settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Mungu anaumba watu wakati Anajua kwamba watenda jahanamu/kuzumuni?

Jibu


Tafadhali elewa kwamba Mungu hamsababishi mtu yeyote kwenda kuzimuni. Badala yake, mwanadamu anachagua yeye mwenyewe kwenda huko. Unaweza kuona vile wanaendelea wale ambao wanamkataa Yesu katika milango mitatu ya kwanza ya kitabu cha Warumi. Ghadhabu ya Mungu imefunuliwa dhidi ya wasio wenye haki kwa sababu mwanadamu anamkataa Muumbaji na kuabudu viumbe (Warumi 1:18-20). Mwanadamu anadai kuwa mwenye hekima mbele ya macho yao (Warumi 1:22) na kubadilisha utukufu wa Mungu kwa sanamu (Warumi 1:23-25). Watu hawa basi wanaendelea katika hali dhaifu ya dhambi ambayo imetajwa katika Warumi 1:28-31, dhambi ambazo sisi wote tunasijua. Hawajishughulishi na hisi dhambi tu pekee, bali wanawapa kongole wale wanaozitenda pia (Warumi 1:32). Wanadamu hawana ulimwengu pekee ili waone nguvu za Mungu, lakini pia wana nia ambayo inawahukumu kwa dhambi zao (Warumi 2:14-15). Mwishowe, watu wameachwa bila sababu. Tunapaswa kufa kwa ajili ya dhambi zetu, na mbele za Mungu tunabaki kuhukumiwa.

Yesu Kristo alikuja katika mwili ili "mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake" (Yohana 20:31). Huu ni Ushahidi mwingine wa kuwepo kwa Mungu na pia unabaki ukiwahukumu wale wanaoamua kumkataa Kristo kama Mwana wa Mungu. Kwa sababu Kristo alikuja kulipa dhamana ya dhambi, alikuja ili amfanye Baba kujulikana (Yohana 1:18), watu hawana sababu ya kumkataa. Watu huamua kwenda kuzimuni kwa sababu ya kumkataa Kristo, sio ni kwa sababu ya Mungu kuwafanya kwenda huko. Mungu amekwisha lipa gharama, amejidhihirisha Mwenyewe kwa wote na sasa wanadamu "hawana sababu" (Warumi 1:20. Mungu anawaruhusu watu kuzaliwa ili awape fursa ya kuamini, lakini ni jukumu la mtu kufanya uamuzi huo. Atakuwa Mungu wa aina gani ikiwa hangewapatia watu fursa ya kuweka Imani yao kwa Bwana?

Bado kunayo dhana ngumu sana kuilewa. Tunaweza kushikilia tu chenye tunafahamu kuhusu asili ya Mungu na sifa zake, tukiamini kuwa uweza wake na hurama haviwezi kanganyana, na kuumini kuwa kila kitu afanyacho/anaruhusu hatimaye itakuwa kwa utukufu wake. Tunajitoa kwake kwa kuabudu na utiifu na kuamini kuwa Yeye "hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake" (Waefeso 1:11) na kuwa njia zake ni kamilifu, hata wakati hatuzielewi. "Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili" (Kumbukumbu 32:4).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Mungu anaumba watu wakati Anajua kwamba watenda jahanamu/kuzumuni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries