settings icon
share icon
Swali

Je Mkristo anafaa kumwona mwanasaikolojia/mwanataaluma ya magonjwa ya akili?

Jibu


Wanasaikolojia na wanataaluma ya magonjwa ya akili ni maprofesa wanaofanya kazi kwenye nyanja ya afya ya kiakili. Mara nyingi watu huchanganyikiwa majukumu yao ama wanawajumulisha na maprofesa wengine wa afya kama vile wale wa matibabu ya kisaikolojia , wale wa uchunguzi nafsia ,ama washauri wa afya ya kiakili . Kuna haina nyingi ya maprofesa wa afya ya kiakili wanaohitaji njia nyingi tofauti za kielimu na kutumia mbinu nyingi za kutibu. Wanasaikolojia lazima wahitimu shahada ya juu ya Ph.D. kwa saikolojia na walenge kimsingi kwa kufanya utafiti, kufunza kwenye kiwango cha chuo kikuu,na kuhifadhi mazoezi ya ushauri wa kibinafsi . Wanaweza kusimamia upimaji kwa ajili ya wengi kutathmini utambuzi na hisia vile vile. Daktari wa magonjwa ya akili kweli ni mtaalamu katika matatizo ya akili. Wauguzi wa akili ni wataalamu tu wa afya ya akili na wana uwezo wa kuagiza dawa na mafunzo katika matibabu kwa afya ya akili.

Wakati watu huhisi haja kwa ajili ya huduma kama vile kupima kwa kutoweza kusoma vizuri au ushauri nasaha, wanaweza kufikiria kwenda kwa mwanasaikolojia. Kwa kawaida, watu humwaona mwanasaikolojia au mtaalamu wa ushauri nasaha wengine kabla ya wao ni inajulikana magonjwa ya akili. Baadhi ya wahuguzi wa akili hufanya ushauri nasaha, lakini wengine husimamia tu na kufuatilia dawa huku wakishirikiana na wataalamu wengine ambao hutubu. Kama katika wito wowote, baadhi wanasaikolojia / wataalamu wa akili watakuwa Wakristo, na wengine sio.

Wakristo kwa kawaida wanataka kujua jinsi Biblia inahusiana na fani hizi. Ukweli ni kwamba, aidha saikolojia wala utaalamu wa akili ni makosa kwa mjibu wa dhambi. Zote mbili hutumikia madhumuni halali na kusaidia. Hakuna hata mmoja wa wataalamu wa afya ya akili huwa na uwezo wa kuelewa kikamilifu jinsi Mungu alimuumba mtu, jinsi akili inafanya kazi, kwa nini sisi hujihisi na kutenda vile sisi hufanya. Wakati kuna wingi wa udunia, nadharia isingatiayo mwanadamu kuhusu masuala ya akili na hisia, pia kuna watu wengi waja Mungu hushiriki katika fani hizi kutafuta kuelewa akili za binadamu kwa mtazamo wa Biblia. Kwa Wakristo, ni bora kutafuta mtaalamu anayedai kuwa muumini, unaweza kueleza ilimu ya Bibilia, na kuonyesha tabia ya kimungu. Shauri yoyote sisi hupokea lazima kuchujwa kupitia maandiko ili, kama kwa kila kitu katika dunia, tunaweza kutambua ni gani kweli na ni gani ya uongo.

Kuona mwanasaikolojia au muhuguzi wa magonjwa ya akili sio dhambi. Hata hivyo, wataalamu wa afya ya akili hutoka katika imani mbalimbali na asili. Hata wanasaikolojia Wakristo na wataalamu wa akili hawataweza kutoa majibu kamili, au wanaweza kuwa dhaifu katika baadhi ya maeneo ya ujuzi yao ya Biblia. Kumbuka kwamba Neno la Mungu ni jibu letu kwanza kwa yote ambayo yanatugonjesha. Kujikinga sisi wenyewe na silaha ya kweli ni muhimu ili kutambua ni gani nzuri na ni gani la kutuongoza hadi kupotea (Waefeso 6: 11-17; 1 Wakorintho 2: 15-16). Kila muumini kibinafsi anawajibika kwa ajili ya kusoma Biblia kwa ukuaji wake binafsi na utambuzi. Roho Mtakatifu atatumia neno kutubadilisha katika mfano wa Yesu Kristo, ambao ndio lengo la mwisho kwa Wakristo wote (Waefeso 5: 1-2, Wakolosai 3: 3).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je Mkristo anafaa kumwona mwanasaikolojia/mwanataaluma ya magonjwa ya akili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries