settings icon
share icon
Swali

Je! Mungu ananipenda?

Jibu


Swali kuwa ikiwa Mungu anatupenda- kipekee na kibinafsi- ni la kawaida. Likizungukwa na upendo kisharti na ulio na mwisho wa mwanadamu, hatuwezi fikiria kiurahisi kwamba Mungu anatupenda. Tunajua udhaifu wetu. Tunajua kwamba Mungu ni mkamilifu na hana dhambi. Tunajua kuwa sisi sio wakamilifu wala bila dhambi. Ni kwa nini Mungu ambaye ni mtakatifu kabisa atupende sisi tulio wadhaifu na wenye dhambi? Na huku ukweli mkuu wa injili ni kwamba, Yeye anatupenda! Mara na mara, maandiko hutukumbusha upendo wa Mungu kwetu.

Kwa kuanzia, Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake mwenyewe. Alifanya hivyo kwa uangalifu mkubwa na huruma. "akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai… Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu" (Mwanzo 2:7, 21-22). Kuna uhusiano hapa kati ya Mung una mwanadamu. Kwa viumbe wengine, Mungu alisumgza na vikawa. Lakini Mungu akachukua muda wake kwa kumuumba mwanaume na mwanamke. Aliwapa mamlaka juu ya ardhi (Mwanzo 1:28). Mungu alihusiana moja kwa moja na Adam una Hawa. Baada ya kuanguka, wanandoa hao walijificha kutoka kwa Mungu wakati alikuja "akitembea bustanini wakati wa jua kupunga" (Mwanzo 3:8). Haikuwa jambo lisilo la kawaida kwa wao kuongea na Mungu; bali hakuwa kawaida wao kujificha.

Uhusiano na Mungu ulivunjika, lakini upendo wake ukasalia bado. Kilichofuata baada ya Mungu kutangaza laana juu hao wana ndoa, Maandiko yanaleta taswira nyingine ya upendo wa Mungu. "Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa" (Mwanzo 3:21-23). Hatua ya Mungu hapa sio cha kulipisa kisasi au adhabu bali ni la kutunza. Mungu aliwavisha Adamu na Hawa ili kuficha aibu yao. Aliwafukuza nche mwa Edeni ili kuwakinga kutoka kwa maovu zaidi. Mungu alitenda kwa upendo. Baadaye mpango wa Mungu wa ukombozi na urejesho ulianza kujidhihirisha-mpango ambao haukuanzishwa baada ya kuanguka, bali kabla ya uumbaji (1Petro 1:20). Mungu anapenda mwanadamu zaidi hadi aliamua kutuumba hata kama alijua uchungu amabo utamsababisha kutukomboa.

Kunavyo vifungu vyingi ambavyo vinaonyesha upendo wa Mungu. Tuanweza kuuona upole wake katika Agano la Kele and Jipya. Daudi pamoja na watunga zaburi wengine walikuwa kinaga naga juu ya upendo wa Mungu. Angalia Zaburi 139. Wimbo ulio bora ni taswira nyingine kubwa ya upendo. Upendo wa Mungu uu Dhahiri katika historia ya Waisraeli, vile alivyo endelea kuwatunza waliobaki na akaapa na watu wake kuwa watii na waishi. Mungu anaonekana kuwa wa haki, na pia mwenye huruma. Yeye ni mpole. Ni Mungu mwenye wivu na watu wake, anatamni uhuriano huo urejeshwe.

Mara nyingine tunaangalia katika Agano la Kale na kufikiria kwamba Mungu anapenda watu kama taifa kwa ujumla na sio watu binafsi. Lakini ni vyema kukumbuka kuwa Ruth, Hagari, Daudi, Ibrahimu, Musa na Yeremia wote walikuwa watu binafsi. Mungu alikia kwa maisha ya kila mmoja wao na kuwapenda wao kibinafsi. Huu upendo uu Dhahiri katika utu wa Yesu.

Mungu alijitwika ngozi ya mwanadamu ili atukomboe (ona wafilipi 2:5-11). Aliingia ulimwengu wetu kama mtoto aliyezaliwa kwa familia isiyo ya kifahari kwa njia ya unyenyekevu (usiku wake wa kwanza alilala kwenye zizi la ngombe). Yesu alikuwa vile mtoto yeyote hukua. Wakati wa huduma yake ya hadhara, kila mara alijumuika na wale waliokataliwa katika jamii. Alisimama kwa ajili ya wagonjwa. Aliwaponya. Aliwasikiliza watu. Aliwabariki Watoto. Pia alitufunza kuhusu upendo wa Mungu. Luka 13:34 inamnakili Yesu akilia, "Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka!" Hii inasungumzia makusudio ya moyo wa Mungu kuwa watu watamrudia Yeye. Anatuhenzi sana. Sio kwa kutuadhibu, bali ni kwa kutupenda.

Pengine taswira kuu ya upendo wa Mungu ni shauku ya Yesu. Paulo anatukumbusha, "Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi" (Warumi 5:6-8). Kazi ya Yesu msalabani ilikua tangazo la wazi la upendo lisilo na kosa na la upendo. Na pendo hili si la masharti. Tulikuwa katika hali mbaya wakati Yesu alikufa kwa ajili yetu. "Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu… Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema" (Waefeso 2:1, 4-5).

Wokovu huu umefanya kuwe na uwezekano wa maisha halisi. "Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu," Yesu akasema. "Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele" (Yohana 10:10). Mungu si mchoyo. Anataka kuachilia utel wa upendo wake kwetu. "Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti," Paulo asema katika Warumi 8:1-2.

Kumbuka, mbeleni Paulo alikuwa adui wa Kristo. Kwa ukali aliwatesa Wakristo. Aliishi kwa barua ya sheria kuliko fahamu ya upendo wa Mungu. Hata kama Paulo angeliwaza upendo wa Mungu, pengine angehisi kuwa Mungu hangeweza kumpenda pasipo na kufuata sheria. Na huku katika Kristo, alipata neema ya Mungu na akaukubali upendo wa Mungu. Tangazo lake kuu la upendo wa Mungu ni hili: "Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?... Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?... Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu" (Warumi 8 :31-32, 35-39).

Kwa hivyo jibu rahisi ni, "naam." Naam, Mungu anakupenda! Huenda inaweza kuwa ngumu kuamini, hiyo ndio kweli.

Maandiko mengine kuhusu upendo wa Mungu kwako:

Yohan 4:8 — "… Mungu ni upendo"

Waefeso 5:1-2 — "Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa; mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato."

Waefeso 5:25-27 — "Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa."

Yohan 15:9-11 — "Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu. Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe"

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mungu ananipenda?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries