settings icon
share icon
Swali

Je! Mwili wa bana una umuimu gani?

Jibu


Kuyachunguza maandiko juu ya mesa ya bwana kunatia moyo kwa sababu ya kifo cha maana yanazungumzia. Ilikuwa ni kwa sababu ya siku za kale za pasaka wakati wa kifo chake Yesu mwenyewe akaanzisha kakula cha ushirika mpya cha maana ambacho twakifuata hii leo. Ni sehemu maalumu kwa kila Mkristo katika kuabudu. Kinatufanya kukumbuka kifo cha Bwana wetu na kufufuka kwake na tutazamie kurejea kwake kwa utukufu mawinguni.

Pasaka ilikuwa mojawapo ya siku kuu takatifiu katika miaka ya dini ya Wayahudi. Ilikuwa ukumbusho wa lile pigo la mwisho kwa Wamisri wakati wazaliwa wa kwanza wa kiume walikufa lakini wa Waisraeli wakaachwa kwa sababu ya damu ya kondoo iliyopakwa katika kizingiti cha juu na miimo ya milango. Huyo Kondoo baadaye alichomwa na kuliwa kwa mkate usiyo na chachu. Amri ya Mungu ilikuwa kwamba kwa vizazi vyote vijao hii dhabihu ya pasaka itasherehekewa. Hadithi hii imeandikwa kitabu cha Kutoka 12.

Wakati ule wa sherehe ya pasaka ya mwisho, Yesu akatwaa kipande cha mkate na akashukuru Mungu. Wakati aliumega na kuwapa wanafunzi wake, akasema, “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akasema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu” (Luka Mtakatifu 22-19-21). Kwa kumaliza pasaka aliimba zaburi (Mathayo 26:30), na wakatoka nche usiku wakielekea mulima wa misaituni. Hapa ndipo Yesu alisalitiwa na Yudasi, vile ilivyotabiriwa. Siku iliyofuata alisulubiwa.

Matukio ya mesa ya Bwana yanapatikana katika injili (Mathayo 26:26-29; Mariko 14:17-25 Luka 22:7-22; na Yohana 13:21-30). Mtume Paulo aliandika juu ya mesa ya Bwana katika 1 Wakorintho 11:23-29. Paulo anatumia maneno yale yale yametumika katika injili: “Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili” (1 Wakorintho 11:27-29). Tunaweza kuuliza je! Inamaanisha nini kushiriki mkate na kikombe “kwa njia isiyostahili.” Yaweza maanisha kuwa, kupuuza ukweli kamili juu ya mkate na kikombe na kusaau dhabihu ya dhamana Mwokozi wetu alilipia wokovu wetu. Au yaweza maanisha kuwa, kiuruhusu sherehe hiyo kuwa kifo cha kawaida, kafara ya kawaida au kuja kushiriki mesa ya Bwana na dhambi ambayo haujatubu. Kwa kuchunga maelekezo ya Paulo, lazima tujihoji wenyewe kabla ya kuula makate na kukinywea kikombe.

Maneno mengine Paulo aliyasema ambayo hayako kwa matukio ya injili ni “Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo” (1 Wakorintho 11:26). Hii inaweka kadirio la wakati kwa sherehe hii- hata Yesu ajapo. Kutoka kwa hili tukio fupi, twasoma jinsi Yesu alivitumia vitu viwili kama mfano wa mwili na damu yake na akaviweka kuwa kama kumbusho la kifo chake. Haikuwa kumbukumbu ya mawe yaliyochongwa au chuma kilichofuliwa na mhunzi, bali ni ya mkate na mzabibu.

Alisema mkate unasimamia mwili wake ambao ungevunjwa. Hakukuwa na mfupa wowote ulivunjwa, lakin mwili wake ulitezwa sana kiwango ambacho ni vigumu kuutambua (Zaburi 22:12-17; Isaya 53:4-7). Mzabibu ulisimamia damu yake, kuashiria kifo cha ajabu baadaye angekipitia. Ni mwana mkamilifu wa Mungu akawa timizo la matukio yasiyo hesabika ya unabii katika Agano la Kale kuhusu mkombozi (Mwanzo 3:15; Zaburi 22; Isaya 53). Wakati alisema, “fanyeni hivyo kwa ukumbusho wangu,” alimaanisha ni sherehe ambalo lingendelezwa baadaye. Pia ilimaanisha kwamba pasaka iliyohitaji kondoo achinjwe na kutazamia kukuja kwa Mwana kondoo wa Mungu ambaye atasichukua ndambi za ulimwengu, hiyo ilitimizwa kwa mesa ya Bwana. Agano jipya linasimama badalay ya Agano La Kale wakati Kristo sadaka ya pasaka (1 Wakorintho 5:7), alisulubiwa (Waebrania 8:8-13). Ule mpangilio wa dhabihu hauitajiki tena (Waebrania 9:25-28). Mesa ya Bwana ni kumbusho la yale Kristo alitufanyia na sherehe ya yale tunayoyapokea kama faida ya ile dhabihu iliyotolewa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mwili wa bana una umuimu gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries