Je! Mungu aliumba watu wengine Zaidi ya Adamu na Hawa?


Swali: "Je! Mungu aliumba watu wengine Zaidi ya Adamu na Hawa?"

Jibu:
Hakuna dalili yoyote katika Biblia inayoonyesha kwamba Mungu aliumba binadamu yeyote isipokuwa Adamu na Hawa. Katika Mwanzo 2 tunasoma, "Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi, hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi; ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi. Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya... Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. '... Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu" (Mwanzo 2: 4-8, 18, 21-22).

Angalia kile kifungu hiki kinasema kwamba, "Hapo alimweka mtu ambaye alikuwa amemuumba." Sio "wanadamu," bali "mtu" mmoja tu. Na mtu huyu alikuwa peke yake (mstari wa 18) hivyo Mungu alimfanya mwanamke kutok umbavuni mwake kuwa rafiki yake. Watu wengine wote wametoka kwa watu hawa wawili wa awali.

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mungu aliumba watu wengine Zaidi ya Adamu na Hawa?

Jua jinsi ya ...

kutumia milele na MunguPata msamaha kutoka kwa Mungu