settings icon
share icon
Swali

Je, Mungu anapenda kila mtu au ni Wakristo tu?

Jibu


Kuna hisia ambayo Mungu anapenda kila mtu katika ulimwengu wote (Yohana 3:16, 1 Yohana 2:2, Warumi 5:8). Upendo huu si wa masharti, ni msingi tu juu ya ukweli kwamba Mungu ni Mungu wa upendo (1 Yohana 4:8, 16). Upendo wa Mungu kwa wote unadhihirika kwa watu katika ukweli kwamba Mungu alionyesha huruma zake kwa kutowaadhibu watu kwa ajili ya dhambi zao (Warumi 3:23; 6:23). Upendo wa Mungu kwa ulimwengu ni wazi katika ukweli kwamba Yeye huwapa watu nafasi ya kutubu (2 Petro 3:09). Hata hivyo, upendo wa Mungu kwa ulimwengu haina maana kuwa atapuuza dhambi. Mungu ni Mungu wa haki (2 Wathesalonike 1:6). Dhambi haiwezi kwenda bilaa adhabu milele (Warumi 3:25-26).

Tendo kuu la upendo wa milele limeelezwa katika Warumi 5:8, Bali Mungu alionyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu katika njia hii. Wakati tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu” Mtu yeyote ambaye hupuuza upendo wa Mungu, na kumkataa Kristo kama Mwokozi, aliyemnunua (2 Peter 2:1).atakuwa chini ya ghadhabu ya Mungu milele (Warumi 1:18), si upendo wake (Warumi 6:23). Mungu anapenda kila mtu bila masharti katika hayo huonyesha huruma zake kwa kila mtu kwa kutowaangamiza mara moja kwa sababu ya dhambi. Wakati huo huo, Mungu analo agano la upendo kwa wale ambao wameweka imani yao kwa Yesu Kristo kwa ajili ya wokovu (Yohana 3:36). Wale tu ambao wanaamini katika Yesu Kristo kama Bwana wao na Mwokozi watauonja upendo wa milele wa Mungu.

Je, Mungu Humpenda kila mtu? Naam. Je, Mungu hupendo Wakristo zaidi kuliko anavyopenda mashirika yasiyo ya Wakristo? La. Je, Mungu hupendo Wakristo kwa kiasi tofauti na anavyopenda wasio Wakristo? Naam. Mungu anapenda kila mtu sawia, katika kwamba yeye ni mwenye huruma kwa watu wote. Mungu anapenda Wakristo kwa sababu wao ndio wako na neema yake ya milele na huruma na ahadi yake ya upendo wa milele mbinguni. upendo usio na masharti Mungu anao kwa kila mtu unastahili kutuleta katika imani yeke, kwa kuupokea katika furaha kubwa upendo mkuu wa masharti ambao ametupa wale ambao watampokea Yesu Kristo kama mwokozi wa wote.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mungu anapenda kila mtu au ni Wakristo tu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries