settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kuwa Mungu hufanya mambo njia ya ajabu?

Jibu


Mungu hufanya mambo kwa njia ambayo mara nyingi huchukuliwa kuwa ya "ajabu"- hiyo ni kusema utaratibu wa Mungu kila mara huacha wat una mshangao. Ni kwa nini Mungu alimwambia Yoshua na wana wa Israeli wauzunguke mji wa Yeriko kwa juma moja (Yoshua 6:1-4)? Ni mazuri gani yangetokana na kwa kufungwa kwa Paulo na sila na kuchabwa bila sababu (Matendo 16:22-24)?

Mchakato ambao Mungu hutumia upatanishi wa uhuru wa mwanadamu na uenzi wa Mungu, muhtasari wa mwisho wa Mungu viko mbali na mawazo ya mwanadamu yaliyo na mwisho kuelewa. Biblia na shuhuda za Wakristo katika vizazi zimejaa na hadhiti ya jinsi Mungu aligueza juu chini hali baada ya hali, shida baada ya shida, maisha baada ya maisha-kila mara yeye hufanya katika njia ambayo haikutarajiwa, ya kushangaza, na isiyoelezeka.

Maisha ya Yusufu ni mfano mzuri wa Mungu kufanya kazi kwa njia ya maajabu (Mwanzo 37:150:26). Katika Mwanzo 50:20, Yusufu anasema haya kwa nduguze, "Nyinyi mlitaka kunitendea vibaya, lakini Mungu alikusudia mema ili watu wengi wapate kuwa hai kama mwonavyo leo." Katika kauli hiia Yusufu anatoa muhtasari wa matukio ya maisha yake, akianzia maovu ambayo nduguze walimtendea na akimalizia kwa kutambua kwake kwamba yote ilikuwa sehemu ya mpango wa Mungu wa kuokoa watu wake wa agano (Mwanzo 15:13:14).

Kulikuwa na njaa Kanaani ambapo uzao wa Ibrahimu, Wayahudi walikuwa eka makao (Mwanzo 43:1), hivyo Yusufu akawaleta wote kutoka Kanaani hadi Misri (Mwanzo 46:26-27). Yusufu alikuwa na uwezo wa kuwalisha wote kwa sababu alikuwa amekwisha kuwa gavana wa Mistri na yeye ndiye alikuwa anasimamia ununuaji na uuzaji wa chakula (Mwanzo 42:6). Ni kwa nini Yusufu alikuwa Mistri? Nduguze Yusufu walikuwa wamemuuza utumwani takribani miaka ishirini iliyopita na sasa walikuwa wakimtegemea kwa chakula chao (Mwanzo 37:28). Kinaya hii ni sehemu ndogo tu ya kile kilitokea kwa maisha ya Yusufu; harakati ya Mungu ya sadifa ni dhahiri katika historia ya Yusufu. Yusufu asingekuwa gavana wa Mistri na kuwaamisha jamaa zake huko, hakungekuwa na historia ya Musa, na kutoka kwa Waisraeli Misri miaka mia nne baadaye (Kutoka 6:1-8).

Ikiwa Yusufu angekuwa na chaguo la kuwakubali au kuwakana ndugu zake ambao walimuuza, ni sahii kudhani kuwa Yusufu angesema "la." Ikiwa Yusufu angepewa chaguo la kufungwa au kutofungwa kwa makosa ya kutuhumiwa (Mwanzo 39:1-20), tena pengine angesema "la." Ni ako tayari kuchagua kudhihakiwa kama huku? Lakini ilikuwa ni Misri ambapo Yusufu aliweza kuokoa familia yake, na ilikuwa ni gerezani mlango wa hikulu ulifunguka.

Mungu "alitangaza mambo ya mwisho tangu mwanzo" (Isaya 46:10-11), na tunaweza kuwa na uhakikisho kuwa kila tukio katika maisha ya kila muumini hutumikia mpango wa Mungu (Isaya 14:24; Warumi 8:28). Kwa mawazo yetu, njia ambazo Mungu uhunganisha matukio ndani na nje ya maisha yetu inaweza onekana kutokuwa ya mantiki na inapita fahamu zetu. Ingawa, twatembea kwa Imani na sio kwa kuona (2 Wakorintho 5:7). Wakristo wanajua kuwa mawazo ya Mungu yanapita mawazo yetu, na njia za Mungu zi juu ya zetu, "mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi" (Isaya 55:8-9).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kuwa Mungu hufanya mambo njia ya ajabu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries