settings icon
share icon
Swali

Biblia inasemaje kuhusu mizuka /kutembelea mara kwa mara?

Jibu


Je, kuna kitu kama mizuka? Jibu la swali hili linategemea nini hasa kinamaanishwa na neno "mizuka." Kama neno ili linamaanisha "viumbe vya mapepo,"basi jibu linahitimu kuwa "ndiyo."ikiwa neno ili linamaanisha "mapepo za watu waliokufa," jibu ni "hapana." Biblia inaweka wazi kwamba kuna viumbe vya mapepo kwa wingi,ambazo ni nzuri na mbaya. Lakini Biblia inpinga wazo kwamba mapepo ya wafu yaweza kubaki duniani na "kuwatembelea walio hai mara kwa mara".

Waebrania 9:27 inakiri, “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu." Hilo ndilo hufanyikia royo ya mtu- baada ya kifo-hukumu. Matokeo ya hukumu hii ni mbinguni kwa muumini (2 Wakorintho 5: 6-8; Wafilipi 1:23) na jehanamu kwa kafiri (Mathayo 25:46; Luka 16: 22-24). Hakuna atakaye kaa kati kati. Hakuna uwezekano wa kubaki duniani kama pepo kama vile "mzuka." Kama kuna vitu kama vile mizuka, kwa mujibu wa Biblia , basi haiwezi kabisa kuwa pepo zilizotolewa kwa miili ya wafu.

Biblia inafunza wazi wazi sana kwamba kuna kweli mapepo halisi ambao yanaweza kujiunganisha na kuonekana katika ulimwengu wetu halisi. Biblia inatambua mapepo haya kama malaika na mashetani. Malaika ni mapepo halisi walio waaminifu katika kumtumikia Mungu. Malaika ni wenye haki, wema, na takatifu. Mashetani ni malaika waliotenda dhambi, malaika walioasi dhidi ya Mungu. Majini ni mapepo mbaya,danganyifu, na haribifu. Kulingana na 2 Wakorintho 11: 14-15,majini hujifanya s kama "malaika wa nuru" na kama “watumwa wa haki.”Kuonekana kama "mzuka" na kuiga mfu bila shaka inaonekana kuwa na nguvu na uwezo ambao majini humiliki.

Mfano wa karibu wa Biblia wa "kusumbuliwa na mapepo mara kwa mara" unapatikana katika Marko 5: 1-20. Jeshi la mapepo lilimshika mtu na kumtumika kwa kutembelea makaburini mara kwa mara. Hakukuwa na mizuka iliyohusika. Ilikuwa ni kesi ya mtu wa kawaida kudhibitiwa na mapepo kwa kuwatishia watu wa eneo hilo. Mapepo tu hutafuta "kuua, kuiba, na kuharibu" (Yohana 10:10). Wao hufanya kitu chochote ndani ya uwezo wao kuwadanganya watu, kuongoza watu mbali na Mungu. Hii inaweze kuwa ndio maelezo ya kazi ya "kizuka" hii leo. Hata kama inaitwa maroho, zimwi mla maiti, au Pepo ghazia, kama kuna shughuli halisi ya kishetani za kiroho zinatokea, ni kazi ya mapepo.

Je kuhusu matukio ambayo "vizuka" hufanya kazi katika njia za kusaidia"? Je, na wale ambao hudai kuwa wanamwita marehemu na kupata habari muhimu kutoka kwao? Tena, ni muhimu kukumbuka kwamba lengo la mapepo ni kudanganya. Kama matokeo yake ni kwamba watu huamini katika mawazo badala ya Mungu, mapepo yatakuwa tayari zaidi kutoa taarifa ya kweli. Hata habari jema na kweli, kama kutoka chanzo kwa nia mbaya, inaweza kutumika kwa kupotosha, danganya, na kuharibu.

Maslahi katika uwazimu inazidi kuwa ya kawaida. Kuna watu na biashara ambazo zinadai kuwa "wawindaji maroho," ambao kwa bei wataondoa vizuka nyumbani kwako. Kienyeji, mkusanyiko wa kuwasiliana na pepo, pepo za wastani zinazidi kuchukuliwa kawaida. Binadamu kindani wana ufahamu wa ulimwengu wa kiroho. Cha kusikitisha, badala ya kutafuta ukweli juu ya roho ya dunia na kuwasiliana na Mungu na kusoma Neno lake, watu wengi hujiruhusu wenyewe kupotoshwa na ulimwengu wa roho. Mapepo hakika hucheka kwa mwingi wa udanganyifu ambao upo katika dunia ya leo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasemaje kuhusu mizuka /kutembelea mara kwa mara?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries