settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu huchukia talaka?

Jibu


Malaki 2:16 ni kifungu kinachonukuliwa sana kinachoelezea jinsi Mungu anavyohisi kuhusu talaka. "'Ninachukia talaka,' asema Bwana Mungu wa Israeli." Lakini kifungu hiki kinasema mengi zaidi kuliko hayo. Ikiwa tunarudi hadi mstari wa 13, tunasoma, "mnaifunikiza madhabahu ya Bwana kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia. Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, ingawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako. Je! Hakuwafanya kuwa mwili mmoja, na sehemu ya Roho katika muunganiko? Na ni nini Mungu alikuwa anatafuta? Mzao mwenye kumcha Mungu. Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana"

Tunajifunza mambo kadhaa kutoka kifungu hiki. Kwanza, Mungu hasikilizi maombi ya baraka kutoka kwa wale ambao wamevunja agano la ndoa. Waraka Wa Kwanza wa Petro 3: 7 inasema, "Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe" (msisitizo aliongezwa). Kuna uwiano wa moja kwa moja kati ya njia ambazo mtu anamtendea mke wake na ufanisi wa sala zake.

Mungu anaelezea wazi sababu zake za kuheshimu ndoa sana. Anasema kuwa ni Yeye ambaye "aliwafanya kuwa mwili mmoja" (Malaki 2:15). Ndoa ilikuwa wazo la Mungu. Ikiwa Yeye ameiumba, basi anapata kufafanua. Kupotoka yoyote kutoka kwa mpango wake ni chuki kwake. Ndoa si mkataba; ni agano. Talaka huharibu dhana nzima ya agano ambalo ni muhimu sana kwa Mungu.

Katika Biblia, mara nyingi Mungu hutoa mifano kwa kufundisha mambo ya kiroho. Wakati Ibrahimu alipomtoa mwanawe Isaka juu ya madhabahu, ilikuwa ni picha ya wakati huo, mamia ya miaka baadaye, kwamba Bwana Mungu atamtoa Mwanawe wa pekee (Mwanzo 22: 9; Warumi 8:32). Wakati Mungu alihitaji dhabihu za damu kwa ajili ya msamaha wa dhambi, alikuwa anachora picha ya sadaka kamili ambayo Yeye mwenyewe angefanya msalabani (Waebrania 10:10).

Ndoa ni picha ya agano ambalo Mungu analo na watu wake (Waebrania 9:15). Agano ni ahadi isiyoweza kuvunjwa, na Mungu anataka sisi tuelewe jinsi anavyotilia maanani. Tunapomtaliki mtu ambaye tulifanya agano naye, inaleta dhihaka kwa dhana ya Mungu ya uhusiano wa agano. Kanisa (wale watu ambao wamempokea Yesu kama Mwokozi na Bwana) wameakilishwa katika Maandiko kama "Bibi arusi wa Kristo" (2 Wakorintho 11: 2; Ufunuo 19: 7-9). Sisi, kama watu wake, "tumeolewa" kwake kwa njia ya agano aliloweka. Mfano sawa unatumiwa katika Isaya 54: 5 wa Mungu na Israeli.

Wakati Mungu alianzisha ndoa katika bustani ya Edeni, aliiumba kama picha ili wanadamu wengi waweze kujua umoja (Mwanzo 2:24). Alitaka sisi kuelewa umoja tunaoweza kuwa nao pamoja kupitia ukombozi (1 Wakorintho 6:17). Wakati mume au mke anachagua kukiuka agano hilo la ndoa, anaasi picha ya agano la Mungu nasi.

Malaki 2:15 inatupa sababu nyingine ambayo Mungu huchukia talaka. Anasema ana "tafuta uzao wa kiungu." Mpango wa Mungu kwa familia ulikuwa kwamba mume mmoja na mwanamke mmoja kujitolea wao kwa wao maishani mwao kulea watoto ili waelewa dhana ya agano pia. Watoto waliolelewa katika masingara mazuri, wakiwa wazazi wawili wa nyumbani wana uwezekano mkubwa zaidi wa kuanzisha ndoa yenye mafanikio wenyewe.

Wakati Yesu aliulizwa kwa nini Sheria iliruhusu talaka, alijibu kuwa Mungu aliiruhusu tu "kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo" (Mathayo 19: 8). Mungu hakutaka talaka kuwa sehemu ya uzoefu wa kibinadamu, na humuumiza wakati tunapofanya mioyo yetu ngumu na kuvunja agano aliloliumba.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu huchukia talaka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries