Swali
Mkristo wa kweli ni nini?
Jibu
Kulingana na Matendo 11:26, wafuasi wa Yesu waliitwa Wakristo kwa mara ya kwanza huko Antiokia. Ni kwa nini waliitwa Wakristo? Kwa sababu walikuwa “wafuasi wa Kristo.” Walikuwa wamejitolea maisha yao “kuenenda kama Yesu alivyoenenda” (1 Yohana 2:6).
Maandiko mengine yanaeleza jinsi mtu anapata kuja katika imani na kuanza uhusiano huu. Kwa mfano, Waefeso 2:8-9 inadhihirisha kwamba mtu anakuwa Mkristo kwa imani, sio kwa kufuafa orodha ya kanuni au matendo mema: “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, si kwa matendo, ili mtu yeyote asije akajisifu.” Mkristo wa kweli ana imani katika Yesu kama Mwokozi.
Warumi 10:9-10 inasema “Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba “Yesu ni Bwana,” na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na hivyo kupata wokovu.” Mkristo wa kweli haoni aibu kusema kuwa Yesu ni Bwana na anaamini kuwa Yesu alifufuliwa kutoka kwa wafu.
Wakorintho wa Kwanza 15:3 inasema ujumbe huu wa Yesu aliyefufuliwa ni wa “umuhimu kwanza.” Bila ufufuo wa Yesu imani yetu ni “batili,” na sisi “tungali katika dhambi zetu” (mstari wa 17). Mkristo wa kweli anaishi kwa imani katika Yesu aliyefufuka (1 Wakorintho 15:13-14).
Paulo anaandika, “Mtu yeyote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo… Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kwamba sisi tu watoto wa Mungu” (Warumi 8:9,16). Mkristo wa kweli Roho Mtakatifu wa Mungu anaishi ndani yake.
Uthibitisho wa Mkristo wa kweli unaonyeshwa katika imani na matendo. “Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya” (2 Wakorintho 5:17). Yakobo anasema, “nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo” (Yakobo 2:18). Yesu anaiweka hivi: “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu yeyote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima” (Yohana 8:12). Mkristo wa kweli ataonyesha imani yake kwa jinsi anavyoishi.
Licha ya aina mbalimbali za imani ambazo ziko chini ya lebo ya jumla ya “Mkristo” hii leo, Biblia inafafanua Mkristo wa kweli kuwa aina ya mtu ambaye amempokea Yesu Kristo kibinafsi kama Mwokozi, anayeamini kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo pekee kwa msamaha wa dhambi, ambaye Roho Mtakatifu anakaa ndani yake, na ambaye maisha yake yanadhihirisha mabadiliko sawia na imani yake katika Yesu.
English
Mkristo wa kweli ni nini?