settings icon
share icon
Swali

Adui wa Kristo ni nani?

Jibu


Kuna uvumi mwingi kuhusu utambulisho wa Mpinga Kristo. Baadhi ya malengo maarufu zaidi ni Vladimir Putin, Mahmoud Ahmadinejad, na Papa Benedict XVI. Nchini Marekani, Raisi wa zamani Bill Clinton na George W. Bush, na Raisi wa sasa Barack Obama, ni wagombea mara kwa mara. Hivyo, nani Mpinga Kristo, na jinsi gani sisi humtambua?

Biblia kweli haisemi chochote hasa kuhusu mahali ambapo Mpinga Kristo atakuja toka. Wasomi wengi wa Biblia hubashiri kwamba yeye atakuja kutoka ushirikiano wa mataifa kumi / au kusaliwa upya kwa Dola ya Kirumi (Danieli 7:24-25, Ufunuo 17:7). Wengine humwona kuwa Myahudi ili kudai kuwa Masihi. Hayo yote ni mafikirio tu tangu Biblia haisemi hasa mahali ambapo Mpinga Kristo atakuja toka au atakuwa wa asili gani. Siku moja, Mpinga Kristo atawekwa wazi. Wathesalonike wa pili 2:3-4 inatuambia jinsi sisi tutamtambua Mpinga Kristo: "Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote maan haiji, usipokuja kwanza ule ukengufu, akafunuliwa yle mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu, yule mpingamizi, ajinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa, hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye."

Kuna uwezekano kwamba watu wengi ambao watakuwa hai wakati Mpinga Kristo atafunuliwa wazi watashangazwa sana katika utambulisho wake. Mpinga Kristo anaweza kuwa hai au asiwe hai hii leo. Martin Luther alikuwa ameshawishika kwamba papa katika wakati wake alikuwa Mpinga Kristo. Katika miaka ya 1940, watu wengi waliamini Adolph Hitler alikuwa Mpinga Kristo. Wengine ambao wamekuwa wakiishi katika miaka mia kadhaa iliyopita wameamini sawa na kuwa na uhakika kama utambulisho wa Mpinga Kristo. Hadi sasa, wote wamekuwa sahihi. Tunapaswa kuweka uvumi nyuma na kuzingatia yale ambayo Biblia inasema juu ya Mpinga Kristo. Ufunuo 13:5-8 inasema, "Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia."

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Adui wa Kristo ni nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries