settings icon
share icon
Swali

Je, inamaanisha nini kwamba Mungu huangalia moyo (I Samweli 16:7)?

Jibu


Watu hupima tabia na dhamana ya wengine kwa kuangalia jinsi wanavyoonekana kimwili. Ikiwa mtu ni mrefu, mrembo, ana mwili mzuri, na amevaa vizuri basi ana sifa za kimwili ambazo kwa kawaida watu hupenda na kuheshimu. Mara nyingi, hizi ni sifa tunazotafuta kwa kiongozi. Lakini Mungu ana uwezo wa kipekee wa kuona mtu kwa undani. Mungu anajua tabia zetu za kweli kwa sababu Yeye "huangalia moyo."

Katika 1 Samweli 16, wakati ulikuwa umetimia wa Samweli kwenda kwa nyumba ya Yese huko Bethlehemu ili kutia wakfu atakayekuwa mfalme wa Israeli. Samweli alipotazama Eliabu, mwana wa kwanza wa Yese, alipendezwa na alichoona. "Hakika, mpakwa mafuta wa mwenyezi Mungu ndiye huyu," akasema nabii (mstari wa 6).

Lakini Mungu akamwambia Samweli, "Usitazame sura yake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo" (1 Samweli 16:7).

Sauli, mfalme wa kwanza, alikuwa mrefu na mwenye sura nzuri. Samweli labda alikuwa anatafuta mtu kama Sauli, na Eliabu alivutia sana. Lakini Mungu alikuwa na mtu tofauti akilini wa kutiwa mafuta ili awe mfalme wa Israeli. Hapo awali Mungu alikuwa amemfunulia Samweli kwamba alitafuta mtu ambaye atamtii kwa moyo wake wote (1 Samweli 13:14).

Samweli aliangalia wana wote wa kwanza saba wa Yese, lakini Bwana aliwakataa wote kama chaguo lake la mfalme. Mungu alikuwa anatafuta mtu ambaye alikuwa na moyo mwaminifu. Daudi, mwana wa mwisho wa Yese, ambaye hata hawakushughulika kumuita, alikua nje akichunga kondoo. Baada ya Samweli kupita mbele ya wana hao wengine, ndipo walimuita Daudi, na Bwana akasema, "sasa huyu ndiye" ( 1 Samweli 16:12).

Daudi alikuwa chaguo la Mungu- hakuwa mkamilifu lakini ni mwaminifu, mtu aliyepatana na moyo wa Mungu. Ingawa Biblia inasema kwamba alikuwa na sura nzuri (aya 12), Daudi hakuwa wa kuvutia. Lakini Daudi alikuwa ameamsha moyo wa kumtafuta Mungu. Akiwa peke yake malishoni akiwalisha mifugo, Daudi alikuja kumjua Mungu kama mchungaji wake (ona Zaburi 23).

Mungaro wa nje unaweza kudanganya. Mwonekano wa nje hauwezi onyesha chenye watu waliko ndani yao. Sura haiwezi tuonyesha dhamni ya mutu au tabia yake au uadilifu au uaminifu wake kwa Mungu. Sifa za nje kiufafanusi ni za juu juu. Maadili na kiroho ni vya muhimu zaidi kwa Mungu.

Mungu anaangalia ndani ya moyo. Moyo katika Maandiko ni maadili ya ndani ya mtu na maisha ya kiroho. Mithali 4:23 inaelezea kwamba kila kitu tunachofanya huchibuka kuotika kwa miyo yetu. Moyo ndio kiini, dhamani ya ndani ya kile tulicho: "Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina bora iliyomo moyoni mwake; na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya kutoka katika hazina mbaya iliyo moyoni mwake, kwa maana mtu huongea kutokana na yale yaliyojaa moyoni mwake" (Luka 6:45).

Kwa kila mmoja aliyemwona, Yuda Iskarioti alionekena kuwa mwanafunzi mwaminifu, lakini kuonekana kwake kulikuwa kunadanganya. Wanafunzi wengine hakuwa na habari ya kile kilichoendelea ndani ya moyo wa Yuda. Yesu ndiye pekee alijua moyo wa Yudasi: "Je, sikuwachagua nyinyi kumi na wawili? Hata hivyo, mmoja wenu ni Ibilisi!" (Yohana 6:70). Njia za Mungu ziko juu, na kuu na za hekima kuliko zetu (Isaya 55:8-9).

Mambo Ya Nyakati ya Pili 16:9 inasema kuwa macho ya Mungu yanaendelea kusunguka kila mahali duniani ili kuwadumisha watu ambao mioyo yao imejitolea kwake. Mungu anaweza kupenya kwa mioyo yetu, na kuchunguza maazimio yetu, na kujua kila kitu ndani yake ni kujua kila kitu kutuhusu (Zaburi 139:1). Mungu anajua ikiwa mtu atakuwa mwaminifu. Mungu anaona chenye watu hawawezi kuona.

Mfalme Daudi alikuwa mbali sana na ukamilifu. Alifanya usinzi na mauaji (2 Samueli 11). Lakini Mungu akaona ndaniya Daudi mtu mwenye imani kubwa ambaye alikuwa amejitolea kwa moyo wake kwa Mungu. Mungu aliona mtu ambaye angemtegemea bwana kwa nguvu na mwongozo (1 Samueli 17:45, 47; 23:2). Mungu aliona mtu ambaye anatambua dhambi zake na udhaifu na anaweza kuungama na kumwomba Mungu msamaha (2 Samueli 12; Zaburi 51). Mungu aliona ndani ya Daudi mtu aliyempenda Bwana wake; mtu ambaye alimwabudu Bwana na nafsi yake yote (2 Samueli 6:14); mtu ambaye alikuwa amekwisha pata utakazo na msamaha wa Mungu (Zaburi 51) na alikuwa ameelewa uzito wa upendo wa Mungu kwake (Zaburi 13:5-6). Mungu aliona mtu mwenye kweli na aliye na uhusiano wa kibinafsi na Muumba wake. Wakati Mungu aliangalia moyo wa Daudi, aliona mtu aliyepatana na moyo wake (Matendo 13:22).

Kama Samueli, hatuwezi kuona chenye Bwana anaona, na ni lazima tumtegemee kwa hekima. Na tunaweza amini kuwa, wakati Mungu anaangalia miyo yetu, anaona uaminifu wetu, uadilifu wetu kamili, na tunacho kidhamani kibinafsi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, inamaanisha nini kwamba Mungu huangalia moyo (I Samweli 16:7)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries