settings icon
share icon
Swali

Je, Mkristo anapaswa kuwa na marafiki mashoga?

Jibu


Katika kuzingatia kama Mkristo anapaswa kuwa na marafiki mashoga, tunahitaji kujiuliza kama yesu angekuwa na marafiki mashoga. Hakuna mahali popote Agano Jipya linawatambua watu falani mahususi kuwa mashoga. Kwa hivyo, hakuna kumbukumbu za Yesu kuingiliana na shoga. Tunajua kutoka kwa injili, hata hivyo kwamba Yesu alimpenda kila mtu Aliyekutana naye. Hakuzingatia kundi moja la watu kustahili injili kuliko linguine. Kwa hakika, Yeye alijitolea ili kumkomboa mtu mwenye pepo (Marko 5:1-20) na kuleta tumaini kwa mwanamke msherati kutoka asili ya kabila iliyodharauliwa (Yohana 4). Aliwaponya wenye ukoma (Luka 17:10-19), alimsamehe mwanamke mzinzi (Yohana 8:1-11), na akala pamoja na watoza ushuru (Marko 2:16)-wote ambao walichukuliwa kuwa hawafai kushirikiana wa watu wema. Tunaweza kudhani Yesu angetumia wakati wake pamoja na mashoga pia.

Ushoga ulikuwa dhambi katika siku za Yesu, na ni dhambi hata sasa. Viwango vya Mungu vya jinsia ya kibinadamu havijabadilika. Hata hivyo, Yesu alikuja kutafuta na kuokoa waliopotea (Luka 19:10). Tunajifunza kutoka kwa njia ya upole Aliyoshughulika na watu wenye dhambi kwamba Angewapa mashoga huruma sawa na fursa ya “enenda na usitende dhambi tena” (Yohana 8:11). Ingewezekana, Yesu anagejumuisha mashoga alipokula kwenye nyumba za “watenda dhambi wenye sifa mbaya” (Luka 15:1).

Ni muhimu kutambua kwamba uchaguzi wa Yesu kutangamana na wenye dhambi ulikuwa kwa kusudi moja. Alikuwa amekuja kuleta nuru katika giza lao (Yohana 1:9; 12:46). Alitaka kuwa pamoja na wenye dhambi ili aweze kuwaeleza upendo na msamaha wa Mungu. Hakuchagua kutangamana nao kwa sababu aliikubali dhambi yao. Hakushiriki kwa njia yoyote au kuwezesha dhambi. Alikuja kuwainua watu kutoka kwa dhambi, ikiwa tu wengemwamini (Luka 7:36-50).

Pia, tunapojiuliza ikiwa Mkristo anapaswa kuwa na marafiki mashoga, tunahitaji kufafanua marafiki. Tunatangamana na watu wa viwango vingi tofauti, kutoka kwa marafiki wa kawaida hadi wenzi wa karibu wa roho. Urafiki unajengwa katika maslahi ya pamoja, maadili, na uzoefu. Mkristo mwenye nia ya kumfuata Yesu hatakuwa na mengi yanayofanana sana na mtu anayefuata maisha mapotovu. Kutakuwa na mipaka kwa jinsi urafiki unavyoweza kuwa wa karibu (2 Wakorintho 6:14-16).

Katika ulimwengu wetu unaozidi kupotoka, aina zote za ngono potovu zinapongezwa kuwa nzuri. Kwa mtazamo wa kibiblia, watu wengi waliochanganyikiwa wamenaswa katika dhambi ya ushoga na wanahitaji kukombolewa. Wanahitaji kujua kwamba Mungu aliwaumba zaidi ya hayo. Aliwaumba kwa ajili Yake. Hawawezi kujiweka huru na dhambi; wanahitaji mkombozi.

Yesu ndiye Mkombozi (Zaburi 18:2; 1 Wakorintho 6:11), na tumeitwa kutangaza ujumbe huo. Sisi ni wapatanishi, tukiwa tumekabidhiwa “huduma ya upatanisho” (2 Wakorintho 5:18). Tukifuata mfano wa Kristo, tunaweza kuwa marafiki wa mashoga, kuonyesha upendo Wake kwao, kuwaombea, na kusherehekea mambo ya kawaida tunayoweza kupata. Katika kutangamana na marafiki mashoga, lazima tuwe waangalifu ili tusiashirie kwamba tunahalalisha dhambi zao. Hatuwezi kuruhusu upendo wetu kwa shoga utafanye tulegeze masharti ya neno la Mungu.

Je, Mkristo anapaswa kuwa na marafiki mashoga? Naam, kwa njia sawa na kwa sababu sawa kwamba Yesu angekuwa na marafiki mashoga. Alimwona kila mtu kama aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27). Alimwona mtu huyo kuwa jinsi alivyomuumba. Aliona hofu yao, kuchanganyikiwa kwao, huzuni zao, na maisha yao bila Yeye. Alimpa kila mtu msamaha sawa na mabadiliko walipokuwa tayari kumfanya Bwana wa maisha yao. Mkristo ni mwenye dhambi ambaye amekubali injili na sasa anamwakilisha Kristo kwa kila mtu, pamoja na marafiki zetu mashoga, kwa neema na ukweli (Yohana 1:14).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mkristo anapaswa kuwa na marafiki mashoga?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries