settings icon
share icon
Swali

Mungu alikuwa anafanya nini kabla aumbe ulimwengu?

Jibu


Akili zetu zilizo na mwisho huipata ngumu kufukiria kuwa kabla ya ulimwengu kuumbwa Mungu aliishi peke yake. Kutoka Yohan 1:1 tunajua kwamba Yesu pia alikuwepo: "Hapo mwanzo, Neno alikuwako; naye alikuwa na Mungu, naye alikuwa Mungu." Kristo mwili alikuwa ameungania na Baba, ndio aweze kushiriki utukufu wake na ndio aweze kuitwa Mungu. Yeye mwenyewe amefafanua hilo katika Yohana 17:5: "Sasa, Baba, nitukuze mbele yako kwa ule utukufu niliokuwa nao kabla ya kuumbwa ulimwengu."

Tunajua pia kwamba Roho Mtakatifu alikuwepo kabla tuumbwe. Mwanzo 1:2 inaelezea Roho "ilikuwa ikitanda juu ya maji" giza na nchi isiyo na umbo na ni tupu. Kwa hivyo, kabla ya nyakati kuwepo, Mungu alikuwepo katika utatu: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Utatu ulikuwepo katika upatano kamilifu na bila hitilafu yeyote, na kuwa na yale yote waliohitaji kwa kila moja. Daudi alisema katika Zaburi 16:11, "furaha na mema ya milele" yako katika uwepo wa Mungu. Hiyo inamaanisha kuwa mbele za Mungu ndani yake mna furaha ipitayo kifani, inayotoshelesha na mema. Kabla ya uumbaji, Mungu alihisi furaha kamili na kutosheka kikamilifu alipo shika na kuunganika nay eye. Mungu ana furaha na kila wakati atakuwa nayo kwa sababu ana fahamu kamilifu ya kuwa yeye ni nani.

Kwa hivyo kabla ya kuumba ulimwengu, Mungu alihisi kutosheleka ya kutosha ndani Yake Mwenyewe. Mungu aliishi kwa furaha peke yake katika mile kama Utatu. Hawa watatu walikuwa pamoja katika ushirika na kila mmoja tangu milele. Wote walipendana. Tunajua kwa wakati mmoja walijadiliana kuhusu ukombozi wa mwanadamu (Waefeso 1:4-5; 2 Timotheo 1:9; Yohana 17:24), lakini kila kitu kingine ni siri.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mungu alikuwa anafanya nini kabla aumbe ulimwengu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries