settings icon
share icon
Swali

Je, Mkristo anapaswa kuwa na mtizamo gani kuhusu michezo/riadha?

Jibu


Jibu: Michezo ni sehemu kubwa ya maisha kwa watu wengi, iwe wanatazam matukio ya riadha, wanaendesha watoto wao kwenda na kutoka mazoezi ya michezo, au kujihuzishaa moja kwa moja na michezo.

Mashindano ya michezo na riadha yamekuwa maarufu tangu zama za kale. Biblia inatoa mlinganisho mbali mbali wa maisha ya Kikristo kutoka ulimwengu wa michezo: 1 Wakorintho 9:26 ina rejeleo la kupiga hewa; mwandishi wa Waebrania analinganisha maisha ya Kikristo na mbio (Waebrania 12:1); na Paulo anatuhimiza “Kwa hiyo kimbieni katika mashindano kwa jinsi ambavyo mtapata tuzo” (1 Wakorintho 9:24).

Kwa kuzingatia utumizi mzuri wa Biblia wa mifano inayohusiana na michezo, hakuwezi kuwa na kosa lolote kwa kutazama au kushiriki katika mashindano ya riadha. Kufuatilia timu ya kandanda unayoipenda zaidi, kucheza duru chache za gofu, kuhudhuria mechi ya voliboli, au kujisajili kwa mpira wa laini wa jumuiya ni jambo ambalo Wakristo wanaweza kufurahia. Wanariadha Wakristo na wakufunzi mara nyingi hupata fursa ya kutumia umashuhuri wao katika michezo kama jukwaa la kuendeleza injili.

Wakristo wanaocheza michezo wanaweza kuthibitisha manufaa mengi ambayo kujihusisha katika michezo kunaweza leta, hii ikiwa ni pamoja na kupunguza mawazo; kudhibiti uzito wa mwili; urafiki; na ukuzaji wa uwajibikaji, uongozi, na mawasiliano, kuweka malengo, na ujuzi wa kutatua matatizo. Uvumilivu na ustahimilivu unaohitajika katika mashindano ya riadha unaweza kuwa wa thamani katika kujenga na kuimarisha tabia.

Mojawapo ya faida kuu za kushindana katika michezo ni kujibuka kwa kujidhibiti: “Kila mmoja anayeshiriki katika mashindano hufanya mazoezi makali” (1 Wakorintho 9:25). Katika suluhu ya hatua ya ushindani, uwepo wa kujithibiti-au ukosefu wake-unakuwa dhahiri kwa watazamaji wote. Baadhi ya wanariadha (na mashabiki) hukabili shida zinazohusiana na mchezo kwa neema na utulivu; wengine huyeyuka kwa hasira ya mtu mzima. Tatizo si mchezo; ni tabia ya ndani ya mwanariadha au shabiki. Kwa njia nyingi, tukio la michezo hutoa fursa ya kujaribu tabia ya washindi na walioshindwa. Wanariadha wa Kikristo, wakufunzi, na mashabiki wanapaswa kujazwa na Roho Mtakatifu na waonyeshe tunda la Roho, bila kujali walipo, iwe ni katika kiwanja cha michezo, uwanjani, au katika chumba za mapumiziko.

Katika nyanja zote za maisha, ni lazima tuwe na usawaziko kuhusiana na kushiriki kwetu katika michezo. Ni lazima tuweke vipaumbele. Ni rahisi kwa shabiki wa michezo kuipindua, kutumia wakti mwingi, pesa, na rasilimali zingine kwa kile kinachopaswa kuwa burudani ya kufurahisha. Ni rahisi kwa mwanariadha anayetaka kufanikiwa kutumia muda na nguvu nyingi kupita kiasi katika mazoezi, kupuuza familia, marafiki, au kutembea na Mungu. Biblia hutusaidia kufafanua vipaumbele vyetu: “Kwa maana mazoezi ya mwili yana faida kwa sehemu, lakini utauwa una faida katika mambo yote, yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa na ya ule ujao” (1 Timotheo 4:8).

Michezo ni nzuri na yenye manufaa inapozingatiwa vyema. Kamwe michezo isiruhusiwe kuchukua wakati na Mungu au kuwa muhimu zaidi kuliko kutafuta ufalme wa Mungu na haki (Mathayo 6:33). Sanamu hazipaswi kuwa sehemu ya maisha ya Kikristo (1 Yohana 5:21). Na katika chochote tunachofanya, ndani au nje ya uwanja, tunapaswa kufanya yote kwa utukufu wa Mungu (1 Wakorintho 10:31).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mkristo anapaswa kuwa na mtizamo gani kuhusu michezo/riadha?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries