settings icon
share icon
Swali

Je, Mungu anasema nini kunihusu?

Jibu


Kabla tuangalie kile Biblia inasema kuhusu mtu binafsi, tunahitaji kuharibu dhana ambayo inakua kwa umaarufu ndani ya Ukristo wa sasa. Ujumbe unaopotosha, ambao umekumbatiwa na wahubiri wa viombo vya habari tofauti tofauti, waandishi wa vitabu wenye mauzo mazuri, na walimu waliofanikiwa, ni kwamba YOTE ni kunihusu. Mungu ni kunihusu. Biblia ni kunihusu. Ulimwengu ni kunihusu. Ndani ya mafundisho haya ni dhana potofu kwamba Mungu yupo kwa ajili yangu. Badala ya Mungu kuumba mwanadamu kwa mfano Wake, tumejaribu kuumba tena Mungu kwa mfano wetu.

Mungu ana mengi ya kusema kutuhusu sisi kabila la binadamu, ingawa, kuna mengi tunaweza kujifunza kujihusu sisi wenyewe kibinafsi katika Biblia. Uamuzi wa Mungu kuzungumza na sisi sio sababu ya kiburi kwa upande wetu bali ya shukrani ya milele. Ili kufahamu kile Mungu anasema kunihusu, lazima nifahamu kile Mungu anasema kuhusu Yeye mwenyewe. Vinginevyo, haijalishi. Ila Mungu ni yule anasema alivyo, basi haijalishi anasema mimi ni nani.

Kitu moja Mungu anasema kunihusu ni kwamba nimeumbwa kwa mfano Wake (Mwanzo 1:27). Mungu aliumba vitu mingi kwa kusema, lakini wakati aliumba mwanadamu, alifanya tofauti. Alichukua mchanga, akaunda binadamu kutoka kwa mchanga ambao alikuwa ameumba, na kisha akapuliza uhai Wake mwenyewe kwa huyo binadamu. Wakati huo, mtu akawa “roho inayoishi” (Mwanzo 2:7). Mungu baadaye akaunda mwanamke kutoka kwa ubavu wa mwanaume na akaunganisha mwanaume na mwanamke pamoja kama mme na mke (Mwanzo 2:21-24). Hawa binadamu walikuwa tofauti kutoka kwa wanyama na mimea ambayo pia ilikuwa na uhai. Mwanaume na mwanamke alikuwa na pumzi ya Mungu katika mapafu yao. Walipewa roho ya milele, jinsi tu Mungu anayo. Hizo roho zitaishi milele, na ilikuwa ni mpango wa Mungu kwamba ziwepo ndani katika ushirika na Yeye.

Kitu kingine Mungu anasema kunihusu ni kwamba mimi ni mwenye dhambi, nimetengwa kutoka kwa Mungu. Adamu na Hawa walikosa kutii Mungu, na tendo hilo likaleta dhambi katika dunia iliyokamili ya Mungu (Mwanzo 2:16-17; Mwanzo 3). Kuanzia wakati huo, binadamu wote wanazaliwa na asili ya dhambi ya wazazi wao (Warumi 5:12). Asili ya dhambi ambayo tunarithi—na dhambi ambayo tunafanya binafsi—inatutenga kutoka uwepo mtakatifu wa Mungu (Warumi 3:23; 6:23).

Kitu kingine Mungu anasema kunihusu ni kwamba Muumbaji wangu ananipenda. Si lazima anipende. Lakini asili Yake ni upendo (1 Yohana 4:8), na anaweka upendo Wake juu yetu. Katika upendo Wake, Mungu nafanya kazi kwa manufaa yetu ya milele, hata kwa kiwango cha kujitolea Mwenyewe ili kutuokoa (Warumi 5:8).

Kitu kingine Mungu anasema kunihusu ni kwamba aliniunda kutimiza kusudi kipekee (Zaburi 139:13-16). Mungu ametutengeneza kila mmoja wetu jinsi anavyotaka Yeye kwa ajili ya utukufu Wake na kuleta mapenzi Yake. Hata uwepo wa mapigano na udhaifu wetu unasisitiza neema Yake na kutusababisha kumshikilia Yeye (ona Kutoka 4:11).

Basi Mungu alionyesha upendo Wake kwa tendo la ukarimu zaidi ulimwengu hautawai kujua. Alituma Mwana Wake Mwenyewe, Yesu, kwa dunia kuchukua adabu ambayo dhambi zetu zinastahili (Yohana 3:16-18; Wakolosai 2:14; 2 Wakorintho 5:21).

Kitu kingine ambacho Mungu anasema kunihusu ni kwamba nipo upande mmoja kati ya makundi mawili: wana wa Mungu au wana wa shetani (1 Yohana3:7-10). Wana wa Mungu ni wale ambao wana Imani katika kifo na ufufuo wa Yesu. Wamepokea msamaha kamili, msamaha wa dhambi, na uzima wa milele (Yohana 1:12). Wanachukuliwa katika familia ya Mungu (Warumi 10:9-13). Wana wa shetani ni wale ambao wanamkataa Kristo na zawadi Yake ya ukombozi. Bado wako katika dhambi na chini ya lawama ya Mungu. Wakolosai 3:1-17 inaeleza tofauti kati ya wale ambao wako chini ya ghadhabu ya Mungu na wale ambao wamerejeshwa na Mungu.

Hivyo, kile Mungu anasema kunihusu inategemea msimamo wangu na Kristo. Kwa wale wanaomkataa, anasema, “Tubuni basi, mrejee” (ona Matendo ya Mitume 3:19). Kwa wale wanampokea, anasema, “Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako” (Luka 5:20) na “Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu” (1 Petro 1:15-16). Wana Mungu wamekwisha chaguliwa, thibitishwa, na kupendwa kwa dhati. Lakini anataka wana Wake wachukue sura ya familia. Anatuokoa ili atuendanishe na usawa wa Yesu (Warumi 8:29).

Wakati nimechukuliwa na Mungu kama mtoto Wake, ana mengi ya kusema kunihusu. Nina sura mpya (Yohana 3:3). Mimi si mtoto wa ghadhabu tena (Waefeso 2:3), kusudiwa daima bila Mungu (Mathayo 25:41). Mimi niko “katika Kristo,” nimefunikwa na haki Yake na kukubalika kamili na Mungu (Wafilipi 1:1). Mungu anasema kwamba siko tena chini ya lawama (Warumi 8:1); Haoni tena kutokamilika kwangu; Badala yake anaona haki ya Mwanaye (Waefeso 2:13; Waebrania 8:12). Mungu anasema mimi ni zaidi ya mshindi “kwa yeye aliyetupenda” (Warumi8:37). Anasema kwamba “ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (2 Petro 1:4).

Katika Siku ya Hukumu, kile Mungu anasema kunihusu kitafanya tofauti daima. Maneno ya Mungu kwa Watu Siku hiyo yaktakuwa labda, “Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu!” (Mathayo 7:23) au, “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu! ….. ingia katika furaha ya bwana wako!” (Mathayo 25:23). Wakati tunasimama mbele za Mungu, kile anasema kutuhusu kitategemea uhusiano, Imani kwa Yesu Kristo (Yohana 3:18). Mungu alimtuma Mwanaye wa pekee ili kulipa deni. Lazima tujibu swali hili: “Je, nitafanya nini na Kristo?”

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mungu anasema nini kunihusu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries