settings icon
share icon
Swali

Je! inamaanisha nini kuwa mbingu na nchi zitapita?

Jibu


Mara kwa mara Biblia inatuonya kwamba ulimwengu huu hautadumu milele. “Mbingu na dunia zitatoweka,” Yesu alisema katika Mathayo 24:35. Kauli yake ilikuwa katika muktadha wa unabii wa nyakati za mwisho na hali ya milele ya maneno ya Yesu: “maneno yangu hayatapita kamwe.” Hii inamaanisha kwamba kumwamini Yesu ni bora kuliko kuamini kitu chochote katika ulimwengu huu.

Vile vile Yesu anairejelea mbingu na dunia zitapita katika Mathayo 5:18. Katika Ufunuo 21:1, Yohana anaandika juu ya mbingu mpya na nchi mpya katika hali ya milele baada ya kuona kuwa “mbingu ya kwanza na dunia ya kwanza zilikwisha kutoweka” (linganisha na Isaya 65:17 na 2 Petro 3:13). “Kupita” ni kutoweka, au kutokuwepo tena. Hii inamaanisha kuwa mbingu na dunia zinazoonekana-ulimwengu wa nyenzo na vyote vilivyomo-lakini sio roho/nafsi ya wanoishi katika maeneo hayo. Maandiko yako wazi kwamba watu wataishi zaidi ulimwengu wa nyenzo ya sasa, wengine katika hali yafuraha na wengine katika hali ya dhiki, na kwamba ulimwengu wa sasa utabadilishwa na mwingine ambao hautaona kutiliwa doha na dhambi.

Namna ambayo ulimwengu wa sasa utaharibiwa imefunuliwa katika 2 Petro 3:10-12: “Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi. Ndipo mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; na vitu vya asili vitateketezwa kwa moto…. siku ambayo mbingu zitateketezwa kwa moto na kutoweka, na vitu vyote vilivyomo ndani yake vitayeyushwa kwa moto.” Katika siku za Noa, ulimwengu uliharibiwa kwa maji, lakini Mungu aliahidi kutoleta mafuriko tena ulimwengu kote (Mwanzo 9:11). Katika Siku ya Bwana, ulimwengu utaangamizwa kwa moto.

Nabii Isaya alitabiri mbingu na nchi kupita pia. “Na jeshi lote la mbinguni litafumuliwa, na mbingu zitakunjwa kama karatasi, na jeshi lao lote litanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika” (Isaya 34:4). Bwana anawahakikishia watu wake kwamba, hata kama mbingu na nchi zinapita, wokovu Wake utakuwa imara: “maana mbingu zitatoweka kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, wanaoishi ndani yake watakufa kadhalika; bali wokovu wangu utakuwa wa milele, na haki yangu haitatanguka (Isaya 51:6).

Kufahamu kwamba mbingu na nchi zitapita hutupa mtazamo wa maisha. Ulimwengu huu sio makao yetu ya milele. “Lakini kufuatana na ahadi yake, sisi tunangojea mbingu mpya na dunia mpya ambamo haki huishi” (2 Petro 3:13). Yesu anatuambia tuwe na vipau mbele vyema: “Msijiwekee hazina nyingi duniani … Lakini jiwekeeni mali mbinguni ambapo wadudu na kutu hawaharibu na wezi hawavunji na kuiba” (Mathayo 6:19-20). Na Petro baada ya kutukumbusha jinsi ulimwengu huu ni wa muda, anasema, “Kwa hiyo wapendwa, kwa kuwa mnatazamia mambo haya, jitahidini ili mkutwe hamna doa wala lawama, mkiwa na amani naye” (2 Petro 3:14).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! inamaanisha nini kuwa mbingu na nchi zitapita?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries