settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Mungu anaruhusu udanganyifu?

Jibu


Kusudi la Mungu ni kuwa watu wote watubu and waokolewe (2Petro 3:9). Wakati huo huo, Shetani ambaye ni "baba wa uongo" (Yohana (8:44), anawadanganya watu ambao wanapaswa kuikubali kweli. "Hao hawaamini kwa sababu yule mungu wa ulimwengu huu amezitia giza akili zao wasipate kuuona wazi mwanga wa Habari Njema ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano kamili wa Mungu" (2Wakorintho 4:4). Mungu anaweza zitisha uongo wa Shetani na kuwapa watu nafasi ya kupambana.

Biblia inatoa taswira ile ile ya jinsi dhambi na uongo vinakaribiana. Chenye kimefunuliwa ni kwamba njina tunajaribu kufikiria udanganyifu ni botovu kidogo. Kusungumza kiroho, ulaghai ni zaidi ya hila au kudanganywa. Ili uokolewe, mtu haitaji kiwango chochote cha ufahamu, uwezo wa kifalsafa, au hekima (Wagalatia 3:28; 1 Wakorintho 1:20, 26). Hakika, mwanadamu ana mazoea mabaya ya kutumia ufahamu wa juu kuansisha njia bunifu za kutenda dhambi.

La muhimu kuelewa ulaghai wa kiroho na hoja kwamba kila mara tunaamua chenye tunataka kuamini badala ya kile tunapaswa kuamini, hata kama kukiwa na udhibitisho (Luka 16:31). "Ingawa Yesu alifanya miujiza hii yote mbele yao, wao hawakumwamini. 38Hivyo maneno aliyosema nabii Isaya yakatimia" (Yohana 12:37). Kumbuka hili hawawezi kumwamini Yesu, pasipo na miujiza. Kutoamini kwao kulikuwa kwa hiari.

Kuanguka kwa Hawa dhambini ni mfano wa kwanza wa vile ulaghai wa kiroho hufanya kazi. Wakati ibilisi anamuuliza, "Je Mungu alisema…" itikio la Hawa kwa kunukuu kile Mungu alikwisha sema, ijapokuwa aliongezea kwa amri (Mwanzo 3:1-3). Anajua chenye anafanya na chenye hastahili kufanya. Na hapo Ibilisi anamjaribu na kile atakipata kutokana na kula kutoka kwa mti (Mwanzo 3:4-5), na anagundua sehemu zingine za kuvutia za tunda (Mwanzo 3:6). Hawa alidanganywa, na ule nyoka alikuwa mjanja sana (2 Wakorintho 11:3), lakini hatima aliamua kutomtii Mungu.

Alipouliwa dhambi zake, Hawa akasema, "Nyoka alinidanganya, nami nikala" (Mwanzo 3:13b). Neno halisi la Kiebrania la "kudanganywa" linamaanisha kuhadaa au ujanja. Hawa alihadaiwa, lakini pia alikuwa na uamuzi katika jambo hilo. Alitumia hiari yake huru aliyopewa na Mungu kufanya uamuzi mbaya, akitafuta raha na kuinuliwa kibinafsi zaidi ya kusudi ambalo Mungu alikuwa nalo kwake.

Hali kama hiyo ipo leo hii. Shetani hushawishi makusudi yetu ya halisi na kutusihi kuyatimiza kwa njia ambazo hazimweshimu Mungu. Makusudi yetu ya kujinufaisha yanafanya ulaghai wa Shetani kuwa wa nguvu zaidi.

Mungu amememtuma mkombozi (Yohana 3:16), ameijaza dunia na ishara zake (Warumi 1:20), ameifanya rahisi Yeye kupatikana kwa wale wamtafutao (Kumbukumbu 4:29), na anawaifadhi wale wakujao kwake (Yohana 6:7). Wakati watu wanakataa chenye "kinaonekana wazi" kuhusu Mungu (Warumi 1:20), inaongoza kuelekea upotevu na giza kwa "moyo mpumbavu" (aya ya 25). Kwa maneno mengine, ulaghai wa kiroho wa mwanadamu ni matokeo ya moja kwa moja kweli tayari. Mwenye hajaokoka amefanya ubadilisho-uongo licha ya ukweli- na Shetani anafurahi kuwezesha ubadilisho huo kwa kumpa mwenye dhambi aina mbali mbali za uongo kuchagua.

Mtu yeyote anayemkataa Mungu anadhahatari kuinngia katika ulaghai wa kiroho (2Wathesaloniki 2:8-10). Asili inachukia utupu, na uwazi ambao umeletwa kwa kutokuwa na kweli hivi karibuni utajazwa na kitu kilicho mbali na kweli. Tupilia mbali kweli na utaanza kuamini kuhusu kitu chochote.

Hawa hakutenda dhambi kwa sababu hakuwa na tumaini kwa kushindwa na nguvu ya pepo, kumfanye yeye kutenda maovu huku akifikiria alikuwa anatenda wema. Naam, alidanganywa, lakini aliamua kusikiza uwongo. Kilichofuatia yeye alitamani kuangazia kile alichokatazwa na hatimaye, kula kwake lile tunda alikuwa na tumaini kuwa maisha yatakuwa mazuri.

Dhambi zote za mwanadamu zinakuja kwa misingi ya uchaguzi (1 Wakorintho 10:13). Wakati tunaikataa kweli, tunajitia hatarini ya kuadaiwa. Kuendelea kukataa ukweli wa kiroho unasabisha ulaghai wa kiroho kama matokeo yake ya kipekee.

Mungu mara nyingi huruhusu ulaghai wa kiroho kama njia ya adhabu kwa dhambi ya makusudi, na ndio ajibushe ndani yetu ufahamu katika maisha yetu jinsi tunavyomhitaji yule ambaye Yeye mwenyewe ni kweli, Bwana wetu Yesu Kristo (Yohana 14:6).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Mungu anaruhusu udanganyifu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries