settings icon
share icon
Swali

Mungu anafananaje?

Jibu


Katika historia, Kila tamaduni imekuwa na wazo fulani kuhusu jinsi Mungu alivyo.Wengine wnadhania kuwa Mungu anadhibiti hali ya anga na wakaunda sanamu za mungu wa dhoruba anayesababisha umeme (ibada ya baali kule Kanaani). Wengine wanafikiri kwamba Mungu ni mwenye nguvu sana na kwa hivyo waliabudu kitu chenye nguvu walichoona ambacho ni jua (ibada ya Ra huko kule Misri). Wengine wanafikiri kuwa Mungu yuko kila mahali na kwa hivyo wameabudu kila kitu(ibada ya miungu katika falsafa ya Stoiki). Wengine wanafikiri kuwa Mungu hafahamiki na wamegeukia kutoamini ili kufunika msingi wa tu, basi wameabudu "Mungu asiyejulikana" (Matendo ya Mitume 17:23).

Tatizo katika dhana hizi ni kwamba wanapata picha isiyokamilifu kuhusu Mungu. Ndio, Mungu anadhibiti hali ya anga, lakini pia anadhibiti mengi zaidi. Yeye nini mwenye nguvu, ana nguvu zaidi kuliko jua. Yeye yuko kila mahali na anapita kila kitu. Ingawa kuna mambo hatuelewi juu ya Mungu, tunashukuru kwa kuwa anajulikana. Kwa kweli, ameweka wazi kila kitu tunachohitaji kujua kumuhusu yeye katika Biblia. Mungu anataka kujulikana (Zaburi 46:10).

Norman Geisler na Frank Turek wana wanasema yafuatayo, katika kitabu chao I Don't Have Enough Faith to Be an Atheist:

• Ukweli unagunduliwa wala sio kubuniwa. Unapatikana huru pasipo na ujuzi wa mtu yeyote. Uzito ulikuwepo kabla ya Newton).

• Ukweli niwa kitamaduni; ikiwa kitu ni kweli basi ni kweli kwa kila mtu, kila mahali, kila wakati. (2+2=4 kwa kila mtu, kila mahali, kila wakati.

• Ukweli haubadiliki hata ikiwa imani yetu kuhusu ukweli inabadilika. (Tulipoanza kuamini kwamba dunia ni mviringo na sio tambarare, ukweli kuhusu dunia haukubadilika, ila tu Imani yetu ndiyo iliyobadilika kuhusu dunia.

Kwa hivyo, tunapojaribu kujua jinsi Mungu alivyo, tunajaribu kugundua ukweli ambao upo tayari.

Kwanza, Mungu yupo. Biblia kamwe haibishani kuhusu uwepo wa Mungu bali inasema tu. Ukweli ni kwamba Mungu anajidhihirisha kupitia kazi ambazo ameumba. (Zaburi 19:1-6). Mwanzo 1:1 inasema, "hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia." Haya ni maneno rahisi lakini yenye nguvu. Ulimwengu ni pamoja na wakati, nafasi, kitu chochote na umeme, kwa hivyo vitu vyote vinavyoonekana katika ulimwengu vilifanyika kwa amri ya Mungu. Nadharia yake Albert Einstein ya marejeleo ya jumla inasema kwamba kila wakati, nafasi, na kitu chochote kilikuwa na mwanzo dhahiri katika wakati mmoja. Kilicho na mwanzo kina sababu. Hiyo ndiyo sheria ya udhuru na ukweli kwamba Mungu anaelezea sababu yake kwa urahisi. Mungu ndiye muumba wa vyote, kwa hivyo tunapata kujua kitu kingine kumuhusu. Yeye ni Mwenyezi (Yoeli 1:15), Yeye anaishi milele (Zaburi 90:2), na Yeye yuko juu na zaidi ya uumbaji wote (Zaburi97:9).

Mungu yule yule aliyeumba vitu vyote pia anadhibiti vitu hivyo. Yeye ni juu ya vyote (Isaya 46:10). Yule anayeunda kitu anakimiliki na anaweza kukitumia jinsi anavyoona inafaa. Kinacho sababisha kitu basi kina mamlaka ya mwisho. Katika Isaya 44:24 Mungu anajidhihirisha kuwa ambaye "ameumba kila kitu, ambaye pekee alieneza mbingu, ambaye alieneza dunia peke yake." Mstari unaofuata unasema kuwa "anarudisha nyuma wenye hekima na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga."(Isaya 44:25). Huyu ni Mungu mwenye nguvu ya kufanya apendavyo.

Mungu ni roho (Yohana 4:24) na hawezi kuwakilishwa na kitu chochote kilichoumbwa; Kwa kweli, jaribio la kuunda uwakilishi huo ni kufuru (kutoka 20:4-6). Mungu habadiliki (Malaki 3:6). Mungu anajua yote (1Yohana 3:20) na yupo kila wakati (Zaburi 139:7-13). Yeye ni mtakatifu na mtukufu (Isaya 6:3). Yeye ni mwenye haki (Kumbukumbu la Torati) na atahukumu dhambi na udhalimu kwa haki (Yuda 1:15).

Hukumu ya Mungu inaonyesha ukweli mwingine kuhusu jinsi alivyo: Yeye ni mwenye maadili. C. S. Lewis, katika Mere Christianity, anafanya kesi kwamba, jinsi ambavyo kuna sheria inayowekwa ya asili (mvuto, nguvu na kadhalika) pia kuna sheria za maadili zinazowekwa. Anaandika, "Kwanza, kwamba wanadamu ulimwenguni kote wana wazo kwamba wanapaswa kuishi kwa njia fulani, na hawawezi kuliondoa. Pili, kwamba kwa kweli hawaishi hivyo. Wanajua sheria ya Asili; na wanaivunja. Ukweli huu ndio msingi wa mawazo yote wazi kutuhusu na ulimwengu tunaoishi." Ingawa kuna maoni tofauti kuhusu ni nini haswa ni haki na mbaya, kuna Imani ambayo ni sawa ulimwenguni kwamba haki na mbaya zipo, na hii ni onyesho la Mungu aliyetuumba (Mwanzo 1:26; Mhubiri 3:11).

Wakati Yesu aliingia ulimwenguni, Alituonyesha Baba (Yohana 14:7-9). Kupitia kwake Yesu, tunaelewa kuwa Mungu anatafuta kuwaokoa waliopotea (Luka 19: 10). Yeye ni mwenye huruma (Mathayo 14:14), Yeye ni mwenye rehema (Luka 6:36), na Yeye husamehe (Mathayo 9:1-8). Wakati huo huo, Yesu anatuonyesha kuwa Mungu atahukumu dhambi ambayo haina toba (Luka 13:5) na kwamba Mungu hukasirika na wanaoishi kwa uongo na wanaokataa kukubali ukweli (Mathayp 23).

Zaidi ya yote, Yesu alituonyesha kwamba Mungu ni upendo ( 1 Yohana 4:8). Ni kwa upendo kwamba Mungu alimtuma Mwanawe ulimwenguni (Yohana 3:16). Ilikuwa kwa upendo kwamba Yesu alikufa msalabani kwa sababu ya wenye dhambi (Warumi 5:8). Ni kwa upendo kwamba Yeye huita wenye dhambi watubu ili wapate neema ya Mungu na kuitwa wana wa Mungu ( 1 John 3:1).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mungu anafananaje?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries