settings icon
share icon
Swali

Je! Ni wakati gani Mkristo anapaswa kumrekebisha Mkristo mwingine?

Jibu


Hili linaweza kuwa suala nyeti. Na jambo la busara kutumia muda katika maombi kwanza, kuangalia msukumo wetu na kuomba mwongozo. Kuna nyakati ambapo Wakristo wanaitwa “kuzungumza na” au kujaribu kumrekebisha Mkristo mwenzao. Ichukuliwe kuwa tunazungumza juu ya suala la dhambi katika maisha ya muumini, nia na dhamira yetu inapaswa kuwa ya kuleta toba na urejesho kwa kaka au dada aliyekosea katika Kristo.

Kwanza, nia yetu ni ya muhimu sana. “Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi” (Waefeso 4:32). Hapo ndipo tunapoweza “kuambiana kweli kwa upendo” (Waefeso 4:15). Katika waraka wake kwa Wagalatia, Paulo alikuwa na onyo kama hilo kuhusu nia: “Ndugu zangu, ikiwa mtu ameghafilika akatenda dhambi, basi ninyi mlio wa rohoni, mrejesheni upya mtu huyo kwa roho ya upole. Lakini jihadharini, ili ninyi wenyewe msije mkajaribiwa” (Wagalatia 6:1). Hapa tunaona kwamba wale walio wa “kiroho,” kumaanisha kutembea katika Roho kwa imani na utiivu, wanapaswa kumrejesha kwa upole mtu aliye katika dhambi, tukijua daima jinsi sisi sote tunaweza kujaribiwa kwa urahisi na Shetani ambaye anataka kumnasa kila mtu katika mitego ya dhambi yake.

Biblia inaelezea utaratibu wa kukabiliana na ndugu au dada aliyetenda dhambi katika kifungu cha kina juu ya nidhamu katika kanisa: “Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonyeshe kosa lake, kati yenu ninyi wawili peke yenu. Kama akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako. Lakini kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili ili kila neno lithibitishwe kwa ushahidi wa mashahidi wawili au watatu. Kama akikataa kuwasikiliza hao, liambie kanisa. Naye kama akikataa hata kulisikiliza kanisa, basi awe kwenu kama mtu asiyeamini au mtoza ushuru” (Mathayo 18:15-17). Tena, huu ni utaratibu wa kumkabili ndugu anaye tenda dhambi, si mtu ambaye unahisi tabia yake inahitaji kurekebishwa kwa njia fulani au mtu anayekukasirisha au kukuudhi.

Kwa njia tofauti, mojawapo ya maandiko yanayonukuliwa mara nyingi zaidi ni “Usihukumu ili usije ukahukumiwa” (Mathayo 7:1). Ikitolewa nje ya muktadha, aya hiyo imetumika kuhalilisha kimakosa kutowahi kuchukua msimamo juu ya jambo lolote ambalo lingehitaji hukumu kutolewa. Badala yake, aya hii inarejelea aina za hukumu za kinafiki, za kujihesabia haki, zisizo za haki, haswa pale ambapo mpinzani ana hatia ya dhambi sawa na yule anayekabiliwa.

Kwa hivyo, ni wakati gani Wakristo wanapaswa kuzungumza na au kujaribu kumrekebisha Mkristo mwenzao? Tunapozungumza na Bwana kwanza, kuwa na nia ya kunyenyekea na kujali mtu mwingine, na kujitolea kufuata taribu zilizoainishwa katika Neno Lake kwa hali kama hiyo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni wakati gani Mkristo anapaswa kumrekebisha Mkristo mwingine?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries