settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Mungu anamruhusu Shetani atushambulie?

Jibu


Mashambulizi ya Shetani dhidi yetu huja kwa aina mbalimbali. 1) Anatumia dunia isiyo ya Mungu (ambayo anaiongoza, 1 Yohana 5:19) ili kuchochea tamaa za mwili ndani yetu ambazo zinatujaribu kutenda dhambi. 2) Anatumia ulimwengu usioamini kujaribu kutudanganya na "hekima" ya kidunia inayopingana na ukweli wa Mungu. 3) Anatumia Wakristo wa uwongo kujaribu kutupoteza katika injili ya uwongo inayomhusu Yesu wa uongo. 4) Wakati mwingine kimwili hutuumiza sisi au wapendwa wetu kwa ugonjwa, uhalifu, msiba, au mateso. Tukijua kwamba Mungu ndiye Mtawala wa ulimwengu wote, kwa kawaida tunauliza, kwa nini Mungu anaruhusu Shetani kutushambulia kwa njia hizi?

Biblia inafundisha kwamba Mungu anamruhusu Shetani kuwa na uhuru fulani (angalia Ayubu 1:12), lakini uhuru huo ni mdogo. Shetani hawezi kufanya yote anayotaka. Shetani anachagua kushambulia watoto wa Mungu (angalia 1 Petro 5: 8), na mpango wake daima ni mabaya; Shetani ni mwuaji (Yohana 8:44). Kwa ulinganisho, mpango wa Mungu kwa kuruhusu mashambulizi fulani ya Shetani daima ni mwema; Mungu anawapenda watoto wake (1 Yohana 4:16). Yusufu alikabiliwa na mashambulizi mengi ya Shetani katika maisha yake, lakini hatimaye angeweza kusema kwa ujasiri madhumuni mawili yanapingana na matukio hayo: "Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema" (Mwanzo 50:20).

Hatuwezi kumlaumu Mungu kwa kile Shetani anachofanya. Hatari yetu ya mashambulizi ya Shetani ilianza na uchaguzi wa Adamu kufuata mapendekezo ya uongo ya Shetani katika bustani mwa Edeni. Wakati Shetani alimshinda Ayubu kwa kupoteza familia yake, utajiri, na afya, Ayubu hakumlaumu Mungu. Angalia Ayubu 1: 21-22, "akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe. Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu."

Waumini wanapokumbana na mashambulizi ya Shetani, wanaweza kuamini ukweli wa Warumi 8:28, " Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao..." Kwa hiyo, dhana ni kwamba tutapata mambo "mema" na "mambo mabaya", lakini "yote" ya mambo haya yanaweza kufanywa kuchangia kuelekea mwisho "mwema" kadri na vile Mungu anafanya kazi. Kwa hivyo hata kama mashambulizi ya Shetani ni mabaya, hatimaye yanaweza na yatakuwa na "matokeo mazuri", kadri na vile Mungu anavyoyatumia ili atufananishe na Kristo, Mwanawe (angalia Waroma 8:29). Mashambulizi kutoka kwa Shetani, pamoja na mateso mengine yote, yanaweza kusababisha waumini kumpenda Mungu zaidi, kumpinga Shetani zaidi, kujitahidi kwa uvumilivu, na kukua imara katika imani yetu kwa njia nyingine nyingi. Asifiwe Mungu kwa ajili ya ulinzi wake mkuu. Mshukuru kwa mpango wake wa kufanya kila kitu-hata mashambulizi ya Shetani- "hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema" hat kwako!

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Mungu anamruhusu Shetani atushambulie?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries