settings icon
share icon
Swali

Mbinguni ni kubwa kiasi gani?

Jibu


Neno mbadala la “mbingu” katika Agano la Kale ni la Kiebrania shameh au shamayim, ambalo linamaanisha anga, upinde wa juu ya ulimwengu ambapo mawingu husonga, na zaidi ya hayo, ni mahali ambapo sayari na nyota zipo. Katika Agano Jipya, neno mbinguni ni tafsiri ya neno la Kigiriki Ouranos, ambalo linamaanisha “anga” na “makao ya Mungu” na, kwa kuongezea, “eneo la milele la furaha na utukufu.” Anga katika ukubwa wake ni sitiari ya ukubwa na ukuu wa Mungu. Ni mfano bora wa kidunia wa mahali ambapo Mungu anaishi.

Mbinguni ni kubwa kadri gani- mahali ambapo Mungu anaishi ni kubwa kiasi gani? Tunajua kwamba Mungu Mwenyewe hana kikomo. Mbingu na nchi haziwezi kumtosha. Kwa upande wa wakati, hakuna mwanzo wala mwisho wa miaka yake (Zaburi 102:27); kwa upande wa ufalme wake, utawala wake hautakuwa na mwisho (Luka 1:33); kwa upande wa tabia yake, Yeye habadiliki (Waebrania 1:12; Yakobo 1:17). Mungu aliumba mbingu na nchi (Mwanzo 1:1). Isaya asema hivi kuhusu uumbaji wa Mungu wa nyota: “Inueni macho yenu mtazame mbinguni: Ni nani aliyeumba hivi vyote? Ni yeye aletaye nje jeshi la nyota moja baada ya nyingine na kuziita kila moja kwa jina lake. Kwa sababu ya uweza wake mkuu na nguvu zake kuu, hakuna hata mojawapo inayokosekana” (Isaya 40:26)

Wanasayansi hawajaweza hata kutoa ramani ya kiwango cha ulimwengu unaojulikana. Kuna picha inayoitwa SDF (eXtreme Deep Field) ambayo iliwekwa pamoja kutoka kwa picha zilizopigwa na Hubble Space Telescope (Wapiga darubini wa anga), kwa kipindi cha miaka kumi. Inaonyesha idadi ya vikundi kubwa vya sayari, kila moja ikiwa na mabilioni ya nyota kama vile jua letu. Jua letu liko umbali wa maili milioni 93 kutoka duniani. Na sayari zingine ziko mbali kutoka kwa nyingine- Andromeda, sayari iliyo karibu na yetu iko umbali wa miaka milioni 2.2 ya mwanga. Ili kutoa wazo la umbali huo, meli inayoenda mwendo wa kasi maili 18,000 kwa saa moja, itahitaji miaka 37,200 kusafiri mwaka mmoja mwepesi. Ulimwengu ni mkubwa kabisa-na Mungu aliuumba wote.

Kwa hiyo, mbinguni ni kubwa kiasi gani? Hatujui hasa. Biblia haitoi vipimo vyovyote vya mstari. Yohana alipokuwa na maono yake ya mbinguni, aliandika hivi: “ Hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna yeyote awezaye kuuhesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo” (Ufunuo 7:9). Kwa hiyo mbingu angalau ni kubwa na ya kutosha kwa umati usiohesabika-na tunaweza waza kwamba hakutakuwa na msongamano mbinguni.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mbinguni ni kubwa kiasi gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries