settings icon
share icon
Swali

je! Inamaanisha nini kuwa Mungu hadhihakiwe?

Jibu


Kumdhihaki Mungu ni kutomweshimu, kumfedhehesha, au kutomjali. Ni kosa mbaya sana linalotendwa na wale hawamchi Mungu au wanaokataa kuwepo kwake. Mfano rahisi unayojulikana kama dhihaki ni kusesha heshima kwa kinachojulikana kama matusi au tendo la dharau. Limehusishwa na kejeli, mzaha, na kukaidi. Dhihaki ni nia isiyo ya heshima ambayo inaonyesha ukadiri hafifu, dhararu au ukaidi wa wasi.

Katika Biblia ukejeli ni tabia na nia ambayo inaoneshwa na wapumbavu (Zaburi 74:22), waovu (Zaburi 1:1), adui (Zaburi 74:10), wanaochukia maarifa (Mithali 1:22; 13:1), wenye kiburi (Zaburi 119: 51; Isaya 37:17), na wasio weza kufunzika (Mithali 15:12). Mtu mwenye kejeli hukosa dhadhimini ya kufanya uamuzi fahamu kwa dhambi. Wakejeli hana roho wa itiivu, kufunzwa, kutambua, hekima, ibada or Imani.

Wale wanaomdhihaki Mungu watawadhihaki wale wamchao Mungu vile vile. Nabii Yeremia, "alikuwa anachekelewa na watu wote" na akadhihakiwa "katika nyombo siku yote" (Maombolezo 3:14). Kejeli kwa manabii wa Mungu ilikuwa jambo la kawaida (2 Mambo ya Nyakati 36:16). Nehemia alidhihakiwa na maadui wake (Nehemia 2:19). Elisha alidhihakiwa na vijana wa Betheli (2Wafalme 2:23). Na hata Bwana wetu Yesu alidhihakiwa- na Herode na askari wake (Luka 23:11), na askari wa Kirumi (Marko 15:20; Luka 23:36), na yule mwizi msalabani (Luka 23:39), na viongozi wa Kiyahudi waliopita karibu na msalaba (Mathayo 27:41).

Ni rahisi kwetu kama waumini kuwanyoshea kidole wale wasio Wakristo ambao humdhihaki Mungu. Lakini kejeli hila kwa Mungu na tena mbaya sana, hutokana na wenzetu ambao huketi kanisani. Tuna hatia ya dhihaka wakati tunaonyesha kwa nje ukuaji wetu wa kiroho au uungu wetu bila mbadiliko wa ndani wa moyo.

Mhubiri wa miaka ya 1800 Charles G. Finney aliandika kuhusu madhara ya kumdhihaki Mungu: "Kumdhihaki Mungu ni kujifanya kumpenda Mungu na kumtumikia ile hali hatufanyi hivyo; na kutenda kinyue, kutokuwa wakweli na kuwa wanafiki katika kukiri kwetu, tukijifanya kuwa tunamtii, mpenda, tumikia, na kumwabudu yeye, wakati hatufanyi hivyo…kumkejeli Mungu huwa inahusunisha Roho Mtakatifu na kukausha dhana; na hivyo dhambi hukomaa na kuwa dhabiti. Pole pole moyo huwa mgumu katika kwendelea kwa hali hiyo."

Mungu anawaonya wakejeli kwa kile kisicho takatifu. Sefania alitabiri kuanguka kwa Moabu na Amoni akisema, "Hayo yatakuwa malipo ya kiburi chao, kwa sababu waliwadhihaki na kujigamba dhidi ya watu wa Mwenyezi-Mungu wa majeshi" (Sefania 2:10). Isaya 28:22 inatuonya kuwa ukejeli utasababisha minyororo ya dhambi ya Yuda kuwa dhabiti na kuwa uharibifu utafuatia. Mithali 3:34 inasema kuwa Mungu atawadharau watu wenye dharau na kuwafadhili wanyenyekevu na waliokandamizwa. Wafalme wa Pili 2:24 imenakili adhabu ambayo itawapata vijana waliomkejeli Elisha.

Hii ndio maana ya kuwa Mungu hadhihakiwi. Kunayo matokeyo ya kupuuaza maagizo ya Mungu na kuchagua dhambi kimakusudi. Adamu na Hawa wajaribu na kusababisha husuni na kifo katika ulimwengu (Mwanzo 2:15-17; 3:6,24). Udanganyifu wa Anania na Safira ulileta hukumu ya hadharani (Matendo 5:1-11). Wagalatia 6:7 inasema kanuni ya wote: "Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna."

Mungu hawezi danganywa (Waebrania 4:12-13). Dhambi ya Akani (Yoshua 7) na kutoroka kwa Yona (Yona 1) sio eti havikuwa vimejulikana kwa Mungu. Neno la Yesu lililoruduwa kwa kila kanisa katika Ufunuo 2-3 lilikuwa, "Nayajua matendo yako." Ni sisi tu hujidanganya wakati tunafikiria nia zetu na matendo yetu hayaonekani na Mungu mwenye mamlaka yote na ajuaye mambo yote.

Biblia inatuonyesha njia ya kuishi maisha yenye baraka, wakati mwingine kwa mifano ya wanaume na wanawake wa Mung una wakati mwingine kwa mifano mibaya ya wale ambao huchagua kuenenda njia nyingine. Zaburi 1:1-3 inasema, "Heri mtu asiyefuata shauri la waovu, asiyeshiriki njia za wenye dhambi, wala kujumuika na wenye dharau; bali huifurahia sheria ya Mwenyezi-Mungu, na kuitafakari mchana na usiku. Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito, unaozaa matunda kwa wakati wake, na majani yake hayanyauki. Kila afanyalo hufanikiwa."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

je! Inamaanisha nini kuwa Mungu hadhihakiwe?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries