dharura ya watu ambao alikutana nao. Katika Matayo 14:18-21 tunaona taswira kamili ya huruma ya Yesus kwa umati uliokuwa na njaa. Maanguli moja kwa maisha ya wengi lakini yana maelezo ya kina, na bado tuna simulisi ya ajabu ya jinsi alivyotoa vyakula vilivyo toka mbinguni kwa watu zaidi ya 5,000 wakiwemo wanaume, wanawake, na watoto.

Watoto ni "vitu vidogo" na wanaweza kuingilia kati kwa vitu vya "maana." Kwa hakika, pindi tu watu waliwaleta Watoto wao kwa Yesu, wanfafunzi wake waliwakemea kwa dhana ya kuwarudisha. "Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao" (Marko 10:14). Yesu si mkubwa sana au kuwa na kazi kiwango hawezi kuwabariki Watoto.

Mungu kwa kweli anajali kuhusu mambo "madogo madogo" ambayo hutokea katika maisha yetu, kwa sababu anatujali. Ikilinganishwa naye na utukufu wake, maisha yetu yameundwa na hivyo vitu "vidogo vidogo." Zaburi 139:17-18 yasema, "Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa jumla yake! Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga; Niamkapo ningali pamoja nawe."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mungu hujali kuhusu mambo madomadogo ambayo hutoke maishani mwetu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries