settings icon
share icon
Swali

Mungu anahitaji nini kutoka kwangu?

Jibu


Watu katika siku za nabii Mika walilalamika kwamba Mungu hakuridhika kamwe. Wakauliza kwa dharau, “Je, Bwana atafurahishwa na kondoo dume elfu, au mito elfu kumi ya mafuta?” (Mika 6:7). Ilikua njia yao ya kuuliza, “hata hivyo, Mungu anataka nini kutoka kwetu? Baadhi ya watu hii leo wanahisi kwamba jitihada zao zote za kumpendeza Mungu zinaambulia patupu, na wao pia huuliza, ”Mungu anataka nini kutoka kwangu?”

Yesu aliulizwa wakati mmoja kuhusu ni amri gani ya sheria iliyokuwa kuu zaidi. Akajibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.’ Ya pili ndiyo hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi” (Marko 12:30-32; ona pia Mathayo 22:27-39). Kile ambacho Mungu anataka ni rahisi sana: Anatutaka sisi. Huduma zetu zote kwa Mungu lazima zitiririke kutoka kwa amri hizo mbili za kupenda, kama sivyo, huduma sio halisi; ni juhudi za kimwili. Na Warumi 8:8 husema kwamba wale walio “katika mwili hawawezi kumpenda Mungu.”

Kwanza, Mungu anataka tumwamini Mwanawe kama Mwokozi na Bwana (Wafilipi 2:9-11). Petro wa Pili 3:9 inasame, “Bwana... Badala yake, yeye anawavumilia ninyi, maana hataki mtu yeyote aangamie, bali kila mtu afikilie toba.” Tunamjua Yesu kwa kutubu dhambi zetu na kumkubali kama dhabihu yetu binafsi (Warumi 10:9; Yohana 1:12). Wanafunzi wa Yesu walipomuuliza awaonyeshe Baba, alijibu, “Mtu yeyote aliyeniona mimi, amemwona Baba” (John 14:9). Mungu anataka tumjue, na tunaweza kumjua Yeye kupitia Yesu.

Kisha, Mungu anataka “tupate kufanana na mfano wa Mwanawe” (Warumi 8:29). Baba anawataka watoto Wake wote wawe kama Yesu. Yeye huleta hali katika maisha yetu ili kutuchonga na kuondoa tabia hizo zenye kasoro ambazo zinatuzuia kuwa watu ambao alitupangia tuwe (Waebrania 12:7; Yakobo 1:12). Kama vile Yesu alivyokuwa mtiifu kwa Baba katika kila jambo, vivyo hivyo lengo la kila mtoto wa Mungu linapaswa kuwa kumtii Baba yetu wa Mbinguni (Yohana 8:29). Petro wa Kwanza 1: 14-15 inasema, “Kama watoto watiifu, msifuate tamaa zenu mbaya wakati mlipoishi kwa ujinga. 15 Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi kuweni watakatifu katika mwenendo wenu wote.”

Watu wengi, kama Mafarisayo katika siku za Yesu, wanajaribu kuweka matendo ya nje kabla ya mabadiliko ya moyo (Luka 11:42). Wanatilia mkazo wote katika kile wanachofanya badala ya kile walicho. Lakini, isipokuwa upendo kwa Mungu ndio msukumo wetu, maonyesho ya nje ya wema yanasababisha kiburi na kufuata sheria. Wala haimpendezi Mungu. Tunapojitoa kabisa kwake, Roho Wake mtakatifu hutuwezesha kumpenda Mungu kikamilifu na kumtumikia kwa nia ifaayo. Huduma ya kweli na utakatifu ni utendakazi wa Roho, utele wa maisha yaliyotolewa kwa utukufu wa Mungu. Wakati lengo letu ni kumpenda Mungu badala ya kumtumikia tu, tunaishia kufanya yote mawili. Ikiwa tunakiuka uhusiano, hudumua yetu sio ya maana tena na haifaidi chochote (1 Wakorintho 13:1-2).

Nabii Mika alijibu malalamiko ya Waisraeli kwamba hawakujua kile Mungu alihitaji kutoka kwao. Nabii anasema, “Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu. Bwana anataka nini kwako? Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako” (Mika 6:8). Nia ya Mungu kwetu ni rahisi sana. Watu huchanganya mambo, wakizingatia sheria zilizotungwa na wanadamu ambazo huhakikisha kufadhaika nakuua furaha katika kumfuata Kristo (2 Wakorintho 3:6). Mungu anataka tumpende kwa mioyo yetu yote na kuruhusu utiifu wetu utoke katika tamaa ya moyoni ya kutaka kuwa wa kupendeza machoni Pake.

Daudi alielewa kile ambacho Mungu alitaka wakati aliomba, “Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningaliileta, hufurahii sadaka za kuteketezwa. Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika,moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau” (Zaburi 51:16-17).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mungu anahitaji nini kutoka kwangu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries