settings icon
share icon
Swali

Je! Mkristo anapaswa kuvaa mapambo ya vito ya kidini, kama vile sanamu ya Yesu Kristo msalabani?

Jibu


Kuna mjadala mkubwa wa ikiwa ni bora ua sio bora-au hata dhambi kuvaa mapambo ya vito ya kidini kama vile sananu ya Yesu Kristo msalabani. Wakristo hawakuvaa vito za misalaba shingoni mwao hadi baada ya kusulubiwa kulikoma kuwa njia ya pekee ya adhabu ya kifo; kwa hiyo sio sawia na mtu wa kisasa akivaa kijisanamu cha chumba kidogo cha kifo shingoni mwake, kama vile baadhi ya watu wamedokeza. Wengi wanautazama msalaba kama chombo cha mauti kilichotumiwa kumuua Mwokozi wetu mpendwa. Wengine wanaona kuwa ni mfano wa kifo na ufufuo wa Yesu, ukumbusho wenye nguvu wa dhabihu na ushindi wa Yesu, na ukumbusho wa zawadi ya Mungu ya neema katika kutupa wokovu. Kwa sababu yalikuwa mapenzi ya Mungu, Yesu alienda msalabani kwa hiari, akichukua dhambi juu yake, akiwatakaza dhambi zao wenyewe wale wanaomwamini.

Sababu pekee ambayo Maandiko yatakataza kuvaa mapambo ya vito ya kidini kama vile msalaba au sanamu ya Yesu msalabani, ni ikiwa kitu hicho kinakuwa sanamu inayotumiwa kwa ibada (1 Wakorintho 10:14) au ikiwa anayevaa anaadhiriwa na jinsi vito hivyo vinamfanya aonekana (1 Petro 3:3) au ikiwa vitakuwa kikwazo kwa wengine (1 Wakorintho 8:9; Warumi 14:13). Watu wengi huvaa vito vya kidini kama urembo bila kujishughulisha na ishara yake au hamu ya kumwakilisha Kristo. Lakini hiyo haimaanishi kuwa Wakristo hawawezi au hawapaswi kuvivaa. Wakristo wengi huvaa misalaba kama onyesho la fahari la upendo wao, heshima, na huduma kwa Kristo, pamoja na ukumbusho wa kile alichotufanyia.

Jambo la kusikitisha ni wakati watu wanaporuhusu vitu kama vile misalaba, sanamu za Yesu msalabani, vinyago, vibandiko vikubwa, n.k. kuchukua nafasi ya badiliko halisi ambalo linastahili kufanyika katika mioyo yetu. Vitu tunavyovaa, kubeba, au kubandika kwenye magari yetu, sivyo vinatufanya kuwa Wakristo. Mungu hajalishwi na mavazi, maadamu hatuvai kwa njia ambayo itamfanya mtu ajikwae katika kutembea kwake na Mungu (Warumi 14:20) na hatujajishughulisha sana namna tunavyoonekana au na mali yetu. Anachunguza mioyo yetu ili kupata ni nani aliye mwaminifu kwake na ikiwa tunahimiza na kuwaonyesha wengine upendo. Haifai yeyote kati yetu kuhukumu iwapo kuvalia mapambo ya vito ya kidini ni bora au la; kila Mkristo lazima atafute kibali cha Mungu katika yote anayoyafanya. Ikiwa haijaainishwa waziwazi katika Maandiko ikiwa jambo ni halali au ni la kujenga, basi jambo hilo ni bora zaidi kuachiwa dhamiri ya kila mtu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mkristo anapaswa kuvaa mapambo ya vito ya kidini, kama vile sanamu ya Yesu Kristo msalabani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries