settings icon
share icon
Swali

Mungu anaweza danganya?

Jibu


Mungu ni mtakatifu (Isaya 6:3), na kigezo hicho huifanya ikuwe ngumu Mungu kudanganya. Utakatifu wa Mungu ni maadili yake na uadilifu wake kamilifu humtofautisha mbali na uumbaji wake. Utakatifu wa Mungu unahusiana ubora wake unaopita mipaka. Mungu hafuatishi kiwango chochote cha usafi, Yeye mwenyewe ni kiwango. Mungu ni mtakatifu kabisa na usafi usio na kikomo ambao hautaweza kubadilishwa. Kwa sababu ya utakatifu wake, wakati Mungu anasungumza, hawezi kunena uwongo. Hadanganyi kamwe, habadiliki kamwe au kutowakilisha asemacho au afanyacho. Udanganyifu ni kinyume na hali yake.

Kwa sababu Mungu hawezi kudanganya, Neno la Mungu, Biblia inaweza kuaminika kikamilifu (1Wafalme 8:56; Zaburi 119:160). "Kila neno la Mungu limehakikishwa" (Mithali 30:5). Maadili ya Mungu na mawasiliano yanajibuka kutoka kwa maadili yake ni matakatifu kuliko kitu chochote ulimwengu huu unaweza toa. "Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba" (Zaburi 12:6).

Msingi wa ahadi ya Mungu kwa Ibrahim katika Mwanzo 12 ulikuwa hali ya Mungu ambayo haibadiliki; ambayo ndio udhabiti wa maadili yake ya kweli ambayo hufanya kila kitu asemacho kuwa cha kweli. "Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake, akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza" (Waebrania 6:13-14). Kifungu hiki kinaendelea kwa kauli kwamba "Mungu hawezi kusema uongo" (Waebrania 6:18).

Ikiwa Mungu angeweza kusema uwongo, basi hangeweza kuwa Zaidi ya vitu vyote; hakika angekuwa kama sisi-ubinadamu una sifa ya kuficha, kuwakilisha vibaya, na kugeuza ukweli. Lakini "Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?" (Hesabu 23:19).

Kutoka mwanzo Mungu amejitunuku Imani (Mwanzo 15:6; Waebrania 11:6). Imani au tumaini inaweza kuwa kitu kizuri ikiwa lengo lake linaweza kuaminika. Tumaini katika mtu asiyeaminika au kitu ni hasara. Ikiwa Mungu anaweza kudanganya basi neno lake ni la kutiliwa shaka, na hivyo hastahili imani yetu. Lakini, jinsi ilivyo Yeye anajisimamia: "Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu, Maagizo yake yote ni amini" (Zaburi 111:7).

Yesu ambaye yuna "namna ya Mungu" (Wafilipi 2:6), yeye "amejawa na neema na kweli" (Yohana 1:14). Kila neno ambalo Yesu alisema na kufundisha ilikuwa ukweli mtupu. Kila jambo alilofanya lilidhihirisha ukweli. Watu kama vile Pilato kila mara wangechanganyikiwa na kweli (Yohana 18:38), lakini Yesu alikuja ili, "ashuhudie kweli" (aya ya 37). Yesu hawezi kudanganya kwa sababu Mungu hawezi kudanganya, "Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu" (Yohana 18:37).

Mungu ambaye hawezi kudanganya anapita kiwa cha ukamilifu wa maadili. Anawataka wanawe wawe na maadili safi. Mungu hawezi kudanganya na hivyo wafuasi wa Kristo hawapaswi kudanganya: ''Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake" (Waefeso 4:25). ''Mungu anaishi kwa mtu gani?" mtunga zaburi anauliza. Jibu la sehemu ni kuwa Mungu hudumu kwa ''Kwa yule …asemaye kweli kwa moyo wake (Zaburi 15:2). Na tuipende kweli jinsi Mungu anavyoipenda.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mungu anaweza danganya?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries