settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu alituumba?

Jibu


Jibu fupi kwa swali "Kwa nini Mungu alituumba?" ni "kwa radhi yake." Ufunuo 4:11 inasema, "Umestahili wewe, Bwana na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza, kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa." Wakolosai 1:16 yarudia dhan hiyo: " vitu vyote viliumbwa wa njia yake na kwa ajili yake" kuumbwa kwa furaha ya Mungu haimaanishi kwamba mwanadamu aliumbwa kumtumbuiza Mungu au kumpatia pumbao. Mungu ni kiumbe bunifu, na inaleta radhi kwake kwa kuumba. Mungu ni kiumbe binafsi, na inampa radhi kwa kuwa na viumbe wengine Yeye anaweza kuwa na uhusiano wa kweli nao.

viumbe walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27), binadamu ana uwezo wa kumjua Mungu na hivyo kumpenda, kumwabudu, kumtumikia, na kuwa na ushirika naye. Mungu hakuumba binadamu kwa sababu alimwihitaji. Kama Mungu, Yeye ahitaji kitu chochote. Katika milele yote iliyopita, Yeye hakuishi upweke, hivyo hakuwa anatafuta "rafiki." Yeye anatupenda, lakini hatuitaji sisi. Kama hatungekuwepo kamwe, Mungu bado angebaki kuwa Mungu - asiyebadilika (Malaki 3:6). MIMI NIKO AMBAYE NIKO (Kutoka 3:14) kamwe hakuchoka kuridhika kuwepo kwake milele. Wakati Yeye aliumba ulimwengu, alifanya mambo yanayompendeza mwenyewe, na tangu Mungu yu kamilifu, hatua yake ilikuwa kamilifu. "Ilikuwa ni nzuri sana" (Mwanzo 1:31).

Pia, Mungu hakuumba "rika" au viumbe sawa na yeye mwenyewe. Kimantiki, hangeweza kufanya hivyo. Kama Mungu angekuwa anaumba mwanadamu mwingine kuwa na mamlaka sawia, akili, na ukamilifu, basi angekoma kuwa Mungu mmoja wa kweli kwa sababu rahisi kwamba kutakuwa na miungu wawili na hiyo haingewezekana. "Bwana ni Mungu; badala yake hakuna mwingine" (Kumbukumbu 4:35). Chochote ambacho Mungu aliumba hakina budi kuwa nguvu kumliko Yeye. Kilichoumbwa hakiwezi kuwa kuu kumliko, au kubwa kama yule aliyemuumba.

Kutambua uhuru kamili na utakatifu wa Mungu, sisi hushangaa kwamba angeweza kuchukua mwanadamu na kumvika taji yake "utukufu na heshima" (Zaburi 8:5) na kwamba anaweza tosheka kutuita "rafiki" zake (Yohana 15:14-15). Kwa nini Mungu alituumba? Mungu alituumba kwa ajili ya radhi yake na hivyo sisi, kama viumbe wake, tuwe na furaha ya kumjua Yeye.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu alituumba?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries