settings icon
share icon
Swali

Je! Mungu aliumba dhambi?

Jibu


Mungu aliumba ulimwngu katika siku sita, lakini mbeleni ulimwngu haukuwa na dhambi-kila kitu alichokiumba "kilikuwa kizuri" (Mwanzo 1:31). Dhambi iliingia ulimwenguni kwa sababu ya tendo la kuasi dhidi ya Mungu, sio eti ni kwa sababu Mungu aliumba dhambi.

Tunafaa kufafanua "dhambi." Yohana wa Kwanza 3:4 yasema, "Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi." Kwa hivyo dhambi ni uasi dhidi ya sheria takatifu ya Mungu. Warumi 3:23 yasema, "kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu." Kulingana na ayah ii, dhambi ni chochote iwe (maneno, fikira, matendo au motisha) ambayo haifikii ukuu na ukamilifu wa Mungu. Sisi wote hutenda dhambi. Warumi 3:23 pia inatufunza kwamba ni lazima tuijue tabia ya Mungu kubla tuweze kufafanua kifasaa dhambi ni nini, kwa sababu utukufu wake ndio kigezo ambacho tunatumia kupima (Zaburi 119:160; Yohana 17:17). Bila kigezo dhabiti, hakuna njia nyingine tunaweza kutadhimini ubora/ukamilifu wa kitu. Bila kigezo kikuu cha utukufu wa Mungu, kila neno au tendo litahukumiwa kwa kosa lake, vigezo hafifu vya watu wasio wakamilifu. Kila amri, sheria na maadili ya kijamii zitakua maoni tu. Na maoni ya mwadamu huwa tofauti na hubadilika kama vile hali ya anga.

Ikiwa mjenzi atajenga juu msingi ambao si dhabiti, anahatarisha udhabiti wa mradi mzima. Jengo haliwezi kuwa bora linapoendelea kwenda juu; linaendelea kuwa hafifu kuenda kombo. Walakini, ikiwa mwanzo wa ujenzi huo ni kamilifu, basi muundo wote utakuwa bora. Misingi ya maadili hufanya kazi vivyo hivyo. Bila sheria ya Mungu ya maadili hatuna njia nyingine ya kujua uzuri na ubaya. Dhambi ni kuenenda mbali na ukweli. Tunaposonga mbali zaidi kutoka kwa vigwango vya maadili vya Mungu ndivyo dhambi inazidi kuwa mbaya zaidi.

Mungu aliwaumba wanadamu na malaika na uhuru wa hiari, ikiwa kiumbe ako n uhuru wa hiari, basi kuna uwezekano atafanya uamuzi mbaya. Mungu aliwaumba wanadamu kwa mfano wake, na jinzi alivyo huru, wanadamu waliumbwa na uhuru pia (Mwanzo 1:27). Hiari huru inahuzisha uwezo wa kuchagua na baada ya Mungu kusungumza viwango vya maadili, alimpa mwanadamu chaguo la kweli (Mwanzo 2:16-17). Adamu alichagua uasi. Mungu hakumjaribu, lazimisha, au kumshawishi Adamu kuasi. Yakobo 1:13 yasema, "Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu." Mungu alimruhusu Adamu kuwa na uhuru wa kuchagua na akiheshimu chaguo hilo kwa madhara ya kadri (Warumi 5:12).

Mungu aliruhusu nafasi ya kufanya dhambi, lakini hakuiumba dhambi wala kuianzisha. Kuwa na nafasi ilikua wakati mwafaka, pasinge kuwa nayo, mwanadamu angekuwa kiumbe kilichotumika kama mfano. Mungu huamrisha, anasihi, na kututia motisha ya kumfuata (Kutoka 19:5; Kumbukumbu 12:28; 1Samweli 15:22). Anaahidi baraka, ushirika, na ulinzi wakati tunamtii (Yeremia 7:23; Zaburi 115:11; Luka 11:28). Lakini hatufungi minyororo. Mungu hakuweka ua kando ya lile tunda walilokatazwa bustani mwa Edeni. Adam una Hawa walikuwa na uhuru wa kuchagua kutii au kutotii. Wakati walichagua dhambi walichagua madhara pia ambayo yaliambatana nayo (Mwanzo 3:16-24).

Hiyo imekuwa hivyo kwa kila mwanadamu tangu enzi hizo. Fursa ya kufanya dhambi ii ndani ya uhuru wetu wa uamuzi. Tunaweza chagua kumtafuta Mungu, ambayo itaongoza hadi maisha matakatifu (Yeremia 29:13; 2Timothy 2:19). Au tunaweza amua kuifuata mapendeleo yetu, ambayo huongoza mbali na Mungu (Mithali 16:5). Biblia ii wazi, njia yoyote ile tutakayo fuata ina madhara. Tunavuna chenye tunapanda (Wagalatia 6:7). Baadhi ya madhara huwa ya milele. Matayo 25:46 inasema kuwa wale ambao hawatamfuata Yesu, "Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele."

Mungu ndiye uhukumu watu (Mhubiri 12:14) na mataifa (Mika 5:15) ambayo hutumia hiari yao huru kuasi Mungu. Mungu hakuumba na haumbi dhambi, wala hapendelei kuwaadhibu wale huchagua dhambi (Ezekieli 33:11). Kusudio lake ni kuwa wote waje katika toba na kushiriki baraka na furaha ya maisha ya milele pamoja naye (2Petro 3:9).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mungu aliumba dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries