settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Mungu anayaruhusu maradhi?

Jibu


Swala la maradhi mara nyingi huwa ngumu kulijadili. La muhimu ni kukumbuka kuwa njia za Mungu zi juu kuliko zetu (Isaya 55:9). Wakati tunateseka kwa maradhi na magonjwa au maumivu, mara nyingi tunaangazia mateso yetu binafsi. Katikati mwa mateso ni vigumu kuzingatia yale ambayo Mungu atatenda baadaye kama matokeo. Warumi 8:28 inatukumbusha kwamba Mungu kutoka kwa hali yoyote anaweza kuleta mazuri. Watu wengi wanatizama nyuma wakati wa kipindi cha magonjwa kuwa nyakati ambazo walikua karibu na Mungu, wajifunza kumtegemea Mungu zaidi, na walijifunza jinsi ya kuthamini maisha. Huu ndio mtizamo ambao Mungu ako nao kwa sababu yeye ni Mwenyezi na anajua matokeo ya mwisho.

Hii haimanishi kila wakati maradhi hutoka kwa Mungu au kila mara Mungu hutuletea magonjwa ili kutufunza kiroho. Katika ulimwengu ulioharibiwa na dhambi, maradhi, magonjwa, na kifo vitakuwa nasi kila wakati. Sisi ni viumbe vilivyoanguka vilivyo na miili ambayo inaweza kabiliwa na maradhi na magonjwa. Maradhi mengine ni kwa ajili ya sababu ya mwenendo wa asili katika ulimwengu huu. Maradhi yanaweza tokea kwa sababu ya kufamiwa na mapepo. Biblia inasimulia matukio mengi wakati mateso ya kimwili yalisababisha na shetani na mapepo zake (Mathayo 17:14-18; Luka 13:10-16). Kwa hivyo maradhi mengine hayatoki kwa Mungu, bali ni kwa shetani. Hata katika matukio haya Mungu bado yuko ushukani. Mungu wakati mwingine anaruhusu dhambi/shetani kusababisha mateso ya kimwili. Hata wakati maradhi moja kwa moja hayatoki kwa Mungu, bado Yeye huyatumia kulingana na mapenzi yake kamilifu.

Ni wazo lizilokataliwa, kwamba Mungu wakati mwingine kwa makusudi huruhusu au hata kusababisha ugonjwa ili kutimiza makusudi yake ya kifalme. Huku maradhi yakiwa hayajatajwa moja kwa moja katika kifungu, Waebrania humwelezea Mungu kuwa anatuadhibu "huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani" (aya ya 11). Maradhi yanaweza kuwa njia ya adhabu ya upendo ya Mungu. Ni vigumu kwetu kuelewa ni kwa nini Mungu anafanya kazi kwa njia hii. Lakini kuamini katika Mungu Mwenyezi, hamna njia nyingine kuliko mateso kuwa kitu Mungu anaruhusu au sababisha.

Mfano wa wazi wa hili katika Maandiko unapatika katika Zaburi 119. hebu angalia yanayoendelea katika aya za 67, 71 na 75- "Kabla sijateswa mimi nalipotea, Lakini sasa nimelitii neno lako…Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa, Nipate kujifunza amri zako… Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki, Ee Bwana, na kwa uaminifu umenitesa." Mtunga Zaburi 119 aliyaona mateso kutoka kwa mtazamo wa Mungu. Ilikuwa bora kwake kuteswa. Ilikua ni uaminifu ambao ulimfanya Mungu kumtesa. Matokeo ya mateso yalikuwa ili ajifunze maagizo ya Mungu na kutii neno lake.

Tena, maradhi na mateso kwamwe sio rahisi kubambana nayo. Jambo moja kwa hakika, maradhi yasitufanye kupoteza imani yetu kwa Mungu. Mungu ni mwema, hata wakati tunapoteseka. Hata wakati wa upeo wa mateso ambaye ni "kifo" bado ni tendo wema la Mungu. Ni vigumu kuliwaza kuwa kila mmoja aliyeko mbinguni kwa minajili ya maradhi au mateso anajutia ni kwa nini waliyapitia hayo maishani.

Jambo la mwisho la kutilia maanani: wakati watu wanateseka, ni jukumu letu kuwahudumia, kuwajali, kuwaombea, na kuwafariji. Wakati mtu anateseka, sio bora kila mara kusisitiza kuwa Mungu ataleta mema tokana na mateso. Naam, huo ndio ukweli. Ijapokuwa, katikati mwa mateso, sio wakati mwafaka wa kushiriki ukweli huo. Watu wanaoteseka wanahitaji upendo wetu na motisha, sio hasa kumbusho la theolojia nzuri ya kibiblia.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Mungu anayaruhusu maradhi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries