settings icon
share icon
Swali

Je miujiza ya Roho Mtakatifu ipo kwa ajili ya siku hizi?

Jibu


Kwanza, ni muimu kutambua kwamba hili si swali la ikiwa Mungu bado anafanya muijiza hii leo. Itakuwa ubumpavu, au swala lisilo la kibibilia kudai kwamba Mungu haponyi, haneni na watu, na hatendi miujiza na maajabu hii leo. Swali ni, ikiwa miujiza ya Roho Mtakatifu imeelezewa katika 1Wakorintho 12-14 kama bado haiko kazini katika kanisa hii leo. Pia hili si swali la kama Roho Mtakatifu anampa mtu miujiza ya Roho ya vipawa. Swali ni ikiwa Roho Mtakatifu bado anadhihirisha miujiza ya vipawa hii leo. Zaidi ya yote zote twatambua kwamba Roho Mtakatifu ako huru kudhihirisha vipawa kulingana na mapenzi yake (1Wakorintho 12:7-11).

Katika kitabu cha Matendo ya Mitume na Barua, wingi wa miujiza unafanywa na Wanafunzi na wendani wa karibu nao. Paulo anatoa sababu ni kwa nini: “Kweli ishara za mtume zilitendwa katikati yenu katika saburi yote, kwa ishara na maajabu na miujiza.” (2Wakorintho 12:12). Kama kila Mkristo katika Kristo alikua amejiami na uwezo wa kutenda ishara, maajabu na miujiza, kwa hivyo, ishara, maajabu na miujiza hivyo basi aingekuwa ishara ya mitume. Matendo ya Mitume 2:22 yatwambia kwamba Yesu “alisifiwa” kwa “miujiza, maajabu na ishara” vilevile, Mitume walitambulika kuwa watume wa kweli kutoka kwa Mungu kwa miujiza waliyoitenda. Matendo ya Mitume 14:3 yaeleza ujumbe wa injili “kuthibitishwa” na miujiza Paulo na Baranaba waliyoitenda.

Mlango wa 12-14 wa 1Wakorintho unashughulikia mada ya vipawa vya Roho Mtakatifu. Inaonekana kutoka kwa dondoo Wakristo wa “kawaida” wakati mwingine walipewa vipawa vya muijiza (12:8-10, 28-30). Hatwambiwie vile vilikuwa vya kila mara. Kutoka kwa kile tulicho kisoma kwamba mitume “walitambulika” kwa ishara na maajabu, inaweza onekana kuwa vipawa vya miujiza vilivyopewa Wakristo wa “kawaida” vilikuwa vya ihari si kwa mjibu wa sheria. Kando na Mitume na wale wendani wao wa karibu, Agano Jipya hakuna mahali kamili inamweleza mtu binafsi akitenda miujiza ya vipawa vya Roho.

Pia ni muimu kugundua kwamba kanisa la kwanza halikuwa na Bibilia iliyo kamilika, vile tuko nayo hii leo (2Timotheo 3:16-17). Kwa hivyo, vipawa vya unabii, maarifa, hekima na kadhalika vilikuwa vya muimu kwa sababu ya Wakristo wa kwanza wajue chenye Mungu anawahitaji wafanye. Kipawa cha unabii kiliwawezesha Wakristo kutangaza ukweli mpya na ufunuo kutoka kwa Mungu. Sasa kwa sababu ufunuo wa Mungu umekamilika katika Bibilia, ufunuo wa vipawa hauitajiki tena, kwa karibu lakini si kiwango sawa vile ilikuwa wakati wa Agano Jipya.

Kimuijiza Mungu huponya watu kila siku. Mungu bado hunena nasi hii leo, iwe ni kwa sauti inayosikika, kwa mawazo yetu au kupitia picha ya kimawazo au hisia. Mungu bado anatenda miujiza ya kushangaza, ishara na maajabu na wakati mwingine anatenda miujiza kupitia kwa Wakristo. Ingawa mambo haya si ya lazima, vipawa vya miujiza vya Roho. Lengo kuu la miujiza lilikuwa kuthibitisha kwamba injili ilikua ya kweli na mitume walikuwa watumwa wa kweli kutoka kwa Mungu. Bibilia haisemi wazi wazi kuwa vipawa vya miujiza vimetoweka, badala, yaweka mzingi, kwamba ni kwa nini havitaweza kutokea tena katika hali sawa na ile vilitokea wakati wa Agano Jipya.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je miujiza ya Roho Mtakatifu ipo kwa ajili ya siku hizi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries