settings icon
share icon
Swali

Ni nini maana ya maombi ya kutembea? Je, ni kibiblia kushiriki kwa maombi ya kutembea?

Jibu


Maombi ya kutembea ni mazoezi ya kuomba kwa eneo, aina ya maombezi ambayo inahusisha kutembea kwa au karibu na mahali fulani wakati unaomba. Baadhi ya watu wanaamini kwamba kuwa karibu na eneo inaruhusu wao "kuomba karibu na kuomba wazi." Matembezi Maombi ni huchukuliwa na watu binafsi, makundi, na hata kanisa nzima. Yanaweza kuwa ya karibu mfano ukuta mmoja au maili nyingi tuwesavyo. Wazo ni kutumia hisia tano, kusikia, kunusa, ladha, na kugusa kusidisha uelewefu wa mwombezi juu ya haja ya sala.

Kwa mfano, ukitembea masingira yako ukitafuta mambo ya kuombea, unaweza fikia uwanja ambao sio safi. Hii inaweza kusukuma kuomba kwa ajili ya afya, yankimwili na kiroho, na ya wakaazi. Baadhi ya makundi ya sala ya kutembea Shuleni, na hivyo husababisha maombi kwa ajili ya walimu na wanafunzi walio ndani, kwa usalama wao na amani, na kwa ajili ya njama za shetani katika shule yao itibuliwe. Baadhi ya watu uhisi wanaweza kujihusisha na kuelekeza maombi yao kwa ufanisi zaidi kwa kutembea karibu na watu na maeneo wanaombfa.

Maombi ya kutembea ni suala jipya, asili yake haijulikani vuzuri. Hakuna mfano wa kibiblia kwa maombi ya kutembea, ingawa tangu kutembea kulikuwa njia pekee ya usafiri katika nyakati za Biblia, ni wazi watu lazima walitembea wakiomba kwa wakati mmoja. Hata hivyo, hakuna amri ya moja kwa moja kwamba maombi ya kutembea ni jambo tunapaswa kufanya. Kuamini kwamba sala inayotolewa katika mazingira yoyote, au wakati wa nafasi yoyote, ni bora zaidi kuliko zile zinazotolewa wakati mwingine au katika namna nyingine sio kimaandiko. Aidha, huku tunaweza kuhisi tunahitaji kuwa karibu na eneo au hali ili tuombe vizuri zaidi, Baba yetu wa mbinguni, ambaye yu kila mahali wakati wote, anayejua hasa mahitaji ambayo yako sasa hivi na atayajibu kwa mapenzi na majira yake kamili. ukweli kwamba Yeye anaturuhusu sisi kuwa sehemu ya mipango yake kupitia maombi yetu ni kwa faida yetu, si yake.

Tumeamriwa "kuomba bila kukoma" (1 Wathesalonike 5:17), na tangu kutembea ni kitu sisi hufanya kila siku, hakika sehemu moja ya kuomba bila kukoma ni kuomba wakati tunatembea. Mungu anasikia maombi yote yanayotolewa na wale ambao hukaa katika Kristo (Yohana 15:7), bila kujali muda, mahali, au nafasi. Wakati huo huo, hakuna amri dhidi ya maombi ya kutembea, na chochote hutusukuma kuomba chastahili kutiliwa maanani.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Maombi ya matembezi ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries