settings icon
share icon
Swali

Mikutano ya kikiristo ilikuwa gani?

Jibu


Mikutano ya kikiristo imetoa baadhi ya mijadala ya mara kwa mara dhidi ya imani ya Kikristo. Baadhi ya magaidi ya Kiislamu hata wanadai kwamba mashambulizi yao ya kigaidi ni kulipiza kisasi kwa yale Wakristo waliyofanya katika vita vya kidini mikutanoni. Hivyo,mikutano hii ya vita vya kidini ilikuwa nini na ni kwa nini inatazamwa kuwa tatizo kubwa hivyo kwa imani ya wakiristo?

Kwanza kabisa, vita vya kidini havipaswi kulejelewa kuwa “ mikutano ya kikiristo.’’Watu wengi waliohusika katika mikutano hawakuwa wakristo wa kweli, ingawa walidai kuwa walikuwa. Jina la Kristo lilitusiwa ,likatumiwa vibaya, na kukasifiwa kwa matendo ya wengi wa wapiganaji wa vita ya kidini katika mikutano ya kikiristo. Pili, mikutano ilifanyika kutoka wastani wa AD 1095 hadi 1230. Je, matendo yasiyo ya kibiblia yayowahusu Wakristo mamia ya miaka iliyopita bado ishirikishwe dhidi ya Wakristo siku hizi?

Tatu, si kwamba hii ni udhuru wa kutosha, lakini ukiristo sio tu dini iliyo na zama iliyokuwa na vurugu. Katika uhalisi, mikutano ya kikiristo ilikuwa majibizano kwa uvamizi wa kiislamu kwa ardhi iliyomilikiwa kimsingi na wakiristo mwanzoni. Kutoka takribani AD 200 hadi 900, nchi ya Israel, Yorodani, Misri, Siria, na Uturuki zilimilikiwa kimsingi na Wakristo. Mara baada ya Uislamu kuwa na nguvu, Waislamu walivamia nchi hizi na kikatili kudhulumu, wakafanya watumwa, wakaweka kizuizini, na hata kuwaua Wakristo walioishi katika nchi hizo. Kwa mjibu, Kanisa Katoliki la warumi na "Kristo" wafalme / watawala kutoka Ulaya waliamuru mikutano ya kikiristo kudai ardhi ambazo Waislamu walikuwa wamechukua. Vitendo ambavyo wengi wa wanaoitwa Wakristo walichukua katika mikutano bado vilikuwa vinasikitisha . Hakuna uhalali wa kibibilia kwa kuvamia na kumiliki ardhi, kuua raia, na kuharibu miji katika jina la Yesu Kristo. Wakati huo huo, Uislamu sio dini inayoweza kuzungumza kutoka kwa hali ya kutokuwa na hatia katika mambo haya.

Kueleza kwa kifupi, mikutano hii ilikuwa na majaribio katika karne ya 11 hadi 13 karne A.D. ili kudai ardhi katika Mashariki ya Kati ambayo ilichukuliwa na waislamu. Mikutano hiyo ilikuwa katili na mbaya. Watu wengi walilazimishwa "kubadili dini" kuwa wakristo. Kama wangekataa, walikuwa wanauawa. Wazo la kuvamia na kuchukua ardhi kwa njia ya vita na vurugu katika jina la Kristo sio kibiblia kabisa. vitendo vingi vilivyofanyika katika mikutano vilikuwa kinyume kabisa kwa vyote ambavyo imani ya wakristo inasimamia .

Jinsi gani tunaweza kujibu wakati, kwa mjibu wa matokeo ya mikutano ya Injili, imani ya Kikristo inavamiwa na wanaomkana Mungu, wasadikio kuwa hawana habari za Mungu wala hawawezi kuzijua, wanaoshuku, na wale wa dini zingine? Tunaweza kujibu kwa njia zifuatazo: 1) Je, unataka kuwajibika kwa matendo ya watu walioishi zaidi ya miaka 900 + iliyopita? 2) Je, unataka kuwajibika kwa matendo ya kila mtu ambaye anadai kuwakilisha imani yako? Kujaribu kulaumu wakristo wote kwa ajili ya mikutano ni sawa na kuwalaumu Waislamu wote kwa ugaidi wa Kiislamu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mikutano ya kikiristo ilikuwa gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries