settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inaelezeaje miili iliyotukuka tutakayokuwa nayo Mbinguni?

Jibu


Ingawa Biblia haielezi kwa undani miili yenye utukufu tutakayopokea mbinguni, tunajua kwamba itakuwa kama mwili wa Yesu uliofufuliwa. Miili yetu ya kibinadamu imeelezewa katika 1 Wakorintho 15:42-53 kama inayoharibika, isiyo na heshima, na dhaifu, yote kwa sababu ya dhambi. Miili yetu tukufu itakuwa isiyoharibika, yenye heshima, na yenye nguvu. Miili yetu mipya haitakuwa tena miili ya “asili”, chini ya kuoza na kufa; tutaishi katika “ushindi juu ya dhambi na mauti,” aliyoshinda Kristo kwa niaba yetu (1 Wakorintho 15:57).

Wakiwa na miili isiyoharibika, hawatateseka tena kutokana na magonjwa na kifo, wala hawatapatwa na joto na baridi au njaa na kiu. Miili yetu mipya itakuwa ya heshima kwa kuwa haitaaibishwa au kuaibika kwa sababu ya dhambi. Adamu na Hawa walipofanya dhambi, jambo la kwanza walilohisi lilikuwa aibu kwa sababu ya uchi wao (mwanzo 3:6-7). Ingawa Biblia haionyeshi miili ya utukufu ikiwa uchi, bali iliyovikwa mavazi maeupe (Ufunuo 3:4-5, 18), watakuwa safi na wasiotiwa unajisi na dhambi. Miili yetu ya hapa duniani ni “dhaifu” kwa njia nyingi. Sio tu kwamba tuko chini ya sheria za asili za mvuto na wakati/uwazi, tunadhoofishwa na dhambi na majaribu yake. Miili yetu tukufu itatiwa nguvu na Roho anayotumiliki, na udhaifu hautakuwepo tena.

Kama vile miili yetu ya hapa duniani inavyofaa kabisa kuishi duniani, miili yetu iliyofufuliwa itafaa kwa uzima wa milele. Tutakuwa na umbo na uimara kwa mguzo (Luka 24:39-40). Kuna uwezekano tutaweza kufurahia chakula, lakini hatutalazimika kula kwa kuwa tuna hitaji kula au kwa tamaa ya kimwili (Luka 24:41-43). Na kama Musa na Eliya, tutaweza kufurahia katika utukufu wa Muumba wetu katika ushirika wa Mwanawe mpendwa (Mathayo 17:2-3; Wafilipi 3:10). Miili tunayorithi itakuwa kama vile Mungu alivyokusidia hapo awali, badala ya ile tunayo sasa. Unyonge na udhaifu wa mwili wetu wenye dhambi utaondoka; badala yake, tutatukuzwa pamoja na Kristo, na utukufu huo utaenea hadi kwenye miili tutakayotwaa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inaelezeaje miili iliyotukuka tutakayokuwa nayo Mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries