settings icon
share icon
Swali

Je! Mungu huchukia? Ikiwa Mungu ni upendo, anawezaje kuchukia?

Jibu


Inaweza onekana kuwa mkanganyo kuwa Mungu ambaye ni upendo anaweza kuchukia. Huku hayo ndiyo biblia inaseama kuwa kweli: Mungu ni upendo (1Yohana 4:8), na Mungu huchukia (Hosea 9:15). Upendo ni uhasili wa Mungu, kila mara yeye hutenda kile kilicho bora kwa manufaa yaw engine-na anachukua kile kilicho kinyume na asili yake-anachukia kile kilicho kinyume na upendo.

Mtu yeyote asishangae wakipata kuwa Mungu anachukia baadhi ya vitu. Ulituumba na uwezo wa kupenda na kuchukia, na tunakubaliana kuwa chuki mara nyingi imehasabiwa haki- kawaida tunachukia vitu ambavyo uharibu kile tunapenda. Hii ni sehemu yetu ya kuumbwa katika mfano wa Mungu. Ukweli kuwa tumetiwa doha na dhambi inamaanisha kuwa upendo wetu na chuki yet umara nyingine huwa kimakosa, walakini kuwepo kwa hali ya dhambi haidunishi uwezo wetu wa kiungu wa kupenda and kuchukia. Haikanganyi kuwa mwanadamu ana uwezo wa kupenda na kuchukia, na wala si mkanganyo kwa Mungu kuweza kupenda na kuchukia.

Wakati Biblia inazungmzia kuhusu chuki ya Mungu, lengo kuu la chuki yake ni dhambi na uovu. Kati ya vitu ambavyo Mungu anachukia ni usinzi (Zaburi 12:31; 16:22), watoto kama kafara, upotovu wa jinsia (Walawi 20:1-23), na wale wanaotenda maovu (Zaburi 5:4-6; 11:5). Mithali 6:16-19 hunakili mambo saba ambayo Mungu anachukia: kiburi, uongo, mauaji, wapangao mabaya, wependao uovu, Ushahidi wa uongo, wasababizao vurumai. Tazama, katika ukurasa huu haujumulishi vitu tu ambavyo Mungu anachukia; inajumuisha watu pia. Sababu ni rahisi: dhambi haiwezi tenganishwa na mtenda dhambi isipokuwa msamaha unaopatikana kupitia kwa Kristo pekee. Mungu anachukia uongo, naam, lakini kila mara uongo unahusisha Mtu- mwongo-anayechagua kudanganya. Mungu hawezi hokum uongo bila kumhukumu mwongo.

Biblia inafunza wazi kuwa Mungu anapenda watu wa ulimwengu (Yohana 3:16). Mungu aliwahurumia nchi ovu ya Ninawi, huku akiwaleta katika toba (Yona 3). Mungu hafurahii kifo cha mwenye dhambi (Ezekieli 18:32). Yeye ni mvumilivu kwa, "maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba" (2Petro 3:9). Haya yote ni tibitisho la upendo- Mungu anatutakia yaliyo mema viumbe wake. Kwa wakati huo huo, Zaburi 5:5 yasema kuhusu Mungu, "Unawachukia wote watendao ubatili." Zaburi 11:5 ni kali zaidi: "Bwana humjaribu mwenye haki; Bali nafsi yake humchukia asiye haki, Na mwenye kupenda udhalimu."

Kabla mtu atubu na kuamini katika Yesu Kristo, yeye ni adui wa Mungu (Wakolosai 1:21). Hata kama kabla aokolewe, bado yeye anapendwa na Mungu (Warumi 5:8)-kwa mfano, Mungu alimtoa dhabihu mwanawe wa pekee kwa niapa yake. Swali tena linaja, ni nini kitamfanyikia mtu anayekaidi upendo wa Mungu, anakataa kutubu, na utundu anakwamilia dhambi zake? Jibu: Mungu atamhukumu, kwa sababu Mungu lazima ahukumu dhambi, na hiyo inamaanisha anamhukumu mwenye dhambi. Hawa ndio waovu ambao Mungu anachukia-wale ambao wanaendelea katika dhambi zao na kuasi, hata mbele ya neema na huruma ya Mungu kupitia Kristo.

Daudi anaandika, "Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia" (Zaburi 5:11). Kwa hakika zote mbili Zaburi 5 na Zaburi 11 zinaleta mkinzano kati ya mwenye haki (wale ambao wanajificha ndani ya Mungu) na waovu (wale ambao wanaasi kinyume na Mungu). Wenye haki na waovu wanafanya maamuzi tofauti na wana hatima tofauti- mmoja ataona dhihirisho la mwisho la upendo wa Mungu, na mwingine atajua dhihirisho la mwisho la ghadhabu ya Mungu.

Hatuwezi kupend na upendo kamilifu, au kuweza kuchukia na chuki kamilifu. Lakini Mungu anaweza kupenda na kuchukia kikamilifu, kwa sababu yeye ni Mungu. Mungu anaweza kuchukia bila kuwa na dhana ya dhambi. Anaweza kumchukia mwenye dhambi kwa njia kamilifu na takatifu na bado kwa upendo amsamehe mwenye dhambi wakati wa toba na Imani (Ufunuo 2:6; 2Petro 3:9).

Katika upendo wake kwa wote, Mungu amemtuma Mwanawe awe mkombozi. Waovu, ambao bado hawajapata kusamehewa Mungu anachukia "wingi wa makosa yao, Kwa maana wamekuasi Wewe" (Zaburi 5:10). Lakini- na hili ni muhimu kuelewa-Mungu anatamani mtu mwovu kugeuka kutoka dhambi zao na kujikinga ndani ya Kristo. Wakati wa imani inayooka, mwenye dhambi mwovu anatolewa katika ulimwengu wa giza na kuhamishwa hadi ulimwengu wa upendo (Wakolosai 1:13). Uadui wote umeyeyushwa, dhambi yote imeondolewa, na mambo yote yamefanywa upya (2Wakorintho 5:17).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mungu huchukia? Ikiwa Mungu ni upendo, anawezaje kuchukia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries