settings icon
share icon
Swali

Je! Mungu ako na hisia?

Jibu


Kuna vifungu vyingi vya maandiko ambavyo vinasungumzia huu ya hisia za Mungu. Kwa mfano, Mungu alionyesha yafuatayo:
• Ghadhabu-Zaburi 7:11; Kumbukumbu 9:22; Warumi 1:18
• Huruma- Zaburi 135:14; Waamuzi 2:18; Kumbukumbu 32:36
• Sikitiko- Mwanzo 6:6; Zaburi 78:40
• Upendo- 1Yohana 4:8; Yohana 3:16; Yeremia 31:3
• Chuki- Mithali 6:16; Zaburi 5:5; Zaburi 11:5
• Wivu- Kutoka 20:5; Kutoka 34:14; Yoshua 24:19
• Furaha- Zefania 3:17; Isaya 62:5; Yeremia 32:41

Walakini, je! hisia za Mungu ni sawia na hisia tunazodhihirisha? Ni vyema kumfikiria kuwa wa ''hisia" (je! Yeye huwa na mhemko unaobadilika badilika)? Katika makundi ya theolojia, nafsi mara nyingi hufafanuliwa kuwa ''hali ya kuwa mtu mwenye ufahamu, hisia, na hiari." Mungu, basi ni "nafsi" kiasi kwamba ni Mungu mwenye nafsi, akili, hisia, na hiari yake mwenyewe. Kukataa hisia za Mungu kukana kuwa hana nafsi.

Wanadamu huitikia mambo katika dunia hii kwa njia ya kimwili, ijapokuwa sisi huitikia kwa njia ya kiroho-nyoyo huchukua hatua na hii ndio tunaita "hisia." Kuwepo kwa hisia za binadamu ni dhibitisho kuwa Mungu ana hasia vile vile, kwa kuwa alituumba kwa mfano wake (Mwanzo 1:27). Dhibitisho lingine ni katika utwaaji utu. Kama mwana wa Mungu katika ulimwengu huu, Yesu hakuwa mwenye hana hisia. Alihisi kile tunachokihisi, aliomboleza na wale waliomboleza (Yohana 11:35), alihisi huruma kwa umati (Marko 6:34), akijawa na huzuni (Mathayo 26:38). Kupitia yote alimfunua Baba kwetu (Yohan 14:9).

Ingawa Mungu anapita fahamu zote, tumekuja kumtambua kama nafsi, Mungu aishiye ambaye anahusiana kwa karibu viumber Wake. Anatupenda njia ambazo hatuwezi kufikiria (Yeremia 31:3; Warumi 5:8; 8:35, 38-39), na hasa Yeye uhumizwa na dhambi zetu na uasi wetu dhidi yake (Zaburi 1:5; 5:4-5; Mithali 6:16-19).

Tunatambua kuwa dhihirisho la hisia hazibadilishi kutoharibika na kudumu kwa mapenzi ya Mungu au ahadi Zake. Kwa maneno mengine, Mungu habadiliki (Malaki 3:6; Hesabu 23:19; 1Samueli 15:29); hana mhemko wa kubadilika. Hisia za Mungu na hatua Zake kwa viumbe wake, hukumu Yake na msamaha, haki Yake na neema, zote zinaambatana na jinsi alivyo (Yakobo 1:17). Itikio la Mungu kwa mema na mabaya hutoka katika hiari Yake isiyogeuka. Mungu hawezi hukumu na kumwadhibu mwenye dhambi ili adhihirishe haki, sawia na kumleta mwenye dhambi katika toba kwa sababu Yeye anataka watu wote waokolewe (1Timotheo 2:4). Tumekuja kumjua Mung una kuhusiana Naye kama watu wenye hisia, watu tuanopenda na kuchukia, huzunika na kucheka, kuhisi ghadhabu na huruma. Anawapenda wanye haki na kuchukia waovu (Zaburi 11:5-7; 5:4-5; 21:8).

Hii haimaniishi kuwa ninasema kwamba hisia zetu na zile za Mungu ziko sawia. Wakati mwingine tunasungumzia hisia zetu sawia na uamuzi wetu kwa sababu hali yetu ya dhambi imeharibu hisia zetu. Lakini Mungu hana dhambi, na hisia Zake haziharibiwe na chochote. Kwa mfano tofauti kubwa kati ya ghadhabu ya uanadamu na ghadhabu ya kiungu. Ghadhabu ya uanadamu ni badilifu, iko chini na kila mara nyingi iko mbali na kudhibitiwa (Mithali 14:29; 15:18; Yakobo 1:20). Ghadhabu ya Mungu imekita mizizi katika haki ya kiungu. Ghadhabu ya Mungu ni ya haki na ya kubashirika, na kamwe si badilifu au ya korofi. Katika ghadhabu yake kamwe hatendi dhambi.

Hisia zote za Mungu zimekita mizizi katika hali yake takatifu na kila mara zinajidhihirisha kuwa bila dhambi. Huruma ya Mungu, huzuni, na furaha kikamilifu zote zinadhihirisha Kiumbe kamilifu. Ghadhabu ya Yesu kwa viongozi wa hekalu katika Marko 3:5 na upendo Wake kwa mtawala tajiri katika Marko 10:21 kikamilifu zote itikio la hali yake ya kiungu.

Njia za Mungu nyakati zote zimeandikwa kwa ajili yetu katika njia tunayoweza kuelewa na kuhusiana nazo. Ghadhabu ya Mungu na hasira Yake dhidi ya dhambi ni za kweli (Mithali 8:13; 15:9). Na huruma Yake kwa wenye dhambi ni dhabiti nay a kweli (2Petro 3:9; Mhubiri 8:11; Isaya 30:18). Kazi zake zinadhihirisha huruma na nehema isiyo na mwisho. Lakini zaidi ya yote, upendo Wake kwa watoto wake hauna mwisho (yeremia 31:3) na hautingiziki (Warumi 8:35, 38-39). Mungu hana mawazo na mipango pekee; ako na hisia na nia pia. Kinyume na kutoaminika na kutokamilika kwa hisia za mwanadamu zilizotiwa doha na dhambi, hisia za Mungu Mungu zinaaminika na hazigeuki jinsi na namna Yeye hageuki.

Kuna mambo mawili ya ajabu kuhusu Mung una hisia: kwanza, anaelewa hisia zetu (tangu ni Yeye alituumba na uwezo wa kuzihisi), na pili, hisia Zake mwenyewe kamwe hujibuka toka ukamilifu Wake. Kamwe Mungu hatakuwa na siku mbaya; hatabadilisha hisia zake kwa wale wake waliokombolewa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mungu ako na hisia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries